BLOG VISITORS

Showing posts with label shamirisho kipozi. Show all posts
Showing posts with label shamirisho kipozi. Show all posts

Tuesday, July 22, 2025

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI (KIPOZI, KITONNDO, NA ALA)

 

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

MAANA YA SHAMIRISHO:

Shamirisho ni neno ambalo huashiria nomino inayopokea kitendo (kitendwa/mtendwa), nonimo inayofaidika kutokana na kitendo (kitendewa/mtendewa), na kifaa kinachotumika katika kitendo (ala), katika sentensi.

AINA ZA SHAMIRISHO

1. Shamirisho Kipozi/ Yambwa Tendwa

2. Shamirisho Kitondo/ Yambwa Tendewa/yambiwa

3. Shamirisho Ala/ Kitumizi

------------------------------------------------------------------------------

1. SHAMIRISHO KIPOZI

Pia huitwa yambwa tendwa (Direct object).
Ni nomino anayopokea athari ya kitendo moja kwa moja.
Mara nyingi hipatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kutenda, japo huwezakupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli zingine.

Mifano

  1. Wizara ya elimu inarekebisha mtaala. (mtaala-shamirisho kipozi)
  2. Mkulima analima shamba.  (shamba-shamirisho kipozi)
  3. Mgonjwa aliletewa chai kwa chupa na Swaleh. 
  4. Kitabu cha mwanafunzi kimepotezwa na mtoto.
  5. Kipenga cha mkufunzi kitanunuliwa wiki ijayo na mwalimu mkuu.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
2. SHAMIRISHO KITONDO
Pia huitwa yambwa tendewa au yambiwa (Indirect Object).
Ni nomino ambayo huathiriwa na kitendo kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Huathiriwa na kitendo kinacho tendwa kwa shamirisho kipozi.
Hupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kitendea/ kutendewa.

Mifano
  1. Mzazi alimnunulia mwanawe baiskeli kwa kupita mtihani.
  2. Kaka atamfyekea babu yangu shamba baada ya kutoa mahindi.
  3. Nina alimpikia mgonjwa chakula chenye ladha tamu.
  4. Walimu waliwekewa runinga kwanye afisi yao.
  5. Mwanasiasa alipigiwa kura na kushinda uchaguzi mdogo wa mkoa.
----------------------------------------------------------------------
3. SHAMIRISHO ALA/ KITUMIZI
Ni nomino ambayo hurejelea kifaa kinachotumiwa kitekeleza kitendo fulani.
Huwakilishwa na vielezi vya namna ala.
KUMBUKA: "kwa" si sehemu ya shamirisho ala.

Mifano
  1. Kaka alilima shamba lake kwa jembe jipya.
  2. Mpishi alikata vitunguu na nyanya kwa kisu.
  3. Mwalimu alisahihisha vitabu vya wanafunzi kwa kalamu.
  4. Juma alisafiri ughaibuni kwa ndege.
  5. Viwanja vilinunuliwa kwa pesa
  6. Mkongwe atajengewa nyumba ya mbao.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
SHUKRAN KWA USOMAJI WAKO πŸ™πŸ‘πŸ˜Ž

UNA SWALI KUHUSU SHAMIRISHO KIPOZI, KITONDO, AMA SHAMIRISHO ALA?
ULIZA HAPA CHINI πŸ‘‡πŸ‘‡


Tuesday, June 8, 2021

VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021

 

VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021

Subscribe to our Youtube Channel for updates on CHECHE ZA MOTO analysis videos and other updates
Click here> YouTube
Wizara ya Elimu imeidhinisha vitabu vipya vya fasihi andishi vitakavyosomwa, kuchambuliwa na kutahiniwa katika shule za upili kote nchini.

CHECHE ZA MOTO iliyoandikwa na John Habwe na kuchapishwa na Jomo Kenyatta Foundation (JKF) ndiyo riwaya ambayo itachukua nafasi ya riwaya ya Chozi la Heri ya Asumpta K. Matei.

Hadithi fupi, MAPAMBAZUKO YA MACHWEO iliyochapishwa na kampuni ya ushapishaji ya Mountain Top ndiyo itachukua nafasi ya Tumbo Lisiloshiba na hadithi nyingine iliyohaririwa na Alifa Chokocho na Dumu Kayanda.

Wizara ya elimu imeidhinisha vitabu hivi baada ya miaka minne ya kutahiniwa kwa Chozi la Heri na Tumbo Lisiloshiba. 

Wakufunzi wameelezea matarajio makuu kwamba Cheche za Moto huenda ikawa nyepesi kwa wanafunzi kuelewa hasa kwa kuzingatia mtitiriko wa vitushi na idadi ya wahusika. Baadhi ya walimu wamedokeza kwamba riwaya inayoondoka imekuwa changamoto kwao na kwa wanafunzi kwa sababu imeshishirikisha wahusika chungu nzima. Vilevile, walimu hao wameeleza kwamba riwaya Chozi la Heri imekuwa na uchangamano mwingi katika muundo wake.

Kwa upande mwingine, wanafunzi waliohojiwa na Homeschool Kenya wamepongeza watunzi mbalimbali wa hadithi katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba. Wanafunzi hao wamedokeza kwamba hadithi hizo mbali na kuburudisha, zimesheheni ujumbe muhimu kwa wanafunzi wote. Nilipowauliza kuhusu changamoto walizokumbana nazo katika usomaji wao wa Tumbo Lisiloshiba, wanafunzi hao walisisitiza kwamba hadithi hizo zimekuwa nyepesi kuelewa.

Tunashughulikia uchambuzi wa Cheche za Moto na Mapambazuko ya Machweo na baada ya siku chache tutachapisha makala hayo humu kwenye blogu kwa manufaa yetu sote. Ahsanteni.

πŸ’«
Wasiliana nasi Kupitia WhatsApp. 

Kwa makala mengine gusa yafuatayo:

NEW BOOK: HOW TO GET AND TEACH FOREIGN STUDENTS ONLINE

 NEW BOOK: HOW TO FIND AND TEACH FOREIGN STUDENTS ONLINE Greetings Mwalimu, and welcome to this educational platform, which has been helping...