This platform offers curated Secondary School Kiswahili/Swahili (Grammar and Literature) and History (Kenyan and World) learning content. We started it in 2020 during the COVID-19 school closures to help our students with homeschooling and ensure learning continued. Over time, it has attracted substantial viewership from students and teachers across the country, Africa, the U.S., Europe and beyond. I hope you find Homeschooling Hub beneficial. Best regards. ✍✍ππ
BLOG VISITORS
SEARCH HERE/ TAFUTA HAPA
Sunday, January 28, 2024
Saturday, October 23, 2021
UFAAFU WA ANWANI CHECHE ZA MOTO na KAKA BOLLO
UFAAFU WA ANWANI CHECHE ZA MOTO-MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO
Maana ya cheche-Cheche ni vijisehemu vya kitu chenye
mwangaza, vinavyotoa mwanga au mwangaza. Maana
ya cheche za moto- Vijisehemu vya moto vinvyoweza kusababisha moto vikiruka
na kutua katika mazingira yanayowezakusababisha/ kukuza moto. Katika riwaya ya Cheche za Moto, anwani hii inarejelea vitendo vinavyohatarisha
maisha ya wananchi wa kawaida, kuwaletea maumivu au hata vifo. Cheche za moto
katika riwaya hii zinatolewa na kiongozi Osman Jumbe, Askari Jeshi, Polisi,
kachero wa Osman Jumbe na vyombo vingine vya Dola.
Anwani hii inaifaa riwaya hii kwa sababu
inadokeza kwa undani mifano kadhaa ya cheche za moto kama ifuatavyo:
1. Askari
wanampiga Benta risasi kwake nyumbani na kutoweka na mumewe uk 14.
2. Askari
wanambaka mkewe Mule na wengine jumajiana na Mule kishoga uk. 5, 6
3. Mafuvu ya
vichwa vinajazwa kule The Red Valley wakati
wa utawala wa Osman Jumbe uk. 5
4. Askari
anamfyatua Mwanakombo risari na kumuua uk. 6/uk. 9
5. Askari
wanawa piga Mule, mkewe na Rita wanapowavamia uk. 3, 5
6. Wasichana na
wavulana wadogo kupigwa risasi uk. 23
7. Vita kati ya
askari Ali na askari jeshi watatu uk. 20
8. Polisi
anamuua kijana kwa kugombania mwanamke vilabuni uk. 25
9. Osman Jumbe
anawaambia Wahindi wa Malanga waondoke warudi kwao uk. 27
10. Masaba anatolewa kwake na askari baaba ya kuambiwa aiage familia yake uk. 35/37
KUNA MIFANO MINGINE ZAIDI YA HAMSINI KATIKA MWONGOZO WETU
MWONGOZO HUU PIA UMESHEHENI YAFUATAYO:
1. Wahusika na sifa zao
2. Dhamira ya mwandishi
3. Maudhui na maelezo yao
4. Mbinu za uandishi na mifano yao
5. Maswali ya kudurusu
JIPATIE NAKALA YA MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO
NUNUA MWONGOZO WA RIWAYA YA CHECHE ZA MOTO KUTOKA KWETU KWA SHILINGI 500 PEKEE
BONYEZA HAPA ILI KUNUNUA MWONGOZO-TUMA SHILINGI MIA TANO
PIA TUNAWAPA MAELEKEZO WANAFUNZI KATIKA RIWAYA YA CHECHE ZA MOTO
WASILIANA NASI KWA NAMBARI 0702371829 KWA MAELEZO ZAIDI
Saturday, August 21, 2021
UCHAMBUZI NA MWONGOZO WA RIWAYA YA CHECHE ZA MOTO na KAKA BOLLO
UCHAMBUZI WA CHECHE ZA MOTO
BONYEZA HAPA KUNUNUA MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO KWA SHILINGI 500
Uchambuzi wa Riwaya ya Cheche za Moto unashugulikia maswala makuu kama vile:
- Mtiririko wa vitushi na ploti,
- Wahusika na sifa zao,
- Dhamira ya mwandishi,
- Maudhui
- Na maswali ya kutarajiwa katika mitihani mbalimbali itakayi tahini riwaya hii.
Uchambuzi huo umeng'oa nanga na umeshika kasi. Baada ya mchakato mzima, tutachapisha makala hayo ya uchambuzi ambayo yatawafaa wakufunzi na wanafunzi kwa pamoja.
Kampuni hii itauza makala hayo kwa shilingi mia tano kwa kila nakala. Vilevile, tutachapisha baadhi ya sehemu za makala hayo humu ili kuwafaidi wale wanaotumia wavuti na simu za mkono kama njia ya kujielimisha.
TUNAWAKUMBUSHA wasomaji wetu kwamba tutachapisha video za uchambuzi wa makala haya katika YouTube kwa wale wanaoelimika bora kwa kusikiliza na kutazama. Kwa hivyo tunawakumbusha wasomaji wetu ku-SUBSCRIBE channel yetu ili kupata ujumbe kuhusu makala/video hizo tunapoyaweka au kuyapakia humo.
Kuuliza swali, andika swali lako kwenye sehemu ya "comment" hapa chini.ππππππ
Wednesday, June 9, 2021
VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021
VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021
Wednesday, February 24, 2021
TAMTHILIA YA KIGOGO: SUMU YA NYOKA
TAMTHILIA YA KIGOGO: ATHARI YA SUMU YA NYOKA SAGAMOYO
1) Vifo- Ngao junior
2) Watu wanageuka vipofu-Mngweni kwa mama pima
3) Ukengeushi mf. Ngurumo
4) Kuanguka chini ovyo ovyo na kugaragara-walevi mangweni
5) Wanafunzi katika shule ya Majoka wamegeuka
vichwa maji- ni makabeji
6) Walevi hawafahamu athari za ulevi.
7) Hawaoni athari ya soko kufungwa- Chapakazi
8) Kupotosha vijana ( gume gume)
9) Kupotoka kwa maadili
10)Kuvunjika kwa ndoa
11)Waathiriwa wanatumiwa na viongozi kutekeleza maovu mf. Ngurumo
kumvinja Tunu muundi.
12)Utepetevu ( uzembe) wanashinda ulevini na kupoteza muda.
13)Kuwaunga mkono viongozi wasiowajibika baada ya kupewa
vipeni. ( vibaraka) kama vile Ngurumo
14)Kutumia lugha chafu/ matusi mf Ngurumo kumtusi Tunu.
15)Kukosa wachumba/ ukapera mf Ngurumo
16)Dharau-Ngurumo kumdharau Tunu na kumwimbia wimbo wa Kuolewa-wa Daudi
Kabaka
17)Kufuja pesa
18)Kutofuata maagizo – Chopi hakufuata maagizo ya kumuua Tanu.
Sunday, February 14, 2021
UJUMBE WA DHARURA KWA WALIMU WOTE
UJUMBE WA DHARURA KWA WAKUFUNZI WOTE
Ni mwaka mpya ambapo
mchakato wa mafunzo umeanzishwa tena rasmi baada ya kusitishwa mwaka uliopita
kutokana na janga la tandavu la Korona. Katika wiki chache ambazo tumekuwa
tukitimiza malengo yetu kwa kuwahudumia wanafunzi kwa njia ya mafunzo,
tumeshuhudia ukatili miongoni mwa mwao katika baadhi ya shule humu nchini. Ukatili
huu umehatarishs maisha ya walimu katika shule husika. Ni muhimu kutambua
kwamba usalama wako ni muhimu sana, kwa hivyo huna budi kuusisitizia. Zifuatazo
ni njia ambazo kulingana nami, zitaweza kutusaidia kuepuka ukatili na udhalimu
wa wanafunzi.
Zingatia jukumu kuu
ambalo uliajiriwa kutekeleza. Iwapo umesahau, rejelea barua yako ya kazi kutoka
kwa tume ya kuajiri walimu. Kila mara hakikisha kwamba umetimiza jukumula kutimiza jukumu lako, na kwa kiwango kinashoridhisha matarajio yako,
ya mwajiri na ya jamii. Kukosa kutimiza jukumu huweza ukazua uhasama wa
wanafunzi dhidi yako, jambo ambalo huenda likatishia usalama wako. Wanafunzi wa
sasa japo wamepungukiwa na motisha ya kujituma masomoni kutokana na athari za
mienendo na maisha ya kijamii, wanatambua wakati ambapo wanapokea huduma bora kutoka kwa Mwalimu na wakati ambapo wanapokea bora huduma.
Je, sheria inakupa
nguvu za kumwadhibu mwanafunzi? La. Ni muhimu kila mkufunzi kufahamu fika
kwamba sote (walimu na wanafunzi) tuko katika karne ambayo mawasiliano hayana
vizingiti. Yanapenya na kupokelewa na kila rika. Kwa hivyo tusipuuze ukweli kwamba
wanafunzi hawa wanafahamu kwamba adhabu ni kinyume cha sharia. Wakati mwingine
unaweza ukagundua kuwa mwanafunzi anapuuza hitaji lako la kumwadhibu akijua
kwamba unakiuka sharia.Wewe kama mkufunzi huenda ukakerwa na jambo hili. Kabla hasira
hazijakutawala, hebu jiulize iwapo kumpa mwanafunzi adhabu nimoja kati ka majukumu uliyokabidhiwa na tume.
Kupitia masomo ya
saikolojia kwenye vyuo mbalimbali tulikosomea ualimu, kila mwalimu aliyekuwa
makini kwa masomo hayo bila shaka anapaswa kuwa na uwezo wa kutambua ama kung’amua
fikra za wanafunzi kutokana na jinsi wanavyozungumza ama kutenda mambo yao. Iwapo
umegundua kisicho kawaida katika tabia na mienendo ya mwanafunzi, kinachoweza
kuhatarisha maisha yako, kumbuka kuwa ni muhimu kutahadhari kabla ya hatari.
Kwa mfano, ukimwona mwanafunzi na kifaa kisichohitajika shuleni kama kisu,
chukua hatua kwa kufuata mchakato unaofaa ili apikonywe kifaa hicho.
Mwanafunzi anapojeruhiwa
ama kwa behati mbaya, anapokufa mikonomi mwa Mwalimu, magari makubwa makubwa huja
skulini kumchukulia hatua mkufunzi husika. Mwalimu anapopitia yayo hayo mikononi
mwa wanafunzi, ni muhali kuona wakuu wakija kuwachukulia wanafunzi hatua. Hili
ni thibitisho tosha kwamba wewe kama Mwalimu, kila mja anaamini kuwa unauwezo wa kujilinda na kujihakikishia usalama wako. Kwa hiyo tambua
kwamba usalama wako unakutegemea wewe mwenyewe.
Saturday, December 26, 2020
KCSE ONLINE REVISION CLASS
KCSE ONLINE REVISION CLASS FOR KISWAHILI
BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA NA KUANZA KUDURUSU
CLICK HERE TO JOIN THE ONLINE CLASS
Tutafanya udurusu wa kazi ya kidato cha nne ili kujitayarishia mtihani wa kitaifa. Tutashughulikia mada vitengo vifuatavyo:
1. Sarufi 2. Ushairi 3. Insha 4. Isimujamii 5. Fasihi Andishi: Kigogo, Chozi la Heri na Tumbo Lisiloshiba.
Whatsapp Click here
TUTASHUGHULIKIA YAFUATAYO
Friday, September 11, 2020
Friday, July 17, 2020
USHAIRI KIKORONA
Thursday, July 16, 2020
SARUFI KIKORONA
-
KONSONANTI GHUNA NA SIGHUNA KONSONANTI GHUNA NA SIGHUNA Ughuna wa sauti, hasa konsonanti huchunguzwa kwa kuzingatia kigezo cha m...
-
MIUNDO YA NOMINO KATIKA NGELI ZA KISWAHILI Maana ya ngeli Ngeli ni makundi mbalimbali ambapo maneno ya Kiswahili yamegwaika. Ni miga...
-
BONYEZA HAPA ILI KUSOMA UFAAFU WA ANWANI -CHOZI LA HERI UTAFITI NYANJANI: UKUSANYAJI WA DATA YA FASIHI SIMULIZI Hiki ni ki...
SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS
PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...