BLOG VISITORS

Showing posts with label matumizi ya lugha. Show all posts
Showing posts with label matumizi ya lugha. Show all posts

Tuesday, July 22, 2025

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI (KIPOZI, KITONNDO, NA ALA)

 

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

MAANA YA SHAMIRISHO:

Shamirisho ni neno ambalo huashiria nomino inayopokea kitendo (kitendwa/mtendwa), nonimo inayofaidika kutokana na kitendo (kitendewa/mtendewa), na kifaa kinachotumika katika kitendo (ala), katika sentensi.

AINA ZA SHAMIRISHO

1. Shamirisho Kipozi/ Yambwa Tendwa

2. Shamirisho Kitondo/ Yambwa Tendewa/yambiwa

3. Shamirisho Ala/ Kitumizi

------------------------------------------------------------------------------

1. SHAMIRISHO KIPOZI

Pia huitwa yambwa tendwa (Direct object).
Ni nomino anayopokea athari ya kitendo moja kwa moja.
Mara nyingi hipatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kutenda, japo huwezakupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli zingine.

Mifano

  1. Wizara ya elimu inarekebisha mtaala. (mtaala-shamirisho kipozi)
  2. Mkulima analima shamba.  (shamba-shamirisho kipozi)
  3. Mgonjwa aliletewa chai kwa chupa na Swaleh. 
  4. Kitabu cha mwanafunzi kimepotezwa na mtoto.
  5. Kipenga cha mkufunzi kitanunuliwa wiki ijayo na mwalimu mkuu.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
2. SHAMIRISHO KITONDO
Pia huitwa yambwa tendewa au yambiwa (Indirect Object).
Ni nomino ambayo huathiriwa na kitendo kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Huathiriwa na kitendo kinacho tendwa kwa shamirisho kipozi.
Hupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kitendea/ kutendewa.

Mifano
  1. Mzazi alimnunulia mwanawe baiskeli kwa kupita mtihani.
  2. Kaka atamfyekea babu yangu shamba baada ya kutoa mahindi.
  3. Nina alimpikia mgonjwa chakula chenye ladha tamu.
  4. Walimu waliwekewa runinga kwanye afisi yao.
  5. Mwanasiasa alipigiwa kura na kushinda uchaguzi mdogo wa mkoa.
----------------------------------------------------------------------
3. SHAMIRISHO ALA/ KITUMIZI
Ni nomino ambayo hurejelea kifaa kinachotumiwa kitekeleza kitendo fulani.
Huwakilishwa na vielezi vya namna ala.
KUMBUKA: "kwa" si sehemu ya shamirisho ala.

Mifano
  1. Kaka alilima shamba lake kwa jembe jipya.
  2. Mpishi alikata vitunguu na nyanya kwa kisu.
  3. Mwalimu alisahihisha vitabu vya wanafunzi kwa kalamu.
  4. Juma alisafiri ughaibuni kwa ndege.
  5. Viwanja vilinunuliwa kwa pesa
  6. Mkongwe atajengewa nyumba ya mbao.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
SHUKRAN KWA USOMAJI WAKO πŸ™πŸ‘πŸ˜Ž

UNA SWALI KUHUSU SHAMIRISHO KIPOZI, KITONDO, AMA SHAMIRISHO ALA?
ULIZA HAPA CHINI πŸ‘‡πŸ‘‡


Wednesday, June 9, 2021

VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021

VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021

Subscribe to our Youtube Channel for updates on CHECHE ZA MOTO analysis videos and other updates
Click here> YouTube


Wizara ya Elimu imeidhinisha vitabu vipya vya fasihi andishi vitakavyosomwa, kuchambuliwa na kutahiniwa katika shule za upili kote nchini.

CHECHE ZA MOTO iliyoandikwa na John Habwe na kuchapishwa na Jomo Kenyatta Foundation (JKF) ndiyo riwaya ambayo itachukua nafasi ya riwaya ya Chozi la Heri ya Asumpta K. Matei.

Hadithi fupi, MAPAMBAZUKO YA MACHWEO iliyochapishwa na kampuni ya ushapishaji ya Mountain Top ndiyo itachukua nafasi ya Tumbo Lisiloshiba na hadithi nyingine iliyohaririwa na Alifa Chokocho na Dumu Kayanda.

Wizara ya elimu imeidhinisha vitabu hivi baada ya miaka minne ya kutahiniwa kwa Chozi la Heri na Tumbo Lisiloshiba. 

Wakufunzi wameelezea matarajio makuu kwamba Cheche za Moto huenda ikawa nyepesi kwa wanafunzi kuelewa hasa kwa kuzingatia mtitiriko wa vitushi na idadi ya wahusika. Baadhi ya walimu wamedokeza kwamba riwaya inayoondoka imekuwa changamoto kwao na kwa wanafunzi kwa sababu imeshishirikisha wahusika chungu nzima. Vilevile, walimu hao wameeleza kwamba riwaya Chozi la Heri imekuwa na uchangamano mwingi katika muundo wake.

Kwa upande mwingine, wanafunzi waliohojiwa na Homeschool Kenya wamepongeza watunzi mbalimbali wa hadithi katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba. Wanafunzi hao wamedokeza kwamba hadithi hizo mbali na kuburudisha, zimesheheni ujumbe muhimu kwa wanafunzi wote. Nilipowauliza kuhusu changamoto walizokumbana nazo katika usomaji wao wa Tumbo Lisiloshiba, wanafunzi hao walisisitiza kwamba hadithi hizo zimekuwa nyepesi kuelewa.

Tunashughulikia uchambuzi wa Cheche za Moto na Mapambazuko ya Machweo na baada ya siku chache tutachapisha makala hayo humu kwenye blogu kwa manufaa yetu sote. Ahsanteni.


Wasiliana nasi Kupitia WhatsApp. 

Kwa makala mengine gusa yafuatayo:


 

Thursday, July 16, 2020

SARUFI KIKORONA


MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
(a) Linanisha na utofautishe sauti zifuatazo           (al.2)
     (i) /th/,/dh/

(c) Tunga sentensi inayodhihirisha           (al.4)
  (i) Nomino ya wingi
  (ii) Kitenzi kishirikishi kuipungufu

(d) Tumia jozi ya maneno yafuatayo kutunga sentenzi moja    (al.2)
  Fumba na vumba

(e) Tofautisha matumizi ya ngali katika sentenzi zifuatazo; (al.2)
      (i) Wanafunzi wangali wanasherehekea
  (ii) Wanafunzi wetu wangalisoma wangalipita mtihani

(f) Tumia ‘O’ rejeshi ili kudhihirisha hali ya mazoea      (al.2)
  Mgonjwa ambaye anakula lishe bora ndiye ambaye atapona haraka

(g) Bainisha aina za virai katika sentensi ifuatayo        (al.3)
   Walimshangilia mgeni wao kwa shangwe

(h) Ainsha viambishi katika neno lifuatalo         (al.3)
   Tutakayempiga

(i) Bianisha aina za yambwa katika sentensi ifuatayo               (al.3)
    Mkulima aliyekata nyasi kwa mundu amewalisha punda

(k) Andika katika usemi halisi                     (al.2)
  Robi alisema kuwa ilikuwa lazima wao waonyeshe heshima kwa watu wote ikiwa walitaka    kuendelea vyema maishani.

(i) Sahihisha sentensi zifuatazo                   (al.2)
   (i) Mbona haujaenda sokoni
(ii) Penye niliandika ni hapo

(m) Andika katika ukubwa              (al.2)
  Wazee hawa wana wake na watoto wengi

(n) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya visanduku         (al.3)
   Motto aliyekamatwa jana ni mwizi

(o) Unda nomino mbili kutokana na kitenzi ‘chuma’   (al.2)

(p) Andika kinyume cha: (al.2)
  Furaha anajenga nyumba mjini                                                                                                   
(q) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendeshea na kutendeshwa                            (al.2)
    (i) Fa
   (ii) Nywa

(r) Kanusha sentensi ifuatayo                      (al.1)
  Ningelikuwa na pesa ningelinunua kitanu kile

   ISIMU JAMII (Alama 10)

     Eleza kwa kutolea mifano dhana zofuatazo
     (a) Sajili

     (b) Lafudhi

     (c) Lahaja

     (d) Lingua franka

     (e) Krioli







Tuesday, June 16, 2020

MIUNDO YA NOMINO KATIKA NGELI ZA KISWAHILI


MIUNDO YA NOMINO KATIKA NGELI ZA KISWAHILI
Maana ya ngeli
Ngeli ni makundi mbalimbali ambapo maneno ya Kiswahili yamegwaika. Ni migawo mbalimbali ya maneno ya Kiswahili.

Tanbihi: Katika othografia/ maandishi, ngeli huandikwa kwa herufi kubwa.
Makala haya yanashughulikia miundo mbalimbali ya maneno katika baadhi ya ngeli za Kiswahili.

Ni wazi kwamba maneno tofautitofauti katika ngeli mahususi huchukua maumbo mbalimbali tofauti. Makala haya yanashughulikia maumbo hayo tofauti ya maneno katika ngeli.



NGELI YA A-WA

1.     Muundo wa M-WA- maneno haya huanza kwa M katika umoja na WA katika wingi. Mfano,
mtoto
watoto
mjomba
Wajomba
mwana
Wana
mzee
Wazee
mtemi
watemi

2.     Muundo wa CH-VY. Maneno haya huanza na CH katika umoja VY katika wingi. Mfano,

chura
Vyura



3.     Muundo wa M-MI.

NGELI YA LI-YA

KWA NGELI ZINGINEZO, BONYEZA HAPA

NGELI ZILIZISHUGHULIKIWA:

A-WA
LI-YA
U-ZI
KI-VI
U-I
I-I









Uliza swali moja kwa moja kupitia <WHATSAPP>



SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI (KIPOZI, KITONNDO, NA ALA)

  SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI MAANA YA SHAMIRISHO : Shamirisho ni neno ambalo huashiria nomino inayopokea kitend...