BLOG VISITORS

Wednesday, June 9, 2021

VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021

Subscribe to our Youtube Channel for updates on CHECHE ZA MOTO analysis videos and other updates
Click here> YouTube

Wizara ya Elimu imeidhinisha vitabu vipya vya fasihi andishi vitakavyosomwa, kuchambuliwa na kutahiniwa katika shule za upili kote nchini.

CHECHE ZA MOTO iliyoandikwa na John Habwe na kuchapishwa na Jomo Kenyatta Foundation (JKF) ndiyo riwaya ambayo itachukua nafasi ya riwaya ya Chozi la Heri ya Asumpta K. Matei.

Hadithi fupi, MAPAMBAZUKO YA MACHWEO iliyochapishwa na kampuni ya ushapishaji ya Mountain Top ndiyo itachukua nafasi ya Tumbo Lisiloshiba na hadithi nyingine iliyohaririwa na Alifa Chokocho na Dumu Kayanda.

Wizara ya elimu imeidhinisha vitabu hivi baada ya miaka minne ya kutahiniwa kwa Chozi la Heri na Tumbo Lisiloshiba. 

Wakufunzi wameelezea matarajio makuu kwamba Cheche za Moto huenda ikawa nyepesi kwa wanafunzi kuelewa hasa kwa kuzingatia mtitiriko wa vitushi na idadi ya wahusika. Baadhi ya walimu wamedokeza kwamba riwaya inayoondoka imekuwa changamoto kwao na kwa wanafunzi kwa sababu imeshishirikisha wahusika chungu nzima. Vilevile, walimu hao wameeleza kwamba riwaya Chozi la Heri imekuwa na uchangamano mwingi katika muundo wake.

Kwa upande mwingine, wanafunzi waliohojiwa na Homeschool Kenya wamepongeza watunzi mbalimbali wa hadithi katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba. Wanafunzi hao wamedokeza kwamba hadithi hizo mbali na kuburudisha, zimesheheni ujumbe muhimu kwa wanafunzi wote. Nilipowauliza kuhusu changamoto walizokumbana nazo katika usomaji wao wa Tumbo Lisiloshiba, wanafunzi hao walisisitiza kwamba hadithi hizo zimekuwa nyepesi kuelewa.

Tunashughulikia uchambuzi wa Cheche za Moto na Mapambazuko ya Machweo na baada ya siku chache tutachapisha makala hayo humu kwenye blogu kwa manufaa yetu sote. Ahsanteni.

Wasiliana nasi Kupitia WhatsApp. 

Kwa makala mengine gusa yafuatayo:

Tuesday, June 8, 2021

๐Ÿ’ซ
Wasiliana nasi Kupitia WhatsApp. 

Kwa makala mengine gusa yafuatayo:

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...