BLOG VISITORS

Showing posts with label arudhi. Show all posts
Showing posts with label arudhi. Show all posts

Tuesday, July 22, 2025

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI (KIPOZI, KITONNDO, NA ALA)

 

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI

MAANA YA SHAMIRISHO:

Shamirisho ni neno ambalo huashiria nomino inayopokea kitendo (kitendwa/mtendwa), nonimo inayofaidika kutokana na kitendo (kitendewa/mtendewa), na kifaa kinachotumika katika kitendo (ala), katika sentensi.

AINA ZA SHAMIRISHO

1. Shamirisho Kipozi/ Yambwa Tendwa

2. Shamirisho Kitondo/ Yambwa Tendewa/yambiwa

3. Shamirisho Ala/ Kitumizi

------------------------------------------------------------------------------

1. SHAMIRISHO KIPOZI

Pia huitwa yambwa tendwa (Direct object).
Ni nomino anayopokea athari ya kitendo moja kwa moja.
Mara nyingi hipatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kutenda, japo huwezakupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli zingine.

Mifano

  1. Wizara ya elimu inarekebisha mtaala. (mtaala-shamirisho kipozi)
  2. Mkulima analima shamba.  (shamba-shamirisho kipozi)
  3. Mgonjwa aliletewa chai kwa chupa na Swaleh. 
  4. Kitabu cha mwanafunzi kimepotezwa na mtoto.
  5. Kipenga cha mkufunzi kitanunuliwa wiki ijayo na mwalimu mkuu.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
2. SHAMIRISHO KITONDO
Pia huitwa yambwa tendewa au yambiwa (Indirect Object).
Ni nomino ambayo huathiriwa na kitendo kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Huathiriwa na kitendo kinacho tendwa kwa shamirisho kipozi.
Hupatikana katika sentensi zilizoandikwa katika kauli ya kitendea/ kutendewa.

Mifano
  1. Mzazi alimnunulia mwanawe baiskeli kwa kupita mtihani.
  2. Kaka atamfyekea babu yangu shamba baada ya kutoa mahindi.
  3. Nina alimpikia mgonjwa chakula chenye ladha tamu.
  4. Walimu waliwekewa runinga kwanye afisi yao.
  5. Mwanasiasa alipigiwa kura na kushinda uchaguzi mdogo wa mkoa.
----------------------------------------------------------------------
3. SHAMIRISHO ALA/ KITUMIZI
Ni nomino ambayo hurejelea kifaa kinachotumiwa kitekeleza kitendo fulani.
Huwakilishwa na vielezi vya namna ala.
KUMBUKA: "kwa" si sehemu ya shamirisho ala.

Mifano
  1. Kaka alilima shamba lake kwa jembe jipya.
  2. Mpishi alikata vitunguu na nyanya kwa kisu.
  3. Mwalimu alisahihisha vitabu vya wanafunzi kwa kalamu.
  4. Juma alisafiri ughaibuni kwa ndege.
  5. Viwanja vilinunuliwa kwa pesa
  6. Mkongwe atajengewa nyumba ya mbao.
----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
SHUKRAN KWA USOMAJI WAKO πŸ™πŸ‘πŸ˜Ž

UNA SWALI KUHUSU SHAMIRISHO KIPOZI, KITONDO, AMA SHAMIRISHO ALA?
ULIZA HAPA CHINI πŸ‘‡πŸ‘‡


Tuesday, April 14, 2020

USHAIRI: SHAIRI HURU


MFANO WA SHAIRI HURU


SEHEMU YA A: USHAHIRI
                                    SHAIRI ‘A’
            (i)                    Umekata mti mtima
                                    Umeangukia nyumba yako
                                    Umeziba mto hasira
                                    Nyumba yako sasa mafurikoni
                                    Na utahama
                                    Watoto wakukimbilia

            (ii)                   Mbuzi kumkaribia chui
                                    Alijigeuza panya
                                    Akalia kulikuwa na paka
                                    Kichwani
                                    Mchawi kutaka sama kutisha
                                    Alijigeuza samba
                                    Akalia na risasi kichwani

            (iii)                  Jongoo wapi sasa yatakwenda
                                    Bwanako kumpa sumu?
                                    Hadija umeshika nyoka kwa mkia
                                    Hadija umepitia nyuma ya punda
Jogoo kataka sana kukimbia
Aliomba miguu elfu

(iv)                  Akaachwa na nyoka
Hadija wapi sasa
Bwanako kumpa sumu?
Hadija umashika nyoka kwa mkia
Hadija amepita nyuma ya punda

SHAIRI ‘B’
                                    Piteni jamani,piteni haraka
                                    Nendeni ,nendeni huko mwendako
                                    Mimi haraka, haraka sina
                                    Mzigo wangu,mzigo mzito mno
                                    Na chui sitaki kuweka

                                    Vijana kwa nini hampiti?
                                    Kwa nini mwanicheka kisogo?
                                    Mzigo niliobeba haupo.

                                    Lakini umenipinda mgongo na
                                    Nendako
                                    Haya piteni!piteni haraka!Heei!

                                    Mwafikiri mwaniacha nyuma!
                                    Njia ya maisha ni moja tu.
                                    Huko mwendako ndiko nilikotoka
                                    Na nilipofikia wengi wenu
                                    Hawatafika

                                    Kula nimekula na sasa mwasema
                                    Niko nyuma ya wakati
                                    Lakini kama mungepita mbele
                                    Na uso wangu kutazama
                                    Ningemwambia siri ya miaka
                                    Mingi

Maswali
(a)Haya ni mashairi ya aina gani?Toa sababu.     (Alama 2)

(b)Washairi hawa wawili wanalalamika.Yafafanue malalamishi yao.             (Alama 4)

(c)Onyesha jinsi kinaya kinavyotokeza katika tungo hizi mbili. (Alama4)                                                                                                                                         
(d)       Ni vipi Hadija :-
  (i) Amekata mti mtima?    (Alama 2)                                              
 (ii)       Amepita nyuma ya punda. (Alama 2)

(e) Toa mifano miwili ya uhuru mshairi kwa kurejelea mashairi haya.            (Alama 2)

(f)        kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:-
                                    (i)        Mzigo
                                    (ii)       Siri
                                    (iii)      Kula nimekula
           (iv)      Niko nyuma ya wakati.(Alama 4)
                                           
###KWA MASWALI YA FASIHI SIMULIZI, GUSA HAPA###

###KWA MASWALI YA KIGOGO, BONYEZA HAPA###

###KWA MASWALI YA TUMBO LISILOSHIBA, GUSA HAPA###

Uliza swali moja kwa moja kupitia <WHATSAPP>

POST A COMMENT DOWN THERE πŸ‘‡

SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI (KIPOZI, KITONNDO, NA ALA)

  SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI SHAMIRISHO KATIKA KISWAHILI MAANA YA SHAMIRISHO : Shamirisho ni neno ambalo huashiria nomino inayopokea kitend...