SOMA SHAIRI HILI KISHA UJIBU MASWALI YANAYOFUATA (ALAMA 20)
Ulimwengu ulimwengu, ulimwengu naratibu
Yaliyo kichwani mwangu, nataka kuyahutubu
Wayasome ndugu zangu, wa mbali na karibu
Cha wenye raha na taabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ulimwengu ni kiwanja, chenye raha na tabu
Wengine wanajikonja, kwa wengine ni adhabu
Kuta na kucha twahanja, kutafuta matulubu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa balaa,
aliniusia babu
Mna mambo yamejaa, ya faraja na kusibu
Na machache ya kufaa, ila mengi ya udubu
Cha wenye raha na tabu ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja cha Amina, Saidi Ali Rajabu
Wengune kitu hatuna, tunaishia kababu
Wale wamejaza sana, wanashindwa kuhesabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa urongo, na kweli pia ajabu
Kichwa hudanganya shingo, tumbo kiuno chasibu
Usitumai ubongo, wa nduguyo na swahibu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa walevi, pombe kwao ni dhahabu
Mara vile mara hivi, wakilewa majudhubu
Maneno ya kiujuvi, hujipaka hata shabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni kiwanja wenye dini, watiio Wahabu
Mashekhe misikitini, humo hufanya muhibu
Mapadri kanisani, huvihubiri vitabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa malofa, lofa mtu mwenye tabu
Kusema sana kashifa, na moyo kisebusebu
Tunakaribia kufa, kwa kushindwa kujimudu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
Ni uwanja wa faraja, alowajali habibu
Na mengine sitotaja, msinambe nina gubu
Ni uwanja wa viroja, vigumu kuvikutubu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
MASWALI
a. Lipe shairi hili anwani mwafaka. (al. 1)
b. Ainisha shairi hili katika bahari mbili na utoe dhibitisho.
(al. 2)
c. Bainisha uhuru wa mtunzi wa shairi hili (al. 2)
d. Eleza muundo wa shairi hili. (al. 5)
e. Andika ubeti wa tano kwa lugha tutumbi. (al. 4)
f. Fafanua mbinu zozote mbili za uandishi zilizotumika katika
shairi (al. 4)
g. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika takika
shairi.(al. 2)
i.
Balaa
ii.
Kisebusebu
##Kwa Tumbo lisiloshiba, GUZA HAPA ##
BONYEZA HAPA KWA CHOZI LA HERI
BOYFA HAPA KWA MAUDHUI TAWALA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
BONYEZA HAPA KWA NGELI
Uliza swali moja kwa moja kupitia <WHATSAPP>
BOYFA HAPA KWA MAUDHUI TAWALA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
BONYEZA HAPA KWA NGELI
Uliza swali moja kwa moja kupitia <WHATSAPP>
POST A COMMENT DOWN THERE π
majibu ya shairi hili?
ReplyDeletemajibu ya shairi hili?
ReplyDeleteMajibu
ReplyDeleteMajibu tafadhali
ReplyDeletemaswali mazuri ya maandalizi ya wanafunzi. Hongera. Naomba kujua kama kuna miongozo ya maswali haya.Pia naomba kujua kama kuna maswali ya vitabu vipya ya fasihi;Bembea ya Maisha na Mapambazuko ya Machweo. Shukrani.
ReplyDelete