BLOG VISITORS

Tuesday, May 19, 2020

SAUTI GHUNA NA SIGHUNA

KONSONANTI GHUNA NA SIGHUNA

KONSONANTI GHUNA NA SIGHUNA

Ughuna wa sauti, hasa konsonanti huchunguzwa kwa kuzingatia kigezo cha mtetemeko wa nyuzi sauti.

Mtetemeko wa nyuzi sauti

Kwa kuangalia kigezo cha mtetemeko wa nyuzi sauti, tunapata aina mbili za konsonanti.
      I.          Sauti/ Konsonanti ghuna/nzito
   II.          Sauti/ Konsonanti sighuna/ konsonanti hafifu.

Konsonanti ghuna ni sauti ambazo zinapotamkwa huwa kuna mtatameko/ mtikisiko wa nyuzi sauti.
Mfano wa sauti ghuna ni : /z/, /b/, /g/, /d/, /gh/, /ny/, /ng/, /j/, /v/, /w/, /dh/, /y/, /n/, /m/.

Konsonanti sighuna ni sauti ambazo zinapotamkwa huwa hakuna mtetemeko au mtikisiko wa nyuzi sauti.
 Mfano wa sauti sighuna ni: /s/, /k/, /t/, /p/, /ch/, /f/, /l/, /h/, /th/.


TANBIHI:
Ni muhimu kutambua kwamba sighuna na ghuna hujitokeza katika majozi ya sauti za vitate.
Kwa mfano;
         
          Sighuna       ghuna
          /p/                /b/
          /t/                 /d/
          /th/               /dh/
          /ch/              /j/
          /f/                 /v/
          /k/                /g/
          /kh/              /gh/
          /s/                 /z/
-                       /n/, /ny/, /ng/, /m/
/h/                -
                   /r/, /l/

##MIFANO ZAIDI##

TANBIHI
รผ Nazali ghuna ya midomoni-/m/.
รผ Nazali ghuna ya ufizi-/n/
รผ Nazali ghuna ya kaakaa laini-/ng’/
รผ Nazali ghuna ya kaakaa gumu-/ny/
รผ Kizuio kwamiza ghuna-/j/
รผ Kizuio kwamiza sighuna-/ch/
รผ Kipasuo ghuna ya kaakaa laini-/g/
รผ Kipasuo sighuna ya kaakaa laini-/k/
รผ Kikwamizo ghuna ya midomo na meno-/v/
รผ Kikwamizo ghuna  cha ufizi- /z/
รผ Kikwamizo sighuna cha midomo na meno-/f/.
รผ Kikwamizo sighuna cha ufizi- /s/
รผ Kitambaza ghuna cha ufizi-/l/
รผ Kikwamizo sighuna cha koromeo-/h/

BONYEZA HAPA KWA FASIHI SIMULIZI

JIKUMBUSHE

VIGEZO VYA KUAINISHA IRABU NI:

  1. Mwinuko wa ulimi (chini, kati, juu)
  2. Mahali pa kutamkia (Mbele, kati au nyuma ya ulimi)
  3. Mkao wa midomo (Mtandazo au mviringo)
VIGEZO VYA KUAINISHA KONSONANTI NI:
  1. Mahali pa kutamkia
  2. Jinsi/ namna ya kutamka
  3. Mtetemeko wa nyuzi sauti
  4. Mkao wa glota/ mkondo hewa

TO SUPPORT US, DONATE TO US ON MPESA 07-02-37-18-29


POST A COMMENT DOWN THERE ๐Ÿ‘‡

43 comments:

  1. Good information Keep up the good work.

    ReplyDelete
  2. Good ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  3. Good ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  4. Nice ๐Ÿ‘ love it

    ReplyDelete
  5. Thanks for the clarification

    ReplyDelete
  6. Good and great work

    ReplyDelete
  7. Well understandable &clear notes, ๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  8. Imenisaidia pakubwa shukran

    ReplyDelete
  9. Thanks for assistance in learning

    ReplyDelete
  10. Hongera kazi kuntu๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  11. Kazi safi ya kuridhisha Asanteni

    ReplyDelete

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...