BLOG VISITORS

Showing posts with label insha. Show all posts
Showing posts with label insha. Show all posts

Sunday, January 28, 2024

BEMBEA YA MAISHA: MASWALI MAKUU YA KUDURUSU ILI KUIELEWA RIWAYA KWA KINA

Bembea ya Maisha, iliyoandikwa na mwandishi hodari, Timothy Arege, ni riwaya iliyosheheni maudhui mengi, mbinu nyingi za uandishi, wahusika wengi na mtiririko mzuri wa vitushi. Maswahi haya yatakusaidia kuyaelewa mambo haya kwa undani.


ILI KUPATA MASWALI MENGINE MENGI....BONYEZA HAPA

Saturday, December 26, 2020

KCSE ONLINE REVISION CLASS

KCSE ONLINE REVISION  CLASS FOR KISWAHILI

BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA NA KUANZA KUDURUSU

CLICK HERE TO JOIN THE ONLINE CLASS


Tutafanya udurusu wa kazi ya kidato cha nne ili kujitayarishia mtihani wa kitaifa. Tutashughulikia mada vitengo vifuatavyo:

1. Sarufi 2. Ushairi 3. Insha 4. Isimujamii 5. Fasihi Andishi: Kigogo, Chozi la Heri na Tumbo Lisiloshiba.

Wasiliana nasi kwa 0702371829

Whatsapp Click here


TUTASHUGHULIKIA YAFUATAYO


1. KARATASI YA KWANZA: INSHA
        A. Insha ya Kiuamilifu/Ya lazima
        B. Insha ya Mjadala
        C. Insha Methali
        D. Insha ya Mdokezo

2. KARATASI YA PILI
        A. Ufahamu
        B. Uarufifupisho
        C. Sarufi
        D. Iimujamii

3. KARATASI YA TATU
        A. Ushairi
        B. Fasihi Andishi: Kigogo, Chozi la Heri, Tumbo Lisiloshiba
        C. Fasihi Simulizi
      
Add a comment in the comment section/ Toa maoni au uliza swali katika sehemu ya maoni hapa chini👇

Tuesday, June 16, 2020

MIUNDO YA NOMINO KATIKA NGELI ZA KISWAHILI


MIUNDO YA NOMINO KATIKA NGELI ZA KISWAHILI
Maana ya ngeli
Ngeli ni makundi mbalimbali ambapo maneno ya Kiswahili yamegwaika. Ni migawo mbalimbali ya maneno ya Kiswahili.

Tanbihi: Katika othografia/ maandishi, ngeli huandikwa kwa herufi kubwa.
Makala haya yanashughulikia miundo mbalimbali ya maneno katika baadhi ya ngeli za Kiswahili.

Ni wazi kwamba maneno tofautitofauti katika ngeli mahususi huchukua maumbo mbalimbali tofauti. Makala haya yanashughulikia maumbo hayo tofauti ya maneno katika ngeli.



NGELI YA A-WA

1.     Muundo wa M-WA- maneno haya huanza kwa M katika umoja na WA katika wingi. Mfano,
mtoto
watoto
mjomba
Wajomba
mwana
Wana
mzee
Wazee
mtemi
watemi

2.     Muundo wa CH-VY. Maneno haya huanza na CH katika umoja VY katika wingi. Mfano,

chura
Vyura



3.     Muundo wa M-MI.

NGELI YA LI-YA

KWA NGELI ZINGINEZO, BONYEZA HAPA

NGELI ZILIZISHUGHULIKIWA:

A-WA
LI-YA
U-ZI
KI-VI
U-I
I-I









Uliza swali moja kwa moja kupitia <WHATSAPP>



Sunday, May 24, 2020

WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA

WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA


Katika fasihi, mhusika ni kiumbe aliyefasiriwa au kubuniwa na mtunzi, anayemwiga na kufanana na kiumbe halisi duniani kwa kiasi Fulani. Kuna aina mbalimbali za wahusika kama vile:

a)    Mhusika mkuu

Huyu ni mhusika ambaye anajitokeza katika hadithi kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko wahusika wengine. Huweza kujitokeza kuanzia mwanzo hadi mwisho wa hadithi.

b)    Wahusika wadogo/ wasaidizi

Hawa ni wahusika ambao hutangamana na mhusika mkuu na kumsaidia kuibua dhamira na maudhui katika hadithi. Wahusika hawa hujitokeza kwa kiasi kidogo tu kwenya hadithi na kisha kupotea.

Diwani ya Tumbo Lisiloshiba ina hadithi kumi na tatu (13) na wahusika ni wafuatao.

TUMBO LISILOSHIBA-Said A. Mohamed

1.     Mzee Mago-Mhusika mkuu
2.     Mwene
3.     Kabwe
4.     Bi. Suruta
5.     Bi. Fambo
6.     Jitu

MAPENZI YA KIFAURONGO-Kenna Wasike
1.     Dennis- Mhusika mkuu
2.     Daktari Mabonga
3.     Penina (mpenzi wa Dennis)
4.     Shakila
5.     Wanafunzi chuoni
6.     Bwana Kitime- babake Penina

SHOGAKE DADA ANA NDEVU-Alifa Chokocho
1.     Safia -mhusika mkuu
2.     Bwana Masudi- babake Safia
3.     Bi. Hamida-mamake Safia
4.     Mkadi (Mtoto wa Habiba Chechei)
5.     Lulua (mnuna wake Safia)
6.     Kimwana (Shogake Safia)

SHIBE INATUMALIZA- Salma Omar Hamad
1.     Sasa
2.     Mbura –wahusika wakuu ni Sasa na Mbura
3.     Mzee Mambo
4.     DJ

MAME BAKARI-Mohammed Khelef Ghassany
1.     Sara –mhusika mkuu
2.     Sarina- rafikiye Sara
3.     Beluwa- dadake Sarina
4.     Bi. Aluwiya- mamake Sara
5.     Babake Sara
6.     Mame Bakari- mtoto aliyezaliwa na Sara
7.     Janadume
8.     Mwalimu Mkuu

Sunday, April 19, 2020

INSHA---HOJA/MAUDHUI YA MADA MUHIMU ZA INSHA




HOJA/MAUDHUI YA MADA MUHIMU ZA INSHA

CHANGAMOTO ZINAZOKUMBA VIJANA
ü Magonjwa sugu (ukimwi)
ü Dawa za kulevya
ü Ukosefu wa ajira
ü Umaskini uliokithiri
ü Uigaji wa tamaduni za kigeni
ü Athari za utandawazi
ü uchumi kudoroa (Kustaafishwa mapema)
ü Kuibuka kwa lugha ya vijana isiyoeleweka na wavyele wao, basi kukosa maongozi bora.
ü Shinikizo la hirimu (marika)
ü Ujana (Ushababi)
Taja zozote 5 (changamoto na pendekezo la kusuluhisha)

DHULUMA DHIDI YA WANAUME
ü Kupigwa
ü Kufanyizwa kazi nzito za kinyumbani.
ü Kutusiwa/kukashifiwa.
ü Kunyimwa haki za ndoa.
ü Kukejeliwa (wakosapo ajira)
ü Kushurutishwa kutoa pesa zote.
ü Kunyimwa uhuru wa kutoa maoni.
ü Kunyimwa chakula (wafikapo nyumbani kuchelewa/walevi)

HATUA ZINAZOPASWA KUCHUKULIWA ILI KUIMARISHA MATOKEO YA MTIHANI SHULENI MWETU
Mwili uzingatie hoja zifuatazo.
ü Kuimarisha nidhamu
ü Kununua vifaa vya kimsingi k.v vitabu
ü Kuhimiza matumizi ya Kiswahili na kiingerza shuleni
ü Kuhimiza matumizi yafaayo ya wakati
ü Kuhimiza vipindi vyote vya masomo kuhudhuriwa.
ü Kununua makala ya kudurusu
ü Kuhimiza wazazi kuwajibikia majukumu yao
ü Kuhimiza uwajibikaji  wa walimu na wanafunzi
ü Kutoa nasaha na ushauri katika masomo mbalimbali na umuhimu wa elimu kwa jumla.
ü Kuimarisha mahabara na maktaba
Mtahiniwa azingatie pande zote mbili hasara na faida kasha achukue msimamo

UTANDAWAZI UNA HASARA KULIKO FAIDA JADILI:
Hasara za utandawazi
ü Maovu  kuzagaa haraka kote
ü Miigo ya mambo yasiyofaa
ü Maadili kuzorota
ü Uhalifu kuongezeka
ü Matumizi mabaya ya mtandao
ü Wanafunzi kuchanganyikiwa

Faida za utandawazi
ü Kukuza maendeleo
ü Kubadilishana mawazo
ü Kuimarisha biashara za kimataifa
ü Kuimarisha elimu
ü Kuhimiza mataifa na uchunguzi
ü Kuimarisha teknolgia ya habari na mawasiliano
ü Mtahiniwa azingatie hoja zilizo hapo juu.
Hoja nyiongine zikadiriwe ipasavyo

HOJA MUHIMU ZA TAWASIFU
ü Jina la mwandishi
ü Tarehe ya kuzaliwa
ü Mahali alipozaliwa
ü Wazazi wake
ü Motot wa ngapi katika uzawa wake
ü Jinsia yake
ü Alikosoma na wakait aliposima
ü Alichosemea na livyofaulu
ü Taaluma, kazi na tajriba
ü Uraibu wake
ü Uananchama wowote
ü Mafanikio yake maishani/tuzo na vyeit alivyowahi kushinda
ü Pingamizi zozote alizowahi kukumbana nazo maishani
ü Hali yake ya ndoa/familia
ü Warejelewa wake
ü Semina/makongamano ambayo amewahi kuhudhuria
ü Majukumu au mchango wake katika jamii
ü Matarajio yake/azma yake/manifesto yake katika wadhifa wake mpay wa Useneta
ü Anatetea nini zaidi katikak jamii
ü Falsafa/mtazamo wake katika jamii kuhusu maswali mbalimbali

PENDEKEZA NJIA KADHAA ZINAZOWEZA KUTUMIWA KATIKA KUBUNI NAFASI ZA KAZI HAPA NCHINI
ü Upanuzi wa viwanda
ü Kuimarisha uchmi wanachi ili pesa zipatikane za kuwaajiri watu
ü Kuhimiza watu kujiajiri na serikali
ü Kupunguza mishahara mikubwa mikubwa ili pes hizo zitumike kuajiri watu wengine
ü Uimarishaji wa sekta ya elimu ili watu wapewe ujuzi mbalimbali
ü Masomo shulnie yalenge kufnza ubunifu wa kiakzi
ü Serikali itoe ya kigeni yanayotaka kufanya biashara nchini yawekewe sheira kuwa ni lazima yaajiri idaid Fulani ya wenyeji ndipo yaruhusiwe kufanya biashara nchini
ü Kushiriki katika shughuli za jua kali
ü Wafanyikazi wa kgieni watozwe usuhur ziaidi kwa mishahara yao ili kuwazuia kuja kuchukua nafasi za kikazi mabazo zingekuwa za wenyeji
ü Sekta ya michezo iimarishwe

UHALIFU
Aina za uhalifu
ü Wizi wa kimabavu
ü Mapigano ya kikabila
ü Ugaidi
ü Ubakaji
ü Mauaji ya kikatili
ü Udanganyifu katika biashara (bidhaa gushi)
ü Ulanguzi wa dawa za kulevya
ü Ulanguzi wa binadamu

Njia za kukabiliana na uhalifu
ü Kuwasaka na kuwakamata wahalifu
ü Kuimarisha usalama nchini.
ü KuhimizaWananchi kuripoti visa vya uhalifu au watu wanaowashuku kuwa wahalifu.
ü Tume ya ukaguzi na ukadiriaji wa ubora kutekeleza wajibu wake.
ü Walinda usalama kupewa motisha.
ü Kufutwa kazi kwa maafisa wausalama wanaoshirikiana na uhalifu.

MANUFAA YA UHIFADHI WA MAZINGIRA
ü Kuwepo kwa miti – ivutayo mvua
ü Itupayo chakula, dawa n.k.
ü Hutupa mbao za ujenzi.
ü Tabaka la ozoni likihifadhiwa tutakingwa dhidi ya miale ya jua isababishayo kansa ya ngozi n.k.
ü Binadamu atakuwa na afya nzuri kutokana na hewa safi yenye oksijeni.
ü Uhifadhi wa msitu utazuia maporomoko ya ardhi yasababishayo vifo na uharibifu mkubwa.
ü Misitu pia itasaidia kuzuia gharika iletayo maafa.
ü -Wanyama na mimea itakuwa bila matatizo na yatokanayo na kemikali hatari na takataka nyingine.
ü Mito na maziwa yatakuwa na maji safi.

SABABU ZA KUTOFANYA VIZURI  KATIKA MITIHANI YA KITAIFA
ü uhaba wa walimu
ü uchache wa madarasa
ü uhaba wa vitabu/vifaa
ü kutokamilisha silabasi kwa wakati ufaao
ü Msongamano wa wanafunzi madarasani
ü Uzembe miongoni mwa walimu
ü migomo shuleni

MADHARA YANAYOTOKANA NA UFISADI
ü Kuharibika  kwa miundo msingi kwa vile barabara
ü Ufisadi huwafanya watu kukosa kufanya kazi vizuri
ü Wananchi kukata  tama wakati jasho lao hafalidiwi
ü Viwanda kuporomoka
ü Ufisadi umewatajarisha matajiri huku maskini wakidhulumiwa
ü Ufisad umesababisha ukosefu wa amani
ü Ufisadi umeendeleza ajali nyingi barabarani
ü Ufisadi umeendelea ajli nyingi bvarabarani
ü Ufisadi umesababisha ukosefu wa maadili katika jamii . k,m uavyaji wa mimba
ü Elimu umeadhirika kutokana na maafisa wafsadi

TAJA  MAMBO YANAYOCHANGIA VITA VYA UKABILA
Sababu
ü Siasa – vyama vya siasa
ü uchochezi kutoka kwa viongozi
ü Chuki na uhasama baina ya makabila
ü Umaskini
ü Ukosefu wa ajira
ü Vikundi haramu vya vijana k.m mungiki, sungusungu MRC nk
ü Ugaidi
ü Dhuluma za kihistoria
Mapendekezo
ü Wachochezi kuchukuliwa hatua za kisheria
ü Wananchi kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani
ü Serikali na washikadau kushirikiana ili kukabili tatizo la umaskini
ü Kubuni nafasi za ajira kwa vijana
ü Serikali kukabili vikundi haramu na ugaidi vilivyo

NAMNA KATIBA ILIVYOSHINDWA KUTIMIZA MALENGO YAKE KWA WANANCHI
ü Imeongeza gharama ya mishahara ya wabunge na wawakilishi hivyo kuacha mzigo kwa wananchi
ü Wananchi wengi wamesalia katika maisha ya ukata licha ya mabadiliko ya kikatiba
ü Licha ya katiba kubadilika viongozi walisalia wale wale wenye ufisadi, ukosefu wa utu, katili kutojali n.k
ü Haikupendekeza namna ya kutatua matatizo sugu yanayowakumba wanchi k.v ukosefu wa kazi
ü Serikali imetumia fedha nyingi kufanikisha utekelezaji wake badala ya kuunda miundo misingi ya kuboresha maisha
ü Kuwepo kwa viwango tofauti vya uongozi yaani serikali ya kitaifa  na kimajimbo kumezorotesha kasi ya maendeleo
ü Katiba haikupendekeza malipo / ajira ya wafanyakazi wa umma badala yake ikapendekeza tume kupiga msasa mishahara hiyo

JUHUDI ZA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...