BLOG VISITORS

Friday, July 17, 2020

USHAIRI KIKORONA

            

         Soma shairi lifuatalo kwa kina kisha ujibu maswali yanayofuata

1.         Natunga nikiwaasa, msije kujijutia,
Mitego sije wanasa, mkaja kuangamia
Tamaa nyingi za pesa, gereza, zitawatia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


2.         Jela inamkonyeza, kama hutajizuwia
Haina ndugu gereza, jela si ya kuchezea,
Inajuvya na kupoza, wenye nguvu kutulia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


3.         Rushwa si kitu chema, walaji jihadharini,
Mkila zitawakwama, zitawatoka puwani,
Wazilao hulalama, si mimi ila Fulani
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


4.         Ridhika na upatacho, kama moja au mbili,
Usitaraji mkocho, upatao, bwana Ali,
Tama zako za macho, zitakulea mbuli
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


5.         Ni mema kemukemu, wenye vyeo kutumia
Maleba wakiwahimu, rushwa kuwaletea,
Muogopeni karimu, leba haombwi rushwa,
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza

6.         Kuna wengi mahakimu, haki wanazopinduwa,
Yatima huwa dhulumu, kwa kupapia rushwa
Kwa kutaka darahimu, aso haki anapewa
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza

Maswali
(a)   Andika kichwa mwafaka cha shairi hili .                                                                  (al.1)
(b)   Taja madhara manne ya rushwa.                                                                               (al.4)
(c)   Eleza  umbo la shairi hili.                                                                                          (al.4)
(d)  Andika ubeti wanne katika lugha nathari.                                                                 (al4)
(e)   Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika shairi hili.                      (al.3)

(f)   Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili .                        (al.4)
(i)              Gereza
(ii)            Mkocho
(iii)          Karimu
(iv)          Darahimu



Thursday, July 16, 2020

SARUFI KIKORONA


MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
(a) Linanisha na utofautishe sauti zifuatazo           (al.2)
     (i) /th/,/dh/

(c) Tunga sentensi inayodhihirisha           (al.4)
  (i) Nomino ya wingi
  (ii) Kitenzi kishirikishi kuipungufu

(d) Tumia jozi ya maneno yafuatayo kutunga sentenzi moja    (al.2)
  Fumba na vumba

(e) Tofautisha matumizi ya ngali katika sentenzi zifuatazo; (al.2)
      (i) Wanafunzi wangali wanasherehekea
  (ii) Wanafunzi wetu wangalisoma wangalipita mtihani

(f) Tumia ‘O’ rejeshi ili kudhihirisha hali ya mazoea      (al.2)
  Mgonjwa ambaye anakula lishe bora ndiye ambaye atapona haraka

(g) Bainisha aina za virai katika sentensi ifuatayo        (al.3)
   Walimshangilia mgeni wao kwa shangwe

(h) Ainsha viambishi katika neno lifuatalo         (al.3)
   Tutakayempiga

(i) Bianisha aina za yambwa katika sentensi ifuatayo               (al.3)
    Mkulima aliyekata nyasi kwa mundu amewalisha punda

(k) Andika katika usemi halisi                     (al.2)
  Robi alisema kuwa ilikuwa lazima wao waonyeshe heshima kwa watu wote ikiwa walitaka    kuendelea vyema maishani.

(i) Sahihisha sentensi zifuatazo                   (al.2)
   (i) Mbona haujaenda sokoni
(ii) Penye niliandika ni hapo

(m) Andika katika ukubwa              (al.2)
  Wazee hawa wana wake na watoto wengi

(n) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya visanduku         (al.3)
   Motto aliyekamatwa jana ni mwizi

(o) Unda nomino mbili kutokana na kitenzi ‘chuma’   (al.2)

(p) Andika kinyume cha: (al.2)
  Furaha anajenga nyumba mjini                                                                                                   
(q) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendeshea na kutendeshwa                            (al.2)
    (i) Fa
   (ii) Nywa

(r) Kanusha sentensi ifuatayo                      (al.1)
  Ningelikuwa na pesa ningelinunua kitanu kile

   ISIMU JAMII (Alama 10)

     Eleza kwa kutolea mifano dhana zofuatazo
     (a) Sajili

     (b) Lafudhi

     (c) Lahaja

     (d) Lingua franka

     (e) Krioli







SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...