BLOG VISITORS

Showing posts with label ushairi. Show all posts
Showing posts with label ushairi. Show all posts

Sunday, January 28, 2024

BEMBEA YA MAISHA: MASWALI MAKUU YA KUDURUSU ILI KUIELEWA RIWAYA KWA KINA

Bembea ya Maisha, iliyoandikwa na mwandishi hodari, Timothy Arege, ni riwaya iliyosheheni maudhui mengi, mbinu nyingi za uandishi, wahusika wengi na mtiririko mzuri wa vitushi. Maswahi haya yatakusaidia kuyaelewa mambo haya kwa undani.


ILI KUPATA MASWALI MENGINE MENGI....BONYEZA HAPA

Saturday, August 21, 2021

UCHAMBUZI NA MWONGOZO WA RIWAYA YA CHECHE ZA MOTO na KAKA BOLLO

 UCHAMBUZI WA CHECHE ZA MOTO

BONYEZA HAPA KUNUNUA MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO KWA  SHILINGI 500

 Uchambuzi wa Riwaya ya Cheche za Moto unashugulikia maswala makuu kama vile:

  •  Mtiririko wa vitushi na ploti, 
  • Wahusika na sifa zao, 
  • Dhamira ya mwandishi, 
  • Maudhui
  • Na maswali ya kutarajiwa katika mitihani mbalimbali itakayi tahini riwaya hii.

Uchambuzi huo umeng'oa nanga na umeshika kasi. Baada ya mchakato mzima, tutachapisha makala hayo ya uchambuzi ambayo yatawafaa wakufunzi na wanafunzi kwa pamoja.

Kampuni hii itauza makala hayo kwa shilingi mia tano kwa kila nakala. Vilevile, tutachapisha baadhi ya sehemu za makala hayo humu ili kuwafaidi wale wanaotumia wavuti na simu za mkono kama njia ya kujielimisha.

TUNAWAKUMBUSHA wasomaji wetu kwamba tutachapisha video za uchambuzi wa makala haya katika YouTube kwa wale wanaoelimika bora kwa kusikiliza na kutazama. Kwa hivyo tunawakumbusha wasomaji wetu ku-SUBSCRIBE channel yetu ili kupata ujumbe kuhusu makala/video hizo tunapoyaweka au kuyapakia humo. 

BONYEZA HAPA ILI KUSUBSCRIBE

Kuuliza swali, andika swali lako kwenye sehemu ya "comment" hapa chini.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡


Friday, July 17, 2020

USHAIRI KIKORONA

            

         Soma shairi lifuatalo kwa kina kisha ujibu maswali yanayofuata

1.         Natunga nikiwaasa, msije kujijutia,
Mitego sije wanasa, mkaja kuangamia
Tamaa nyingi za pesa, gereza, zitawatia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


2.         Jela inamkonyeza, kama hutajizuwia
Haina ndugu gereza, jela si ya kuchezea,
Inajuvya na kupoza, wenye nguvu kutulia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


3.         Rushwa si kitu chema, walaji jihadharini,
Mkila zitawakwama, zitawatoka puwani,
Wazilao hulalama, si mimi ila Fulani
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


4.         Ridhika na upatacho, kama moja au mbili,
Usitaraji mkocho, upatao, bwana Ali,
Tama zako za macho, zitakulea mbuli
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


5.         Ni mema kemukemu, wenye vyeo kutumia
Maleba wakiwahimu, rushwa kuwaletea,
Muogopeni karimu, leba haombwi rushwa,
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza

6.         Kuna wengi mahakimu, haki wanazopinduwa,
Yatima huwa dhulumu, kwa kupapia rushwa
Kwa kutaka darahimu, aso haki anapewa
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza

Maswali
(a)   Andika kichwa mwafaka cha shairi hili .                                                                  (al.1)
(b)   Taja madhara manne ya rushwa.                                                                               (al.4)
(c)   Eleza  umbo la shairi hili.                                                                                          (al.4)
(d)  Andika ubeti wanne katika lugha nathari.                                                                 (al4)
(e)   Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika shairi hili.                      (al.3)

(f)   Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili .                        (al.4)
(i)              Gereza
(ii)            Mkocho
(iii)          Karimu
(iv)          Darahimu



Tuesday, April 14, 2020

USHAIRI: SHAIRI HURU


MFANO WA SHAIRI HURU


SEHEMU YA A: USHAHIRI
                                    SHAIRI ‘A’
            (i)                    Umekata mti mtima
                                    Umeangukia nyumba yako
                                    Umeziba mto hasira
                                    Nyumba yako sasa mafurikoni
                                    Na utahama
                                    Watoto wakukimbilia

            (ii)                   Mbuzi kumkaribia chui
                                    Alijigeuza panya
                                    Akalia kulikuwa na paka
                                    Kichwani
                                    Mchawi kutaka sama kutisha
                                    Alijigeuza samba
                                    Akalia na risasi kichwani

            (iii)                  Jongoo wapi sasa yatakwenda
                                    Bwanako kumpa sumu?
                                    Hadija umeshika nyoka kwa mkia
                                    Hadija umepitia nyuma ya punda
Jogoo kataka sana kukimbia
Aliomba miguu elfu

(iv)                  Akaachwa na nyoka
Hadija wapi sasa
Bwanako kumpa sumu?
Hadija umashika nyoka kwa mkia
Hadija amepita nyuma ya punda

SHAIRI ‘B’
                                    Piteni jamani,piteni haraka
                                    Nendeni ,nendeni huko mwendako
                                    Mimi haraka, haraka sina
                                    Mzigo wangu,mzigo mzito mno
                                    Na chui sitaki kuweka

                                    Vijana kwa nini hampiti?
                                    Kwa nini mwanicheka kisogo?
                                    Mzigo niliobeba haupo.

                                    Lakini umenipinda mgongo na
                                    Nendako
                                    Haya piteni!piteni haraka!Heei!

                                    Mwafikiri mwaniacha nyuma!
                                    Njia ya maisha ni moja tu.
                                    Huko mwendako ndiko nilikotoka
                                    Na nilipofikia wengi wenu
                                    Hawatafika

                                    Kula nimekula na sasa mwasema
                                    Niko nyuma ya wakati
                                    Lakini kama mungepita mbele
                                    Na uso wangu kutazama
                                    Ningemwambia siri ya miaka
                                    Mingi

Maswali
(a)Haya ni mashairi ya aina gani?Toa sababu.     (Alama 2)

(b)Washairi hawa wawili wanalalamika.Yafafanue malalamishi yao.             (Alama 4)

(c)Onyesha jinsi kinaya kinavyotokeza katika tungo hizi mbili. (Alama4)                                                                                                                                         
(d)       Ni vipi Hadija :-
  (i) Amekata mti mtima?    (Alama 2)                                              
 (ii)       Amepita nyuma ya punda. (Alama 2)

(e) Toa mifano miwili ya uhuru mshairi kwa kurejelea mashairi haya.            (Alama 2)

(f)        kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:-
                                    (i)        Mzigo
                                    (ii)       Siri
                                    (iii)      Kula nimekula
           (iv)      Niko nyuma ya wakati.(Alama 4)
                                           
###KWA MASWALI YA FASIHI SIMULIZI, GUSA HAPA###

###KWA MASWALI YA KIGOGO, BONYEZA HAPA###

###KWA MASWALI YA TUMBO LISILOSHIBA, GUSA HAPA###

Uliza swali moja kwa moja kupitia <WHATSAPP>

POST A COMMENT DOWN THERE πŸ‘‡

USHAIRI: SHAIRI LA ARUDHI

SOMA SHAIRI HILI KISHA UJIBU MASWALI YANAYOFUATA (ALAMA 20)
MFANO WA SHAIRI LA ARUDHI
      
Ulimwengu ulimwengu, ulimwengu naratibu
Yaliyo kichwani mwangu, nataka kuyahutubu
Wayasome ndugu zangu, wa mbali na karibu
Cha wenye raha na taabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ulimwengu ni kiwanja, chenye raha na tabu
Wengine wanajikonja, kwa wengine ni adhabu
Kuta na kucha twahanja, kutafuta matulubu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa balaa, aliniusia babu
Mna mambo yamejaa, ya faraja na kusibu
Na machache ya kufaa, ila mengi ya udubu
Cha wenye raha na tabu ulimwengu ni kiwanja.

Ni kiwanja cha Amina, Saidi Ali Rajabu
Wengune kitu hatuna, tunaishia kababu
Wale wamejaza sana, wanashindwa kuhesabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa urongo, na kweli pia ajabu
Kichwa hudanganya shingo, tumbo kiuno chasibu
Usitumai ubongo, wa nduguyo na swahibu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa walevi, pombe kwao ni dhahabu
Mara vile mara hivi, wakilewa majudhubu
Maneno ya kiujuvi, hujipaka hata shabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni kiwanja wenye dini, watiio Wahabu
Mashekhe misikitini, humo hufanya muhibu
Mapadri kanisani, huvihubiri vitabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa malofa, lofa mtu mwenye tabu
Kusema sana kashifa, na moyo kisebusebu
Tunakaribia kufa, kwa kushindwa kujimudu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa faraja, alowajali habibu
Na mengine sitotaja, msinambe nina gubu
Ni uwanja wa viroja, vigumu kuvikutubu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

MASWALI

a.      Lipe shairi hili anwani mwafaka. (al. 1)

b.     Ainisha shairi hili katika bahari mbili na utoe dhibitisho. (al. 2)
c.      Bainisha uhuru wa mtunzi wa shairi hili (al. 2)

d.     Eleza muundo wa shairi hili. (al. 5)

e.      Andika ubeti wa tano kwa lugha tutumbi. (al. 4)

f.       Fafanua mbinu zozote mbili za uandishi zilizotumika katika shairi (al. 4)

g.      Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika takika shairi.(al. 2)
i. Balaa
ii. Kisebusebu


##Kwa  Tumbo lisiloshiba, GUZA HAPA ##


POST A COMMENT DOWN THERE πŸ‘‡

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...