UTAFITI NYANJANI:
UKUSANYAJI WA DATA YA FASIHI SIMULIZI
Hiki ni kitendo cha kwenda katika jamii fulani na kukusanya data inayohitajika na kuichambua.
UMUHIMU WA UTAFITI NYANJANI KATIKA FASIHI SIMULIZI
ü Huwezesha kuendelezwa kwa utamaduni wa jamii mbalimbali
ü Hukuza na kuendeleza somo la fasihi simulizi.
ü Huzia kupotea kwa fasihi simulizi.
ü Hushughulikia mambo mapya ambayo hayakushughulikiwa hapo
mwanzoni.
ü Hukuza na kusambaza maarifa na ujumbe wa fasihi simulizi kwa
jamii pana.
ü Humpa mwanafunzi mbinu za utafiti anazoweza kutumia katika
masomo mengine.
ü Huibua na kukuza vipawa vya watafiti kama vile utambaji,
uigizaji, usogora na kadhalika.
HATUA ZA KUFANYA UTAFITI
1)
Maandalizi: Huhusisha mambo yafuatayo:
i. Uteuzi wa mada ya utafiti
ii. Kubainisha na kueleza
malengo ya utafiti huo.
iii. Kutambia eneo la kufanyia
utafiti
iv. Kutambua utafiti ambao
tayari ulifanywa kuhusu mada yako.
v. Kukadiria gharama katika
shughuli nzima.
2) Ukusanyaji
wa Data yenyewe
Ukusanyaji unawezakufanywa
kupitia jia hizi:
ü Kushuhudia
ü Kujaza fomu
ü Kushiriki
ü Kuhoji nk
3) Kurekodi
Data yako
Unahitaji kurekodi data
zako kupitia njia zifuatazo:
ü Kuandika
ü Kupiga picha
ü Kuchukua video
ü Kunasa habari nk
4) Kuchunguza
Data
Data ambayo umekusanya
inahitaji kuchunguzwa, kufsiriwa na kuandikwa upya, neno baada ya neno ili
maana halisi inayokusudiwa isipotezwe.
5) Kuchambua
na kufasili Data
Data uliyokusanya inahitaji
kuchambuliwa, kulinganishwa, kufasiliwa, kutathminiwa na kisha kujumuishwa ili
kupata matokeo kamili ya utafiti wako.
TO SUPPORT US, DONATE TO US ON MPESA 07-02-37-18-29
MBINU ZA KUKUSANYA DATA
1.
KUSHUHUDIA/KUTAZAMA/UCHUNGUZAJI
Katika mbinu hii, mtafiti
husimama kando na kurekodi utendaji/ matendo yanayoendelea katika jamii
anayotafiti.
2.
KUSHIRIKI
Mtafiti hujihushisha na
kuchangia katika utendaji wa shughuli inayofanywa na wanajamii inayotafitiwa.
Mbinu ya kushiriki ni
muhimu kwa sababu:
Ø Hukuza ushirikiano na mlahaka mzuri baina ya mtafiti na watafitiwa.
Ø Huleta jamii inayotafitiwa karibu na kumfanya mtafiti kuwa
huru kuwauliza maswali.
Ø Humwezesha mtafiti kusisimka/kufurahia shughuli hiyo ya
utendaji.
3. MAHOJIANO/USAILI
Huhushisha mtafiti kumhoji/kumuuliza
swali mtafitiwa, ili kupata majibu (data) ya maswala anayoyatafitia.
4. HOJAJI/FOMU YA MASWALI
Mtafiti huandaa hojaji
kabla ya kwenda nyanjani na kuwapa watu kujaza. Pia, mchunguzi anaweza kumhoji
mtu na kujaza hojaji mwenyewe.
5. UTAFITI MAKTABANI
Huhusisha kuchunguza na
kupitia mambo ambayo tayari yameandiwa vitabuni, mtandaoni na kwenye majarida
kuhusu mada unayotafitia.
MBINU
ZA KUREKODI NA KUHIFADHI DATA
Mbinu hizi zimegawika katika makundi
mawili kv:
i.
Mbinu za zamani
ii.
Mbinu za kisasa
Mbinu za kizamani
a) Kuhifadhi mongoni/akili
SWALI: Eleza udhaifu/
changamoto za kuhifadhi data akilini.
ü Mtafiti/ fanani huwezakufa
ü Mtafiti huwezakusahau maswala aliyoweka akilini
ü Mtafiti huwezakuathirika kiakili
ü Mtafiti huweza kubadili aliyohifadhi akilini
ü Mfatiti/fanani huwezakupoteza fahamu
Mbinu za kisasa
SWALI: Taja mbinu za kisasa za kuhifadhi data.
i.
Kutumia
kanda za kunasa sauti
ii.
Video
iii.
Maandishi
iv.
Filamu
v.
Kupiga
picha kutumia kamera
vi.
Tepu-rekoda
vii.
Sidi
SWALI: Eleza matatizo/ changamoto za kutumia mbinu za kisasa
kuhifadhi data.
ü Huhitaji ujuzi wa kutumia vifaa hivi.
ü Ni ghali/ huwa na gharama ya juu.
ü Huwezakupoteza data muhimu zikuharibika
ü Haziwezi kufanya kazi bila nguvu za umeme
MATATIZO AMBAYO HUWAKUMBA WATAFITI WAKIWA NYANJANI KUKUSANYA
DATA
SWALI: Eleza matatizo ambayo mtafiti huweza kukumbana nayo
akiwa nyanyani.
i.
Kutoelewa lugha ya jamii
anayotafiti
ii.
Vifaa vya kutafitia kuharibika
ama kupotea
iii.
Changamoto za usafiri
iv.
Jamii husika inaweza
kumshuku mtafiti kuwa anawapepeleza na hivyo kubadili tabia.
v.
Washiriki huwezakuhitaji
kulipwa pesa.
vi.
Kukosa ruhusa kutoka kwa
vyombo vya dola kama vile polisi ambao huwezakuchochea shughuli ya kukusanya
data.
vii.
Hali mbaya ya anga kama
vile mvua kunyesha zaidi na kuzuia utafiti kuendelea.
Kazi ya kumezea mate.kongole
ReplyDeleteKAZI NZURI SANAA
ReplyDeletePONGEZI KWA KAZI NZURI NA KWA UJUMBE MUHIMU KWETU WANAFUNZI TUNATARAJIA MENGI MAZUZI
ReplyDeleteKazi nzuri, iwapo kuna yeyote anayeweza kunijuza na Umuhimu wa maandalizi kabla ya utafiti.Nitashukuru sana
ReplyDeleteKwa uchambuzi zaidi, majibu ya maswali na makala mengine, subscribe channel yetu ye YoutTube hapa.
ReplyDeletehttps://www.youtube.com/channel/UC3EEBQNhW-y6VNg3JgpN76Q
Unayo makala katika PDF?
ReplyDeleteMakala ya pdf yako. 250/- pekee.
DeleteAsante. Kazi nzuri
DeleteAsanti sana
DeleteKuntu
DeleteKazi nzuri lakini hujatupa marejeo
DeleteSwadakta sana
Deletekuntu!
ReplyDeletenimeelimika sana na makala haya .asante
ReplyDeleteHongera kabisa,kazi nzuri hio ,na nawahiza mwendelee kutia bidiii zaidi . Asanteni🙏
ReplyDeleteHongera sana kazi yako yanata
ReplyDeleteAsante sana mwalimu ...imenisaidia katika kazi ya likizo
ReplyDeleteGood work you are really helpful
ReplyDeleteThanks
DeleteHongera kwa kazi nzuri
DeleteKazi murua zaidi,imenifutia na kufanya kulipenda hili somo,natumai ungekuwa mwalimu wangu enzi zile.
ReplyDeleteKazi shwari
ReplyDeleteKazi nzur
ReplyDelete𝔸𝕤𝕒𝕟𝕥 𝕤𝕒𝕟𝕒
ReplyDeleteKazi Safi!
ReplyDeletePongezi kwa kazi nzuri
ReplyDeleteKazi kuntu. Kongole!
ReplyDeleteKazi kuntu
ReplyDeleteAsante sana mwalimu......imenisaidia sana katika kazi ya likizo
ReplyDeleteAsante Sana
ReplyDeleteOngera
ReplyDeleteThanks for good work
ReplyDeleteVery good work
ReplyDeleteGood work may God bless
ReplyDeleteyou
Kazi ya kiwango Cha juu Sana,,vyema
ReplyDeleteKazi nzuri sana
ReplyDeletekazi nzuri
ReplyDeleteKongole, kazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDelete