BLOG VISITORS

Showing posts with label jukumu. Show all posts
Showing posts with label jukumu. Show all posts

Tuesday, July 22, 2025

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI (KIPOZI, KITONNDO, NA ALA)

 

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

MAANA YA SHAMIRISHO:

Shamirisho ni neno ambalo huashiria nomino inayopokea kitendo (kitendwa/mtendwa), nonimo inayofaidika kutokana na kitendo (kitendewa/mtendewa), na kifaa kinachotumika katika kitendo (ala), katika sentensi.

AINA ZA SHAMIRISHO

1. Shamirisho Kipozi/ Yambwa Tendwa

2. Shamirisho Kitondo/ Yambwa Tendewa/yambiwa

3. Shamirisho Ala/ Kitumizi

------------------------------------------------------------------------------

1. SHAMIRISHO KIPOZI

Pia huitwa yambwa tendwa (Direct object).
Ni nomino anayopokea athari ya kitendo moja kwa moja.
Mara nyingi hipatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kutenda, japo huwezakupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli zingine.

Mifano

  1. Wizara ya elimu inarekebisha mtaala. (mtaala-shamirisho kipozi)
  2. Mkulima analima shamba.  (shamba-shamirisho kipozi)
  3. Mgonjwa aliletewa chai kwa chupa na Swaleh. 
  4. Kitabu cha mwanafunzi kimepotezwa na mtoto.
  5. Kipenga cha mkufunzi kitanunuliwa wiki ijayo na mwalimu mkuu.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
2. SHAMIRISHO KITONDO
Pia huitwa yambwa tendewa au yambiwa (Indirect Object).
Ni nomino ambayo huathiriwa na kitendo kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Huathiriwa na kitendo kinacho tendwa kwa shamirisho kipozi.
Hupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kitendea/ kutendewa.

Mifano
  1. Mzazi alimnunulia mwanawe baiskeli kwa kupita mtihani.
  2. Kaka atamfyekea babu yangu shamba baada ya kutoa mahindi.
  3. Nina alimpikia mgonjwa chakula chenye ladha tamu.
  4. Walimu waliwekewa runinga kwanye afisi yao.
  5. Mwanasiasa alipigiwa kura na kushinda uchaguzi mdogo wa mkoa.
----------------------------------------------------------------------
3. SHAMIRISHO ALA/ KITUMIZI
Ni nomino ambayo hurejelea kifaa kinachotumiwa kitekeleza kitendo fulani.
Huwakilishwa na vielezi vya namna ala.
KUMBUKA: "kwa" si sehemu ya shamirisho ala.

Mifano
  1. Kaka alilima shamba lake kwa jembe jipya.
  2. Mpishi alikata vitunguu na nyanya kwa kisu.
  3. Mwalimu alisahihisha vitabu vya wanafunzi kwa kalamu.
  4. Juma alisafiri ughaibuni kwa ndege.
  5. Viwanja vilinunuliwa kwa pesa
  6. Mkongwe atajengewa nyumba ya mbao.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
SHUKRAN KWA USOMAJI WAKO πŸ™πŸ‘πŸ˜Ž

UNA SWALI KUHUSU SHAMIRISHO KIPOZI, KITONDO, AMA SHAMIRISHO ALA?
ULIZA HAPA CHINI πŸ‘‡πŸ‘‡


Sunday, February 14, 2021

UJUMBE WA DHARURA KWA WALIMU WOTE

 

UJUMBE WA DHARURA KWA WAKUFUNZI WOTE

Ni mwaka mpya ambapo mchakato wa mafunzo umeanzishwa tena rasmi baada ya kusitishwa mwaka uliopita kutokana na janga la tandavu la Korona. Katika wiki chache ambazo tumekuwa tukitimiza malengo yetu kwa kuwahudumia wanafunzi kwa njia ya mafunzo, tumeshuhudia ukatili miongoni mwa mwao katika baadhi ya shule humu nchini. Ukatili huu umehatarishs maisha ya walimu katika shule husika. Ni muhimu kutambua kwamba usalama wako ni muhimu sana, kwa hivyo huna budi kuusisitizia. Zifuatazo ni njia ambazo kulingana nami, zitaweza kutusaidia kuepuka ukatili na udhalimu wa wanafunzi.

Zingatia jukumu kuu ambalo uliajiriwa kutekeleza. Iwapo umesahau, rejelea barua yako ya kazi kutoka kwa tume ya kuajiri walimu. Kila mara hakikisha kwamba umetimiza jukumula kutimiza jukumu lako, na kwa kiwango kinashoridhisha matarajio yako, ya mwajiri na ya jamii. Kukosa kutimiza jukumu huweza ukazua uhasama wa wanafunzi dhidi yako, jambo ambalo huenda likatishia usalama wako. Wanafunzi wa sasa japo wamepungukiwa na motisha ya kujituma masomoni kutokana na athari za mienendo na maisha ya kijamii, wanatambua wakati ambapo wanapokea huduma bora kutoka kwa Mwalimu na wakati ambapo wanapokea bora huduma.

Je, sheria inakupa nguvu za kumwadhibu mwanafunzi? La. Ni muhimu kila mkufunzi kufahamu fika kwamba sote (walimu na wanafunzi) tuko katika karne ambayo mawasiliano hayana vizingiti. Yanapenya na kupokelewa na kila rika. Kwa hivyo tusipuuze ukweli kwamba wanafunzi hawa wanafahamu kwamba adhabu ni kinyume cha sharia. Wakati mwingine unaweza ukagundua kuwa mwanafunzi anapuuza hitaji lako la kumwadhibu akijua kwamba unakiuka sharia.Wewe kama mkufunzi huenda ukakerwa na jambo hili. Kabla hasira hazijakutawala, hebu jiulize iwapo kumpa mwanafunzi adhabu nimoja kati ka majukumu uliyokabidhiwa na tume.

Kupitia masomo ya saikolojia kwenye vyuo mbalimbali tulikosomea ualimu, kila mwalimu aliyekuwa makini kwa masomo hayo bila shaka anapaswa kuwa na uwezo wa kutambua ama kung’amua fikra za wanafunzi kutokana na jinsi wanavyozungumza ama kutenda mambo yao. Iwapo umegundua kisicho kawaida katika tabia na mienendo ya mwanafunzi, kinachoweza kuhatarisha maisha yako, kumbuka kuwa ni muhimu kutahadhari kabla ya hatari. Kwa mfano, ukimwona mwanafunzi na kifaa kisichohitajika shuleni kama kisu, chukua hatua kwa kufuata mchakato unaofaa ili apikonywe kifaa hicho.

Mwanafunzi anapojeruhiwa ama kwa behati mbaya, anapokufa mikonomi mwa Mwalimu, magari makubwa makubwa huja skulini kumchukulia hatua mkufunzi husika. Mwalimu anapopitia yayo hayo mikononi mwa wanafunzi, ni muhali kuona wakuu wakija kuwachukulia wanafunzi hatua. Hili ni thibitisho tosha kwamba wewe kama Mwalimu, kila mja anaamini kuwa unauwezo wa kujilinda na kujihakikishia usalama wako. Kwa hiyo tambua kwamba usalama wako unakutegemea wewe mwenyewe.

Kwa jumla, wazo langu kihusu usalama wa Mwalimu ni kwamba usalama huo unamtegemea Mwalimu mwnyewe. Kwanza, epuka matendo ambayo huenda yakazua uhasama kati yako na wanagenzi. Pili, fahamu fika jukumu lako na ulitimize ipasayvo. Tatu, chunguza na utambue tabia hasi miongoni mwa wanafunzi ambazo huenda zikaangamiza usalama wako, kisha chukua hatua kuzikomesha. Mwisho, unauwezo wa kujihakikishia usalama na kujilinda. Jilinde.

 

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI (KIPOZI, KITONNDO, NA ALA)

  SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI MAANA YA SHAMIRISHO : Shamirisho ni neno ambalo huashiria nomino inayopokea kitend...