SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI
SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI
MAANA YA SHAMIRISHO:
AINA ZA SHAMIRISHO
1. Shamirisho Kipozi/ Yambwa Tendwa
2. Shamirisho Kitondo/ Yambwa Tendewa/yambiwa
3. Shamirisho Ala/ Kitumizi
------------------------------------------------------------------------------
1. SHAMIRISHO KIPOZI
Ni nomino anayopokea athari ya kitendo moja kwa moja.
Mara nyingi hipatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kutenda, japo huwezakupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli zingine.
Mifano
- Wizara ya elimu inarekebisha mtaala. (mtaala-shamirisho kipozi)
- Mkulima analima shamba. (shamba-shamirisho kipozi)
- Mgonjwa aliletewa chai kwa chupa na Swaleh.
- Kitabu cha mwanafunzi kimepotezwa na mtoto.
- Kipenga cha mkufunzi kitanunuliwa wiki ijayo na mwalimu mkuu.
- Mzazi alimnunulia mwanawe baiskeli kwa kupita mtihani.
- Kaka atamfyekea babu yangu shamba baada ya kutoa mahindi.
- Nina alimpikia mgonjwa chakula chenye ladha tamu.
- Walimu waliwekewa runinga kwanye afisi yao.
- Mwanasiasa alipigiwa kura na kushinda uchaguzi mdogo wa mkoa.
- Kaka alilima shamba lake kwa jembe jipya.
- Mpishi alikata vitunguu na nyanya kwa kisu.
- Mwalimu alisahihisha vitabu vya wanafunzi kwa kalamu.
- Juma alisafiri ughaibuni kwa ndege.
- Viwanja vilinunuliwa kwa pesa
- Mkongwe atajengewa nyumba ya mbao.