“O” NA “AMBA” REJESHI: MASWALI NA MAJIBU
MAKUENI
Iandike sentensi ifuatayo kwa kutumia ‘O’ rejeshi. (alama 2 )
Kijana ambaye hutumbuiza watu ametuzwa.
JIBU: Kijana atambuizaye watu ametuzwa.
HOMABAY
Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi cha kati. (alama 2)
(i) Kalamu imeibwa
(ii) Kalamu ni yangu
JIBU: Kalamu iliyoibwa ni yangu
RABAI
Andika sentensi hii upya ukitumia ‘o’ rejeshi tamati.
Zimwi ambalo humla mtu ni lile ambalo linaogopewa. (alama 2)
JIBU: Zimwi lilalo mtu ni lile liogopewalo
KIHARU
Tumia kirejeshi “O” tamati katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
Kijana ambaye anapendendeza ni yule ambaye hutia bidii.
JIBU: Kijana apendezaye ni yule atiaye bidii.
NANDI YA KATI
Tunga sentensi ukitumia kirejeshi tamati. (alama 1)
JIBU: Asomaye kwa bidii hufaulu. (alama 1)
(sentensi ionyeshe kuwa kirejeshi tamati huonyesha mazoea)
NANDI KASKAZINI
Tumia ‘amba’ rejeshi katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
Mchezaji ninayempenda ni Messi.
JIBU: Mchezaji ambaye ninampenda ni Messi.
NANDI KUSINI –TINDIRET
Kanusha bila kutumia ‘amba’ (alama 2)
Nitamtuza mwanafunzi ambaye ni nadhifu.
JIBU:Sitamtuza mwanafunzi asiye nadhifu.
ELDORET MAGHARIBI
Andika upya bila ya kutumia ‘amba’: (alama 1)
Mtoto ambaye alianguka shimoni ametibiwa.
JIBU: Mtoto aliyeanguka shimoni ametibiwa.
KERICHO
Tumia kirejeshi ‘O’ tamati katika sentesi ifuatayo : (al.2)
Kalamu ambayo alinunua ni ile ambayo anaipenda.
JIBU: Kalamu ainunuayo ni ile aipendayo
NANDI KATI
Tumia ‘amba’ katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
Wanafunzi wapitao mtihani husherehekea.
JIBU: Wanafunzi ambao hupita mtihani husherehekea.
KEIYO
Ondoa “amba” bila kubadilisha maana. (alama 2)
Jogoo ambaye huwika sana ndiye anayechinjwa.
JIBU: Jogoo awikaye / anayewika sana ndiye achinjwaye / anayechinjwa.
BUSIA
Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia ‘O’ rejeshi na kiambishi ngeli. (ala.2)
Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo.
JIBU: Mwanafunzi aliyetumwa nyumbani juzi hajapata karo hadi leo.
Andika sentensi ifuatayo bila kutumia “amba”:-
(i) Jitu ambalo linatusumbua sharti liadhibiwe vikali (alama 1)
JIBU: (i) Jitu linalotusumbua sharti liadhiwe vikali
(ii) Weka sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea:-
Mmea ambao unapandwa katika msimu wa masika unamea (alama 1)
JIBU: (ii) Mmea upendwao/ambao hupandwa katika msimu wa masika humea
MUUNGANO
Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O”
Mtoto anayelia huchapwa (alama 2)
JIBU: Mtoto aliaye huchapwa
KISII KUSINI
Iandike sentensi ifuatayo upya ukitumia ‘0” rejeshi tamati (ala 2)
Chumvi iliyochafuka si ile unayoizungumzia.
JIBU: Chumvi ichafukayo si ile uizungumziayo
KISUMU KASKAZINI NA MASHARIKI
Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia virejeshi vya tamati: (alama 2)
Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayewatii wazazi wake.
JIBU: Mwanafunzi afanikiwaye maishani ni Yule asomaye kwa bidii na pia awatiiye wazazi wake. (bila ‘O’ ya tamati asipate)
MBITA- SUBA
Kanusha ukitumia ‘O’ rejeshi. (al. 2)
Migomba ambayo hupaliliwa vizuri hunawiri sana.
JIBU: Migomba isiyopaliiwa vizuri hainawiri sana.
MERU KATI
Andika sentensi upya hila kutumia ‘0’ rejeshi. (alama 2)
Simba aendaye pole ndiye anywaye maji mengi.
JIBU: Simba ambaye huenda pole ndiye ambaye hunywa maji maenge
MBOONI MAGHARIBI
Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia ‘Amba’ – rejeshi. (alama2)
(i) Alizaa ndama mkubwa.
(ii) Ng’ombe alivunjika mguu.
JIBU: Ng’ombe ambaye alizaa ndama mkubwa alivunjika mguu.
Au
Ng’ombe ambaye alivunjika mguu alizaa ndama mkubwa.
KURIA MASHARIKI
Andika sentensi ifuatayo upya ukizingatia maagizo uliyopewa. (alama 2)
Tumia kirejeshi ‘o’ tamati.
Tunda ambalo huliwa ni lile lililoiva.
JIBU: Tunda liliwalo ni lile liivalo.
KITUI KATI
Tumia ‘O’ rejeshi katika sentensi uliyopewa. (Alama 2)
Uzuri ambao unasimuliwa unasifika.
JIBU: Uzuri unaosimuliwa unasifika
KILUNGU
Tumia kirejeshi ‘O’ katika sentensi hii. (alama1)
Mvua imenyesha na kuleta maafa mengi.
JIBU: Mvua inyeshayo huleta maafa mengi. (alama 1)
JIBU: Mvua iliyonyesha ilileta maafa mengi.
KITUI MAGHARIBI
Unganisha sentensi hii kwa kutumia kirejeshi ‘O’
Kucha zake ni ndefu. Kucha zimekatwa. (Alama 2)
JIBU: Kucha zake zilizokuwa ndefu zimekatwa (al. 2)
MASINGA
Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. (Alama 2)
Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.
JIBU: Yule ndiye mkwasi ambaye alinusurika
JIBU: Yule ndiye mkwasi aliyenusurika
NDHIWA
Tumia ‘o’- rejeshi badala ya ‘amba’ (Alama 2)
Mtu ambaye hufungwa ni yule ambaye huhalifu sheria.
JIBU: Mtu afungwaye ni yule alalifuye sheria.
TO SUPPORT US, DONATE TO US ON MPESA 07-02-37-18-29
BONYEZA HAPA KWA SAUTI GHUNA NA SIGHUNA
BOFYA HAPA KWA HISTORIA
BOFYA HAPA KWA FASIHI SIMULIZI
TOA MAONI AU ULIZA SWALI HAPO KWENYE SEHEMU YA COMMENT 👇
Walimu wanaokuwa na bidii ni Bora. Tumia -o- rejeshi tamati.
ReplyDeleteWalimu wenye bidii ni bora
DeleteMaximum bidii ni bora
DeleteWalimu wakuawo na bidii ni bora
ReplyDeleteWanafunzi ambao wanasoma kwa bidii watatuzwa
ReplyDeleteGeuza katika hali ya mazoea
Walimu wakuao na bidii hutuzwa.
ReplyDeleteshe did just HDB bent
ReplyDeleteSahihisha au rekebisha sentesi ifuatayo kwa njia mbili tofauti kwa kutumia kirejeshi- kinachofaa" yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika"
ReplyDelete