1. LAZIMA
“Asante ya punda kweli
ni mateke. Sikujua ungekuja kunihangaisha ...”
a) Weka
dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Onyesha
jinsi msemewa anamwangaisha msemaji. (alama 2)
c) Kwa
kurejelea tamthilia nzima onyesha ukweli wa methali “Asante ya punda ni
mateke.” (alama 14)
HADITHI FUPI
Tumbo lisiloshiba na
hadithi nyingine
2. “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu,
maskini na tajiri”
a) Eleza
muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Taja
na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo
hili. (alama
4)
c) Mambo
yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana
? (alama 6)
d) Taja
na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo
hili. (alama 6)
3. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani
ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi
katika malezi. (alama 20)
Kigogo
Tibu
swali la 2 au 3
2. Tusiwaruhusu watu
wachache waliojazwa kasumba….kuturejesha ….hatuwezi kukubali kutawaliwa
kidhalimu
tena.
a. Eleza
muktadha wa dondoo hili.
b. Kwa
kumrejelea mzungumzaji wa maneno haya, bainisha unafiki katika kauli hii. (alama
16)
3. Eleza jinsi
mbinu ya taharuki ilivyotumika kufanikisha maudhui katika tamthilia ya
kigogo. (ala
20)
HADITHI FUPI
Eunice Kimaliro : Mtihani wa
Maisha.
4. “…..ilmuradi mawazo
yanamwadhibu sasa”
a. Eleza
muktadha wa dondoo
hili.
b. Fafanua
sifa za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)
c. Onyesha
mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.
Alfa
Chokocho : Tulipokutana tena
5. a. “
Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza
muktadha wa dondoo hili.
ii) Tathmini
umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi
hii.
b.
Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto
ya Mashaka”
2. “
Do ! Do ! Simameni ! Simameni leo kutanyesha mawe! “
i) Eleza
muktadha wa dondoo hili.
ii) Fafanua mbinu
za lugha zilizotumika katika dondoo
iv) Dhihirisha kwa
kuzingatia hoja sita jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika tamthilia
ya “ Kigogo.” (alama 12)
3) Eleza kwa kutolea
mifano mitano mitano jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu za :
i)
majazi
ii)mbinu
rejeshi
SEHEMU C: HADITHI FUPI
Tumbo
Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
4. i) Sekta ya elimu ina changamoto
nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo : (alama 20)
a) Mapenzi ya Kifaurongo
b)
Shogake dada ana Ndevu
c)
Mwalimu Mstaafu
d)
Mtihani wa maisha
5) ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya
mwenye njaa… ‘’
i) Thibitisha ukweli wa kauli hii
kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo
Lisiloshiba (al
10)
ii) Jadili uhalisia wa hadithi ya
Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja
kumi. (al
10)
6. Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe
macho”.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo
hili.
(c) Ushauri uliotolewa na msemaji baadaye kama njia mojawapo
ya kuwa macho ni wa
kidhalimu. Fafanua. (alama
4)
(d) Eleza namna unafiki wa msemaji na upumbavu wa mnenewa
unavyodhihirika katika muktadha wa dondoo hili.(alama
(e) Onesha jinsi ukweli wa kauli hii ulivyojitokeza baadaye
katika tamthilia.
3. Jadili migogoro
inayojitokeza katika tamthilia ya kigogo, kisha utathmini namna
ilivyosuluhishwa. (alama 20)
SEHEMU
YA C:HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
Jibu swali la 4 au 5
4. “Kesho kama sote
tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo
hili (alama 4)
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika
dondoo hili. (alama 4)
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya (alama
6)
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka
katika bara la Afrika.
Taja mambo sita (alama 6)
5.Ukengeushi huzorotesha
maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya
‘Mkubwa’. (alama 20)
“ Mguu huu ni wako”
· Eleza
muktadha wa dondoo hili (al. 4)
· Ni
tamathali gani ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. Eleza maana yake (al.2)
· Msemewa
alipewa ahadi zipi (al. 5)
· Eleza
sifa na umuhimu wa mzungumzaji (al. 9)
5 Eleza mbinu ya
· Majazi
(al.10)
· Kinaya (al.10)
6. TUMBO
LISILOSHIBA
Kwa kuzingatia hadithi
zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo
lisiloshiba (Diwani)
7 “Kesho panapo
majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu
zinazosimamia juu ya ardhi
hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
b Eleza sifa nne za msemaji (al. 4)
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo
hili (al. 2)
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina
tumbo lisiloshiba (al. 10)
“Oooh bebi, miaka yaenda mbio sana,
nayo sura yako inachujuka……”
a) Weka
dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Mhusika
anayehusishwa na wimbo huu ana msimano gani wa kimapinduzi?( 8)
c) Taja
sifa zozote nane za muhusika huyu (alama 8)
5. Tamthilia
ya ‘Kigogo’ ni kioo cha uhalisia wa maisha ya jamii
nyingi za kiafrika. Thibitisha. (alama
20)
SEHEMU YA
D: HADITHI FUPI TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINEZO
Jibu swali la 6 au la 7
6. “Rasta
twambie bwana!”
a) Weka
dondo katika muktadha (ala 4)
b) Taja
mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (ala 2)
c) Ni
kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe? ( 4)
d) Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya
hadithi hii. (alama10 )
7. Jadili
mashaka ya Mashaka katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka” (alama
20
2. “Kitabu si jalada, fungua ndani usome
mambo. Kitanda
usichokilalia kunguni wake huwajui.”
(i) Eleza
muktadha wa dondoo hili. (al.4)
(ii) Kwa
kurejelea tamthilia ya kigogo, thibitisha ukweli wa
dondoo hili. (al.14)
(ii) Taja tamathali
za usemi zilizotumika katika dondoo hili. (al.2)
3. Eleza
mbinu alizotumia majoka kuendeleza uongozi wake. (al.20)
HADITHI FUPI: TUMBO
LISILOSHIBA.
6.Huku ukirejelea
hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji
wa
haki. (al.20)
Tumbo
lililoshiba na Hadithi nyingine
4. "Penzi lenu na nani? . . . .
Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo
hii. (alama 4)
b) Taja naufafanue mbinu mbili
za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
c)Onyesha vile maudhui ya
utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
d)Eleza sifa sita za
mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)
5. Ilikuwa kama vile katia
saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa
kitanzi.
a)Fafanua tamathali mbili
zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
b)Jadili vipengele vitano vya
sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. (alama 10)
c)Onyesha dhiki
iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo. (alama 6)
KIGOGO Pauline Kea
“Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza
majeraha yao ya kufungiwa soko.”
a) Weka
maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
b) Tambua
mbinu mbili za lugha katika dondoo hili (alama 2)
c) Kando
na kufungiwa soko, Wanasagmoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa
na utawala wa Majoka (alama 5)
d) Fafanua
sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 9)
SEHEMU C: HADITHI FUPI :TUMBO
LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
2. “hebu
sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?
a) Weka
dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Tambua mbinu
tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili na umuhimu wake (alama 6)
c) Onyesha jinsi
dhana ya nzi kufia kidondani inabainika hadithini (alama 4)
d) Hali ya
kutowajibika inajitokeza vipi katika hadithi? (alama 6)
3. Huku
ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana
katika jamii (alama 20)
SHIBE INATUMALIZA -
Salma Omar Hamad.
1. Lazima. (alama
20)
“Hatuwezi
kumaliza kula, kila leo tunakula”
(a)
Eleza mukadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b)
Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika. (alama
2)
(c) Eleza umuhimu wa
mnenaji. (alama 4)
(d) “Lakini nakwambia tena,
kula kunatumaliza” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli
hii. (alama 10)
TAMTHILIA
Pauline
Kea: Kigogo
4. “Shika hamsini zako wewe ... Hatutaki kufanya
nira na mtu ...”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama
4)
(b)
Eleza tamathali ya usemi iliyotumika. (alama 2)
(c)
Uongozi wa Majoka umesheheni sumu ya nyoka.
Thibitisha
kwa kudokeza hoja kumi na nne. (alama 14)
5.Utawala mbaya ni
tatizo sugu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika.
Jadili, kwa
kurejelea matukio ishirini katika tamthilia ya Kigogo. (alama 20)
PAULINE KEA: KIGOGO
Jibu swali la 4 au la 5.
4. “Ukitaka kukula asali kaa na nyuki!”
a) Eleza muktadha wa
dondoo hili. [alama 4]
b) Bainisha mbinu
iliyotumika katika dondoo hili. [alama 2]
c) Eleza jinsi wahusika
hawa walivyofaidika kutokana na kukaa na nyuki. [alama 14]
i) Chopi
ii) Kenga
iii) Ngurumo
iv) Mamapima
5. Eleza jinsi mwandishi
alivyotumia mbinu ya majazi. [alama 20]
SEHEMU YA D: HADITHI
FUPI:Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
6. Eleza sifa za wahusika wafuatao. [alama 20]
i) Mwalimu Musi
ii) Jairo
iii) Sera
iv) Mke wa Jairo
7. “ Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi
wafanikiwe.”
a) Eleza muktadha wa
dondoo hili [alama 4]
b) Fafanua sifa za
mhusika katika dondoo hili. [alama 8]
c) Fafanua mbinu zozote
nne za kifani katika hadithi hii. [alama
8]
KIGOGO na Timothy A .
Rege
1. “………..Acha
porojo zako . Kigogoo hachezewii watafuta maangamimi!”
a)Eleza muktadha wa
dondoo hili ( alama 4)
b)Fafanua sifa za
muzungumzaji ( alama 4)
c)El;eza jinsi msemewa
alivyokuwa akimchezea kigogo katika muktadha huu.(2)
Kwa kurejelea hoja kumi kutoka
kwenye tamthilia Onyesha ukweli kuwa
‘Kogogo hachezewi
2. Kwa
kirejelea tamthilia ya kigogo , jadili mbinu -
ishi tunazojifunza kutokana na kijana Tunu . ( alama 20)
3. HADITHI FUPI
Tumbo lisilishiba na
hadithi nyingine.
Shogake Dada ana Ndevu.
“Hapana cha ala, bwana.
Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri
ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi
……”
a) Eleza
muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)
b) Bainisha
tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili ( alama 2
c) Fafanua
sifa moja u a msemaji inayodokezwa na dondoo hili ( alama 2)
d) Msemaji wa
mabo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtundini. Eleza
ukitoa mfano kutoka hadithi. ( alama
4)
e) Eleza
maudhui ya malezi kama yanavyojotokeza katika hadithi ya shogaka Dada ab Ndevu
. (
alma 8
4. Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo
lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya kifaurongo
b) Shagake dada ana ndevu .
c) Mamake Bakari .
d) Mwalimu mstaafu .
e) Mtihani wa maisha .
TAMTHLIA - KIGOGO – PAULINE KEA
Jibu swali la 2 au la 3
2. “ Mimi ni mtu wa vitendo, si wa vishindo.”
(a) Weka dondoo hili
katika muktadha
wake. (al.
4)
(b) Kwa kurejelea dondoo
eleza sifa mbili za
mnenaji (al.
4)
(c) Thibitisha ukweli wa
kauli ya
mnenaji. (al.
12)
3. Ukiukaji
haki na uvunjaji sheria ni mambo yaliyokithiri katika jimbo la Sagamoyo.
Thibitisha. (al. 20)
SEHEMU
IV: HADITHI FUPI;
Tumbo Lisiloshiba na hadithi Nyingine.
6. Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na
ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya
utabaka. (al.
20)
Pauline Kea: Kigogo
4. Uongozi mbaya ni tatizo sugu linalokumba mataifa mengi ya
Afrika. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo.
(Alama 20)
5. ``Haja zako ni haja zangu, shida zako ni shida zangu, kiu yangu
ni kiu yako.``
a) Weka dondoo hili katika
muktadha wake. (Alama 4)
b) Kwa kurejelea dondoo taja na ueleze sifa nne
za msemaji na msemewa.(AL8)
c)
Taja tamathali ya usemi inayojitokeza katika dondoo (Alama 2)
d)
Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo eleza jinsi mbinu zifuatazo zimejitokeza (
6)
i)
Nyimbo
ii)
Jazanda
iii)
Majazi
SEHEMU D: HADITHI FUPI
6. a) Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni
mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua (ALama 10)
b) Fafanua sifa kumi za mzee Mago (Alama 10)
7. Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa. (Alama
20)
TAMTHILIA (Kigogo)
2. Eleza jinsi mbinu zifuatazo zilivyotumika katika Tamthlia hii. (alama
20)
a) Kinaya
b) Majazi
3. Ami
? Tangu lini ukawa ami yangu?
a) Eleza muktadha wa dondoo (Alama 4)
b) Taja mbinu iliyotumika katika dondoo
hili (AIama 2)
c) Eleza sifa za msemaji (AI 8)
d) Bainisha maudhui ya nafasi ya mwanamke ukizingatia mhusika
huyu (AIama 8)
SEHEMU YA TANO: HADITHI
FUPI
8..Kwa kurejelea hadithi
zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya
utabaka. (Alama 20)
8. Huacha
shughuli zote za pale zifanywe na ndugu yake.... Yeye mno hupiga mbio huku na
kule, kujaribu hili na lile
a. Fafanua muktadha wa dondoo hili (al.4)
b. Eleza shughuli zilizomfanya mrejelewa kumwachia nduguye
shughuli za pale. (al.2)
c. Huku ukitoa mifano mwafaka kutoka hadithini eleza sifa
bainifu za mrejelewa. (al. 14)
SEHEMU C: TAMTHILIA KIGOGO
4. Kwa kurejelea mifano mbalimbali
thibitisha dai kuwamwandishi huyu amemlika uhalisia
wa jamiiya Kenya (al. 20)
5. Ona
sasa! Mnaniharibia biashara. Nimewapa dakika moja muione nyumba hii
paa. Nikiwapatahapa, mtajua kwa nini wananiita
a. Fafanua muktadha wa
dondoo hili. (al. 4)
b. Tambua kwa kutolea mfano
mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika muktadha huu (al.2)
c. Kwa kurejelea mifano mbalimbali eleza
madhara/matokeo ya shughuli za msemaji katika dondoo hili
kwa jamii husika.
HADITHI FUPI- TUMBO
LISILOSHIBA
1. “Kwetu
tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha
wa dondoo hili (alama 4)
b) Taja tamathali
mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili (alama2)
c) Fafanua sifa za
msemaji (alama 4)
d) Jadili maudhui
ya utabaka ukjirejelea hadithi husika. (alama 10)
2. a) Mhini
na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya
mkubwa (alama10)
b) thibitisha
kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa (alama10)
SEHEMU YA D. KIGOGO
3. a) Utawala
wa sagamoyo unatumia mbinu nyingi kubakia mamlakani. Fafanua zozote kumi (ala
10)
b) Mwanamke
ni nguzo imara katika ujenzi wa jamii. Eleza kauli hii ukirejelea tamthilia ya
kigogo (ala 10)
4. “
Tuacheni kufumbatia maji kama jiwe. Sagamoyo inahitaji mabadiliko ,damu nyepesi
ili kuufungua ukurasa mpya”
a) Eleza muktadha
wa dondoo hili (ala 4)
b) Kwa kutoa mifano
taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo
hili (ala4)
c) Kwa nini
sagamoyo inahitaji mabadiliko? (ala 10)
d) Taja
sifa moja ya msemaji inayojitokeza katika dondoo hili (ala2)
“Unayazika
matumizi yetu .Unaifukia kesho yetu.”
a. Eleza
muktadha wa dondoo hili.
b. Onyesha
jinsi anayeambiwa maneno haya anavyoifukia kesho ya wenzake
3. ”Msiba wa kujidunga hauna
kilio.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea ya Kigogo (alama 20)
4. HADITHI FUPI
“Naapa
na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”
a. Eleza
muktadha wa dondoo hili
b. Tathmini
umuhimu wa mzungumzaji
c. “Biashara
inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi
hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
5. Jadili
maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame
Bakari.’
Kigogo; Pauline Keya
Ndege ruka, ndege ruka, na barua mkononi,
Kifika kamwambie kimbuga usiku mchana,
Kila uchao twasema heri yaliyopita jana
Hata nami sasa naja mbuga nami nachama
Hapa hapataniweka najua tutaonana
4. (a) Weka
dondoo hili katika muktadha wake ( alama 4)
(b) Eleza
aina ya urudiaji inayojitokeza katika dondooo ( alama 2)
(c) Eleza
sifa na umuhimu wa mhusika anayesema maneno haya ( alama 4)
(d) Fafanua
maudhui yanayojitokeza katika dondoo ( alama 2)
(e) Taja
na ueleze matumizi mengine manne ya mbinu hii katika tamthilia ukifafanua
ujumbe unaowasilishwa ( alama 8)
5. Amenifukuza,
anataka mkufu wangu wa dhahabu, nimeuficha.
(a) Fafanua
muktadha wa dondoo hili ( alama 4)
(b) Eleza mbinu ya
sanaa inayojitokeza katika dondoo ( alama 1)
(c) Eleza
maudhui yanayojitokeza katika
muktadha (alama
2)
(d) Jadili sifa
zozote sita za mnenaji wa maneno
haya (alama
6)
(e) Toa
matumizi mengine ya mbinu hii na ueleze ujumbe uliomo (alama 4)
SEHEMU D: HADITHI FUPI
Tumbo lisiloshiba na
hadithi zingine
6. ………
“ Mimi naweza kumtoa mtu chango sasa hivi! Usituangalie bwana. Kwani tunakula
kwa babako?”
(a) Kwa
nini msemaji anaongea hivi? (alama 2)
(b) Anayeambiwa
ni nani? Alikuwa anaenda
wapi? (alama
2)
(c) Anayezungumza
ni kielelezo cha watu walioathirika katika jamii kwa kurejelea
hadithi nzima. Onyesha vile mwandishi
amesawiri
athari hiyo (alama 10)
(d) Eleza
sifa za anayeambiwa (alama 4)
(e) Taja
na ueleze mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika
dondoo. (alama 2)
7. Said.A.Mohammed (Tumbo
lisiloshiba) na Salma Omar Hamad ( Shibe inatumaliza) walidhamiria kuonyesha
uozo katika jamii za kiafrika. Thibitisha (alama 20)
KIGOGO
4. "Mataifa mengi ya
Afrika yamekumbwa na tatizo la uongozi mbaya." Thibitisha
ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (al 20)
HADITHI FUPI (ALAMA 20)
Jadili ufaafu wa anwani
TUMBO LISILOSHIBA kwenye hadithi hii. (Alama 20)
1. Utawala
wa majoka katika jimbo la sagamoyo umejaa sumu ya nyoka’’. Jadili usemi
huu kwa hoja kuntu. (Alama 20)
2 ‟Wamenimaliza… Wamenigeuka…″.
a) Weka dondoo hili katika muktadha
wake. (Alama 4)
b) Eleza namna msemaji amemalizwa na
kugeukwa? (Alama 4)
c) Eleza umuhimu wa msemaji. (Alama
4)
d) Eleza jinsi wahusika wengine walivyomaliziwa
katika tamthilia. ( Alama 8)
SEHEMU YA D: HADITHI
FUPI
Tumbo lisiloshiba
3. (a)
Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika
tumbo lisiloshiba (alama 10)
(b)Dhihirisha
ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi
ya kifaurongo (alama 10)
7. Aliyeumwa
na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka (alama 4)
a) Weka dondoo hili
katika muktadha
b) Eleza namna
mzungumziwa alivyoumwa na nyoka (alama 6)
c) Mzungumziwa
anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu? (alama 10)
KIGOGO
1. Hivi
vishahada vyao wanavyovipata siku hizi vinawavimbisha kichwa! Mtu anaitwa
daktari na hata kazi ya maana hana....
a. Weka
dondoo hili hili katika muktadha wake (Alama 4)
b. Fafanua
mbinu mbili za sanaa alizozitumia mwandishi (Alama 4)
c. Ukirejelea
tamthilia ya Kigogo, dhihirisha kuwa mtu anaitwa daktari na hata kazi ya maana
hana.
HADITHI FUPI: TUMBO
LISILOSHIBA
Jibu
swali la 4 au 5
2. “Hakuchukua
muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile
kilichokuwa kikitokea ...”
a. Eleza muktadha wa dondoo
hili (Alama 4)
b. Fafanua
tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili (Alama 2)
c. Fafanua
kile kilichokuwa kikitokea (Alama 2)
d. Eleza
juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke (Alama 12)
3.
a. Ulezi
umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana
ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii (Alama 10)
b. Fafanua
changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya
kisasa (Alama 10)
BONYEZA KISWAHILI ILI KUPATA MAKALA MENGINE YA KISWAHILI
CLICK HISTORY TO READ MORE MATERIALS ON HISTORY
POST YOUR COMMENT DOWN THERE 👇
No comments:
Post a Comment