MENU

SEARCH HERE/ TAFUTA HAPA

Tuesday, June 9, 2020

UFAAFU WA ANWANI MTIHANI WA MAISHA


Samweli Matandiko  baada ya kuanguka mtihani anaamua kujitoa uhai kwa kujitupa kidimbwini ili afe.

Mamake Samweli anamwambia kuwa japo ameshindwa na mtihani wa shule, hawezi kushindwa na mtihani wa maisha.

Samweli anaporudi shuleni kuchukua matokeo yake, mawazoni anamwona mwalimu mkuu kama hambe au zuzu.

Jamii inaamini kuwa mtu akianguka mtihani wa shuleni basi hawezi kufaulu katika mtihani wa maisha.

Elimu ya shuleni inakadiriwa kama msingi wa maisha bora baada ya shuleni ndiposa Samweli, dada zake na wanafunzi wengine shuleni wanahudhuria masomo.

Ni wajibu wa wazazi kugharamia elimu ya watoto wao hadi wamalize elimu yao. Babake Samweli anafadhili masomo ya binti zake na mwanawe Samweli.

Samweli anamaliza mtihani wa shule na anapopokea matokeo mabaya, anatamauka na kujitumbukiza majini ili afe.

Mtihani wa shule ulimshinda kwa vile anafeli. Anasema kuwa mto Limpopo unapatikana Misri na Mto Zambezi upo Tanzania.

Samweli anatembea kilomita sita asubuhi na jioni kwa miaka mine akihudhuria shule ya Busukalala kisha mwishowe anafeli mtihani.

Babake Samweli anatarajia mwanawe kupita mtihani na kupata alama bora. Anauza ng’ombe ili kufadhili elimu yake.

Dada zake Samweli ambao ni Bilha na Mwajuma wanasoma katika shule ya Busukalala kabla ya Samweli na wanapita mitihani yao na kujiunga na elimu ya juu.

Babake Samweli anakasirishwa na kufeli kwa Samweli. Anapompata Samweli kando ya bwawa baada ya kuokolewa na mpita njia, anampa Samweli Kamba ili ajitie kitanzi.

Samweli anajipendekeza kwa mpenzi wake Nina kuwa bingwa masomoni. Baadaye anamwona Nina miongoni mwa umati wa wanakijiji wanaomzuia asijitose majini tena.

MADA ZINGINE ZILIZOSHUGHULIKIWA HUMU

HADITHI FUPI- TUMBO LISILOSHIBA
RIWAYA CHOZI LA HERI
TAMTHILIA YA KIGOGO
Post your comment in the comment section below 👇

3 comments:

  1. You are doing good to educate has keep the spirit moving. Thanks.

    ReplyDelete
  2. Naomba jazanda ya mtihani wa maisha tafadhali

    ReplyDelete
  3. I want notes for bembea ya maisha

    ReplyDelete