UJUMBE WA DHARURA KWA WAKUFUNZI WOTE
Ni mwaka mpya ambapo
mchakato wa mafunzo umeanzishwa tena rasmi baada ya kusitishwa mwaka uliopita
kutokana na janga la tandavu la Korona. Katika wiki chache ambazo tumekuwa
tukitimiza malengo yetu kwa kuwahudumia wanafunzi kwa njia ya mafunzo,
tumeshuhudia ukatili miongoni mwa mwao katika baadhi ya shule humu nchini. Ukatili
huu umehatarishs maisha ya walimu katika shule husika. Ni muhimu kutambua
kwamba usalama wako ni muhimu sana, kwa hivyo huna budi kuusisitizia. Zifuatazo
ni njia ambazo kulingana nami, zitaweza kutusaidia kuepuka ukatili na udhalimu
wa wanafunzi.
Zingatia jukumu kuu
ambalo uliajiriwa kutekeleza. Iwapo umesahau, rejelea barua yako ya kazi kutoka
kwa tume ya kuajiri walimu. Kila mara hakikisha kwamba umetimiza jukumula kutimiza jukumu lako, na kwa kiwango kinashoridhisha matarajio yako,
ya mwajiri na ya jamii. Kukosa kutimiza jukumu huweza ukazua uhasama wa
wanafunzi dhidi yako, jambo ambalo huenda likatishia usalama wako. Wanafunzi wa
sasa japo wamepungukiwa na motisha ya kujituma masomoni kutokana na athari za
mienendo na maisha ya kijamii, wanatambua wakati ambapo wanapokea huduma bora kutoka kwa Mwalimu na wakati ambapo wanapokea bora huduma.
Je, sheria inakupa
nguvu za kumwadhibu mwanafunzi? La. Ni muhimu kila mkufunzi kufahamu fika
kwamba sote (walimu na wanafunzi) tuko katika karne ambayo mawasiliano hayana
vizingiti. Yanapenya na kupokelewa na kila rika. Kwa hivyo tusipuuze ukweli kwamba
wanafunzi hawa wanafahamu kwamba adhabu ni kinyume cha sharia. Wakati mwingine
unaweza ukagundua kuwa mwanafunzi anapuuza hitaji lako la kumwadhibu akijua
kwamba unakiuka sharia.Wewe kama mkufunzi huenda ukakerwa na jambo hili. Kabla hasira
hazijakutawala, hebu jiulize iwapo kumpa mwanafunzi adhabu nimoja kati ka majukumu uliyokabidhiwa na tume.
Kupitia masomo ya
saikolojia kwenye vyuo mbalimbali tulikosomea ualimu, kila mwalimu aliyekuwa
makini kwa masomo hayo bila shaka anapaswa kuwa na uwezo wa kutambua ama kung’amua
fikra za wanafunzi kutokana na jinsi wanavyozungumza ama kutenda mambo yao. Iwapo
umegundua kisicho kawaida katika tabia na mienendo ya mwanafunzi, kinachoweza
kuhatarisha maisha yako, kumbuka kuwa ni muhimu kutahadhari kabla ya hatari.
Kwa mfano, ukimwona mwanafunzi na kifaa kisichohitajika shuleni kama kisu,
chukua hatua kwa kufuata mchakato unaofaa ili apikonywe kifaa hicho.
Mwanafunzi anapojeruhiwa
ama kwa behati mbaya, anapokufa mikonomi mwa Mwalimu, magari makubwa makubwa huja
skulini kumchukulia hatua mkufunzi husika. Mwalimu anapopitia yayo hayo mikononi
mwa wanafunzi, ni muhali kuona wakuu wakija kuwachukulia wanafunzi hatua. Hili
ni thibitisho tosha kwamba wewe kama Mwalimu, kila mja anaamini kuwa unauwezo wa kujilinda na kujihakikishia usalama wako. Kwa hiyo tambua
kwamba usalama wako unakutegemea wewe mwenyewe.