MASWALI YA TAMTHILIA YA KIGOGO
1.
“Kigogo hachezewi; watafuta
maangamizi!”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (al. 4)
(b) Jadili ufaafu wa jina Kigogo kwa mrejelewa (al. 16)
2.
Msichana mrembo kama wewe,
ni kitu gani kinakufanya usiolewe?
Elimu unayo ya kutosha,
hata nga’ambo umeenda ukarudi.
Ukionyesha majivuno kwa
vijana, utazeeka ukiwa nyumbani kwenu.
Oooh bebi, miaka yaenda mbio sana,, nayo sura yako
ninachujuka.
a. Eleza muktadha wa dondoo hii. (al.4)
b. Eleza maswala muhimu yanayodokezwa na dondoo hii. (al.6)
c. Tathmini umuhimu wa mbinu ya ishara klatika kujenga tamthilia
ya Kigogo (al.10)
3.
Eleza jinsi mwandishi
alivyotumia mbinu ya kinaya katika tamthilia ya Kigogo (al.20)
4.
Eleza ujumbe unaopatikana
kwenye nyimbo zifuatazo; (al.20)
a. Wimbo wa uzaledo unaoimbwaredioni mjumbe anapotangaza kuhusu
maandalizi ya sherehe.
b. Wimbo wa Mamapima
c. Wimbo wa Daudi Kabaka anaoimbiwa Tunu.
5.
a. Nini umuhimu wa matumizi
ya lugha ya kishairi katika tamthilia ya Kigogo? (al.6)
b. Onyesha jinsi mwandishi
alivyotumia lugha ya kishairi katika tam,thilia ya Kigogo. (al.14)
6.
bainisha tamathali za usemi
zilizotumiwa katika kauli zifuatazo. (al.12)
i. “mwimbaji ninga kwelikweli”
ii. “…asidiriki katu kuionja kuonja shubiri na tamu ya
mapambano.”
iii. “…lakini huu wako wa kuishi milele suiwezi.”
iv. “…sitaki hawa makunguru wanidhuru.”
v. “…kitu cha aali cha tunu kama wewe.”
vi. “Sitaacha kula mkate kwa kuchelea kiungulia.”
7.
Bainisha mbinu za kimtindo
zilizotumiwa katika kauli zifuatazo. (al.8)
a. Viongozi wa usoni wa Sagamoyo. Hamjambo?
b. “ kila kitu ni Tunu. Tunu, Tunu, Tunu.
c. “…nayo haina maisha Sagamoyo.”
8.
‘Nusura roho ianguke
mwanangu. Wametutia woga mwingi sana. Tywaishi kwa hofu.’
a. Eleza muktadha wa dondoo hii (al.4)
b. Eleza uhusiano kati ya msemaji na msemewa wa kauli hii.
(al.2)
c. Bainisha imani zozote mbili
za kidini zinazojitokeza katika
kauli za baadaye za mnenaji wa maneno haya. (al.4)
d. Fafanua jinsi maidhui ya kuzorota kwa usalama yanavyodokezwa
na dondoo hili na yanavyojitokeza katika tamthilia nzima. (al.10)
9.
‘koma! Wajua ni hatia kuuza
pombe haramu?
a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b. Aliyeambiwa maneno haya alitoa jibu gani? (al.2)
c. Fafanua sifa zozote mbili za aliyeambiwa maneno haya (al.4)
d. Msemaji ni kielelezo cha maadili katika jamii ya Sagamoyo.
Fafanua. (al.10)
BOFYA HAPA KWA 'O' NA 'AMBA' REJESHI
MAUDHUI TAWALA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
BOFYA HAPA KWA 'O' NA 'AMBA' REJESHI
MAUDHUI TAWALA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
No comments:
Post a Comment