MENU

SEARCH HERE/ TAFUTA HAPA

Wednesday, February 24, 2021

TAMTHILIA YA KIGOGO: SUMU YA NYOKA

TAMTHILIA YA KIGOGO: ATHARI YA SUMU YA NYOKA SAGAMOYO

#Wasiliana nasi. Bonyeza hapa

 


Athari za sumu ya nyoka

1)    Vifo- Ngao junior

2)    Watu wanageuka vipofu-Mngweni kwa mama pima

3)    Ukengeushi mf. Ngurumo

4)    Kuanguka chini ovyo ovyo na kugaragara-walevi mangweni

5)    Wanafunzi katika shule ya Majoka wamegeuka vichwa  maji- ni makabeji

6)    Walevi hawafahamu athari za ulevi.

7)    Hawaoni athari ya soko kufungwa- Chapakazi

8)    Kupotosha vijana ( gume gume)

9)    Kupotoka kwa maadili

10)Kuvunjika kwa ndoa

 #Nunua Mitihani@Kshs. 100

11)Waathiriwa wanatumiwa na viongozi kutekeleza maovu mf. Ngurumo kumvinja Tunu muundi.

12)Utepetevu ( uzembe) wanashinda ulevini na kupoteza muda.

13)Kuwaunga mkono viongozi  wasiowajibika baada ya kupewa vipeni. ( vibaraka) kama vile Ngurumo

14)Kutumia lugha chafu/ matusi mf Ngurumo kumtusi Tunu.

15)Kukosa wachumba/ ukapera mf Ngurumo

16)Dharau-Ngurumo kumdharau Tunu na kumwimbia wimbo wa Kuolewa-wa Daudi Kabaka

17)Kufuja pesa

18)Kutofuata maagizo – Chopi hakufuata maagizo ya kumuua Tanu.

 #TAZAMA MADA YA ZIADA KWENYE YOUTUBE

1. CHOZI LA HERI

2. TUMBO LISILOSHIBA

3. KIGOGO

4. FASIHI SIMULIZI

TOA MAONI HAPA KWENYE SEHEMU YA MAONIπŸ‘‡

Sunday, February 14, 2021

UJUMBE WA DHARURA KWA WALIMU WOTE

 

UJUMBE WA DHARURA KWA WAKUFUNZI WOTE

Ni mwaka mpya ambapo mchakato wa mafunzo umeanzishwa tena rasmi baada ya kusitishwa mwaka uliopita kutokana na janga la tandavu la Korona. Katika wiki chache ambazo tumekuwa tukitimiza malengo yetu kwa kuwahudumia wanafunzi kwa njia ya mafunzo, tumeshuhudia ukatili miongoni mwa mwao katika baadhi ya shule humu nchini. Ukatili huu umehatarishs maisha ya walimu katika shule husika. Ni muhimu kutambua kwamba usalama wako ni muhimu sana, kwa hivyo huna budi kuusisitizia. Zifuatazo ni njia ambazo kulingana nami, zitaweza kutusaidia kuepuka ukatili na udhalimu wa wanafunzi.

Zingatia jukumu kuu ambalo uliajiriwa kutekeleza. Iwapo umesahau, rejelea barua yako ya kazi kutoka kwa tume ya kuajiri walimu. Kila mara hakikisha kwamba umetimiza jukumula kutimiza jukumu lako, na kwa kiwango kinashoridhisha matarajio yako, ya mwajiri na ya jamii. Kukosa kutimiza jukumu huweza ukazua uhasama wa wanafunzi dhidi yako, jambo ambalo huenda likatishia usalama wako. Wanafunzi wa sasa japo wamepungukiwa na motisha ya kujituma masomoni kutokana na athari za mienendo na maisha ya kijamii, wanatambua wakati ambapo wanapokea huduma bora kutoka kwa Mwalimu na wakati ambapo wanapokea bora huduma.

Je, sheria inakupa nguvu za kumwadhibu mwanafunzi? La. Ni muhimu kila mkufunzi kufahamu fika kwamba sote (walimu na wanafunzi) tuko katika karne ambayo mawasiliano hayana vizingiti. Yanapenya na kupokelewa na kila rika. Kwa hivyo tusipuuze ukweli kwamba wanafunzi hawa wanafahamu kwamba adhabu ni kinyume cha sharia. Wakati mwingine unaweza ukagundua kuwa mwanafunzi anapuuza hitaji lako la kumwadhibu akijua kwamba unakiuka sharia.Wewe kama mkufunzi huenda ukakerwa na jambo hili. Kabla hasira hazijakutawala, hebu jiulize iwapo kumpa mwanafunzi adhabu nimoja kati ka majukumu uliyokabidhiwa na tume.

Kupitia masomo ya saikolojia kwenye vyuo mbalimbali tulikosomea ualimu, kila mwalimu aliyekuwa makini kwa masomo hayo bila shaka anapaswa kuwa na uwezo wa kutambua ama kung’amua fikra za wanafunzi kutokana na jinsi wanavyozungumza ama kutenda mambo yao. Iwapo umegundua kisicho kawaida katika tabia na mienendo ya mwanafunzi, kinachoweza kuhatarisha maisha yako, kumbuka kuwa ni muhimu kutahadhari kabla ya hatari. Kwa mfano, ukimwona mwanafunzi na kifaa kisichohitajika shuleni kama kisu, chukua hatua kwa kufuata mchakato unaofaa ili apikonywe kifaa hicho.

Mwanafunzi anapojeruhiwa ama kwa behati mbaya, anapokufa mikonomi mwa Mwalimu, magari makubwa makubwa huja skulini kumchukulia hatua mkufunzi husika. Mwalimu anapopitia yayo hayo mikononi mwa wanafunzi, ni muhali kuona wakuu wakija kuwachukulia wanafunzi hatua. Hili ni thibitisho tosha kwamba wewe kama Mwalimu, kila mja anaamini kuwa unauwezo wa kujilinda na kujihakikishia usalama wako. Kwa hiyo tambua kwamba usalama wako unakutegemea wewe mwenyewe.

Kwa jumla, wazo langu kihusu usalama wa Mwalimu ni kwamba usalama huo unamtegemea Mwalimu mwnyewe. Kwanza, epuka matendo ambayo huenda yakazua uhasama kati yako na wanagenzi. Pili, fahamu fika jukumu lako na ulitimize ipasayvo. Tatu, chunguza na utambue tabia hasi miongoni mwa wanafunzi ambazo huenda zikaangamiza usalama wako, kisha chukua hatua kuzikomesha. Mwisho, unauwezo wa kujihakikishia usalama na kujilinda. Jilinde.