BLOG VISITORS

Showing posts with label tumbo lisiloshiba. Show all posts
Showing posts with label tumbo lisiloshiba. Show all posts

Wednesday, June 9, 2021

VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021

VITABU VIPYA VYA FASIHI ANDISHI VYA SHULE ZA UPILI 2021

Subscribe to our Youtube Channel for updates on CHECHE ZA MOTO analysis videos and other updates
Click here> YouTube


Wizara ya Elimu imeidhinisha vitabu vipya vya fasihi andishi vitakavyosomwa, kuchambuliwa na kutahiniwa katika shule za upili kote nchini.

CHECHE ZA MOTO iliyoandikwa na John Habwe na kuchapishwa na Jomo Kenyatta Foundation (JKF) ndiyo riwaya ambayo itachukua nafasi ya riwaya ya Chozi la Heri ya Asumpta K. Matei.

Hadithi fupi, MAPAMBAZUKO YA MACHWEO iliyochapishwa na kampuni ya ushapishaji ya Mountain Top ndiyo itachukua nafasi ya Tumbo Lisiloshiba na hadithi nyingine iliyohaririwa na Alifa Chokocho na Dumu Kayanda.

Wizara ya elimu imeidhinisha vitabu hivi baada ya miaka minne ya kutahiniwa kwa Chozi la Heri na Tumbo Lisiloshiba. 

Wakufunzi wameelezea matarajio makuu kwamba Cheche za Moto huenda ikawa nyepesi kwa wanafunzi kuelewa hasa kwa kuzingatia mtitiriko wa vitushi na idadi ya wahusika. Baadhi ya walimu wamedokeza kwamba riwaya inayoondoka imekuwa changamoto kwao na kwa wanafunzi kwa sababu imeshishirikisha wahusika chungu nzima. Vilevile, walimu hao wameeleza kwamba riwaya Chozi la Heri imekuwa na uchangamano mwingi katika muundo wake.

Kwa upande mwingine, wanafunzi waliohojiwa na Homeschool Kenya wamepongeza watunzi mbalimbali wa hadithi katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba. Wanafunzi hao wamedokeza kwamba hadithi hizo mbali na kuburudisha, zimesheheni ujumbe muhimu kwa wanafunzi wote. Nilipowauliza kuhusu changamoto walizokumbana nazo katika usomaji wao wa Tumbo Lisiloshiba, wanafunzi hao walisisitiza kwamba hadithi hizo zimekuwa nyepesi kuelewa.

Tunashughulikia uchambuzi wa Cheche za Moto na Mapambazuko ya Machweo na baada ya siku chache tutachapisha makala hayo humu kwenye blogu kwa manufaa yetu sote. Ahsanteni.


Wasiliana nasi Kupitia WhatsApp. 

Kwa makala mengine gusa yafuatayo:


 

Wednesday, February 24, 2021

TAMTHILIA YA KIGOGO: SUMU YA NYOKA

TAMTHILIA YA KIGOGO: ATHARI YA SUMU YA NYOKA SAGAMOYO

#Wasiliana nasi. Bonyeza hapa

 


Athari za sumu ya nyoka

1)    Vifo- Ngao junior

2)    Watu wanageuka vipofu-Mngweni kwa mama pima

3)    Ukengeushi mf. Ngurumo

4)    Kuanguka chini ovyo ovyo na kugaragara-walevi mangweni

5)    Wanafunzi katika shule ya Majoka wamegeuka vichwa  maji- ni makabeji

6)    Walevi hawafahamu athari za ulevi.

7)    Hawaoni athari ya soko kufungwa- Chapakazi

8)    Kupotosha vijana ( gume gume)

9)    Kupotoka kwa maadili

10)Kuvunjika kwa ndoa

 #Nunua Mitihani@Kshs. 100

11)Waathiriwa wanatumiwa na viongozi kutekeleza maovu mf. Ngurumo kumvinja Tunu muundi.

12)Utepetevu ( uzembe) wanashinda ulevini na kupoteza muda.

13)Kuwaunga mkono viongozi  wasiowajibika baada ya kupewa vipeni. ( vibaraka) kama vile Ngurumo

14)Kutumia lugha chafu/ matusi mf Ngurumo kumtusi Tunu.

15)Kukosa wachumba/ ukapera mf Ngurumo

16)Dharau-Ngurumo kumdharau Tunu na kumwimbia wimbo wa Kuolewa-wa Daudi Kabaka

17)Kufuja pesa

18)Kutofuata maagizo – Chopi hakufuata maagizo ya kumuua Tanu.

 #TAZAMA MADA YA ZIADA KWENYE YOUTUBE

1. CHOZI LA HERI

2. TUMBO LISILOSHIBA

3. KIGOGO

4. FASIHI SIMULIZI

TOA MAONI HAPA KWENYE SEHEMU YA MAONIπŸ‘‡

Saturday, December 26, 2020

KCSE ONLINE REVISION CLASS

KCSE ONLINE REVISION  CLASS FOR KISWAHILI

BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA NA KUANZA KUDURUSU

CLICK HERE TO JOIN THE ONLINE CLASS


Tutafanya udurusu wa kazi ya kidato cha nne ili kujitayarishia mtihani wa kitaifa. Tutashughulikia mada vitengo vifuatavyo:

1. Sarufi 2. Ushairi 3. Insha 4. Isimujamii 5. Fasihi Andishi: Kigogo, Chozi la Heri na Tumbo Lisiloshiba.

Wasiliana nasi kwa 0702371829

Whatsapp Click here


TUTASHUGHULIKIA YAFUATAYO


1. KARATASI YA KWANZA: INSHA
        A. Insha ya Kiuamilifu/Ya lazima
        B. Insha ya Mjadala
        C. Insha Methali
        D. Insha ya Mdokezo

2. KARATASI YA PILI
        A. Ufahamu
        B. Uarufifupisho
        C. Sarufi
        D. Iimujamii

3. KARATASI YA TATU
        A. Ushairi
        B. Fasihi Andishi: Kigogo, Chozi la Heri, Tumbo Lisiloshiba
        C. Fasihi Simulizi
      
Add a comment in the comment section/ Toa maoni au uliza swali katika sehemu ya maoni hapa chiniπŸ‘‡

Friday, September 11, 2020

Tuesday, June 30, 2020

PANUA BONGO NA FASIHI




 1.   LAZIMA
       “Asante ya punda kweli ni mateke. Sikujua ungekuja kunihangaisha ...”
       a)    Weka dondoo hili katika muktadha wake.     (alama 4)
       b)    Onyesha jinsi msemewa anamwangaisha msemaji.    (alama 2)
       c)    Kwa kurejelea tamthilia nzima onyesha ukweli wa methali “Asante ya punda ni mateke.”       (alama 14)

 HADITHI FUPI
       Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
2.    “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
       a)    Eleza muktadha wa dondoo hili.     (alama 4)
       b)    Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.            (alama 4)
       c)    Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ?       (alama 6)
       d)    Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.       (alama 6)
3.    Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.    (alama 20)

  Kigogo
       Tibu swali la 2 au 3 
2. Tusiwaruhusu watu wachache waliojazwa kasumba….kuturejesha ….hatuwezi kukubali kutawaliwa
    kidhalimu tena.
              a.    Eleza muktadha wa dondoo hili.     
              b.    Kwa kumrejelea mzungumzaji wa maneno haya, bainisha unafiki katika kauli hii. (alama 16)
  3. Eleza jinsi mbinu ya taharuki ilivyotumika kufanikisha maudhui katika tamthilia ya kigogo.                               (ala 20)

HADITHI FUPI
              Eunice Kimaliro :  Mtihani wa Maisha.
4. “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
              a.   Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                       
              b.   Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.  (alama 6)
              c.   Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili. 

              Alfa Chokocho  :  Tulipokutana tena

5. a.   “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
       i)   Eleza muktadha wa dondoo hili.          
       ii)  Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii. 
    b. Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”   

2.  “ Do ! Do ! Simameni ! Simameni leo kutanyesha mawe! “
i)   Eleza muktadha wa dondoo hili.  
ii) Fafanua mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo    
iv) Dhihirisha kwa kuzingatia hoja sita jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika tamthilia ya  “ Kigogo.”      (alama 12)

3) Eleza kwa kutolea mifano mitano mitano jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu za :
     i) majazi                          
     ii)mbinu rejeshi                

SEHEMU C: HADITHI FUPI
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
4. i)  Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo : (alama 20) 
           a) Mapenzi ya Kifaurongo
           b) Shogake dada ana Ndevu
           c) Mwalimu   Mstaafu
           d) Mtihani wa maisha
          
5) ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’
i)  Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba                    (al 10)
ii)  Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.                       (al 10)   

    
6. Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe macho”.                                                
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.  
(b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.  
(c) Ushauri uliotolewa na msemaji baadaye kama njia mojawapo ya kuwa macho ni wa kidhalimu.  Fafanua.          (alama 4)
(d) Eleza namna unafiki wa msemaji na upumbavu wa mnenewa unavyodhihirika katika muktadha wa dondoo hili.(alama   
(e) Onesha jinsi ukweli wa kauli hii ulivyojitokeza baadaye katika tamthilia.    

3. Jadili migogoro inayojitokeza katika tamthilia ya kigogo, kisha utathmini namna ilivyosuluhishwa.    (alama 20)

       SEHEMU YA C:HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
Jibu swali la 4 au 5
4. “Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a)   Eleza muktadha wa dondoo hili      (alama 4)
(b)  Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.   (alama 4)
(c)   Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya  (alama 6)
(d)  Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita      (alama 6)
5.Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii.  Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.  (alama 20)
“ Mguu huu ni wako”
·       Eleza muktadha wa dondoo hili   (al. 4)
·       Ni tamathali gani ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. Eleza maana yake  (al.2)
·       Msemewa alipewa ahadi zipi   (al. 5)
·       Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji  (al. 9) 
5 Eleza mbinu ya
·       Majazi    (al.10)
·       Kinaya   (al.10)


6. TUMBO LISILOSHIBA
Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo lisiloshiba   (Diwani)

7 “Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimamia juu ya              ardhi hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili  (al. 4)
b Eleza sifa nne za msemaji   (al. 4)
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili (al. 2)
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina tumbo lisiloshiba (al. 10)
“Oooh bebi,  miaka yaenda mbio sana, nayo  sura yako inachujuka……”
a)   Weka dondoo hili  katika muktadha wake.  (alama 4)
b)   Mhusika anayehusishwa na wimbo  huu ana msimano gani wa kimapinduzi?( 8)
c)   Taja sifa zozote nane za muhusika huyu   (alama 8)
5.   Tamthilia ya ‘Kigogo’ ni kioo cha  uhalisia wa maisha ya jamii nyingi  za kiafrika.  Thibitisha.               (alama 20)

SEHEMU YA D:  HADITHI FUPI TUMBO LISILOSHIBA  NA HADITHI NYINGINEZO
Jibu swali la 6 au la 7
6.    “Rasta twambie bwana!”
a)   Weka dondo katika muktadha  (ala 4)
b)   Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi  katika dondoo hili  (ala 2)
c)   Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe?  ( 4)
d)   Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya hadithi hii. (alama10 )

7.  Jadili mashaka ya Mashaka  katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”  (alama 20
2.  “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni wake huwajui.”
(i)  Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
     (ii)    Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo, thibitisha ukweli wa dondoo           hili. (al.14)
(ii) Taja tamathali za usemi zilizotumika katika dondoo hili.  (al.2)
3.  Eleza mbinu alizotumia majoka kuendeleza uongozi wake.  (al.20)

HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA.
6.Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki.               (al.20)

Tumbo lililoshiba na Hadithi nyingine
      4.   "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
      a) Eleza muktadha wa dondoo hii.   (alama 4)
      b) Taja naufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.  (alama 4)
      c)Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima.  (alama 6)
      d)Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo.  (alama 6)
    
5. Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
      a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
      b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. (alama 10)
 c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo. (alama 6)

KIGOGO   Pauline Kea
“Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko.”
a)          Weka maneno haya katika muktadha wake.  (alama 4)
b)          Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili  (alama 2)
c)          Kando na kufungiwa soko, Wanasagmoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka  (alama 5)
d)          Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 9)

SEHEMU C:  HADITHI FUPI :TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

Thursday, June 11, 2020

MAUDHUI TAWALA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA


MAUDHUI TAWALA KATIKA DIWANI YA TUMBO LISILOSHIBA
Makala haya yanashughulikia baadhi ya maudhui ambayo yanajitokeza katika zaidi ya hadithi moja katika msururu wa hadithi katika hadithi fupi ya Tumbo Lisiloshiba.
MAUDHUI
HADITHI
MIFANO
Umasikini
1.     Tumbo Lisiloshiba
2.     Mapenzi ya Kifaurongo
3.     Ndoto ya Mashaka
4.     Nizikeni papa hapa
1.     Eneo la Madongoporomoka na Wanaoishi hapo.
2.     Dennis Machora na wazazi wake.
3.     Nyanya yake Mashaka na Mashaka mwenyewe.
4.     Otii na watu wa nyumbani.
Utabaka
       I.          Tumbo lisiloshiba
    II.          Mapenzi ya Kifaurongo
  III.          Shibe inatumaliza
   IV.          Ndoto ya Mashaka
     V.          Kidege
I.       Matajiri wanaomiliki majumba mijinina masikini wa Madongoporomoka.
II.    Familia ya Dennis ni masikini ilhali ya Panina ni tajiri.
III.  Nyanya yake Mashaka ni masikini ilhali wazazi wake Penina ni matajiri.
IV.   Videge na visamaki.
Elimu
1)    Mame Bakari
2)    Mapenzi ya Kifaurongo
3)    Shogake Dada ana Ndevu
4)    Mwalimu Mstaafu
5)    Mtihani wa Maisha
1)    Sara anabakwa na Janadume anapotoka kusoma.
2)    Dennis Machora, Penina na wanafunzi wengine wako chuoni. Daktari Mabonga pia.
3)    Mwalimu Mstaafu Mosi anawafunza wanafunzi wengi.
4)    Samweli Matandiko anafeli mtihani. Dada zake Bilha na Mwajuma pia wanasoma katika shule ya Busukalala.
Tamaa
a)    Tumbo Lisiloshiba
b)    Shibe inatumaliza
c)     Mkubwa
d)    Mapenzi ya Kifaurongo
a)    Viongozi wanatamani ardhi ya Wanamadongoporomoka. Jitu lina tamaa.
b)    Sasa na Mbura wanakula kupita kiasi kutokana na tamaa.
c)     Mkubwa anatamani awe kiongozi ili aifanye vyema biashara ya unga.
d)    Penina anatamani Dennis Machora awe mpenzi wake.


Ukatili
1.     Mapenzi ya Kifaurongo
2.     Tumbo Lisiloshiba
3.     Mtihani wa Maisha
4.     Kidege
5.     Mame Bakari
1.     Penina anafukuza Dennis Machora kutoka kwake baada ya Dennis kukosa kazi.
2.     Askari wa Baraza la mji wanabomoa vibanda vya wenyeji. Jeshi la polisi linawapiga virungu watu wasio na kosa.
3.     Babake Samweli Matandiko anampa Kamba ili ajimalize baada ya Samweli kutaka kujiua.
4.     Midege inavivamia visamaki na kuanza kuvila.
5.     Watu wanalivamia jitu ambalo lilimbaka Sara na kuliua kwa matofali.
Ushirikiano
A.     Tumbo Lisiloshiba
B.     Ndoto ya Mashaka
C.     Nizikeni Papa Hapa

A.     Wanamadongoporomoka wanatumia umoja wao kuhakikisha kwamba ardhi yao haijanyakuliwa.
B.     Wanyonge wanashirikiana kuandaa maandamano ambayo yanabadilisha maisha na kila kitu kunakuwa sawa. Utabaka unaisha.
C.     Wanachama wa Chama cha Watu wa wanashirikiana na kumchangia Otii pesa za kumsafirisha kwa nyumbani Sidindi.
Uozo katika Jamii
1.     Tumbo Lisiloshiba
2.     Shogake Dada ana Ndevu
3.     Shibe Inatumaliza
4.     Mame Bakari
5.     Masharti ya Kisasa
6.     Nizikeni Papa Hapa
7.     Mkubwa
8.  Kidege

1.     Ukatili wa Jitu na Askari wa Baraza la Mji
2.     Safia kufanya mapenzi na shogake badala ya kusoma.
3.     Ulafi wa Mzee Mambo, Sasa, Mbura na Dj.
4.     Kubakwa kwa Sara na Janadume.
5.     Kukosa uaminifu katika ndoa.
6.     Mapuuza/ maradhi kutokana na mapenzi ya kiholela
7.     Uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya.
8.  Joy na Achesa wanabingiria na kutulia huku midomo yao anashikana. Ishara ya mapenzi hadharani.

MADA ZAIDI ZILIZOSHUGHULIKIWA- TUMBO LISILOSHIBA

  1. WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
  2. UFAAFU WA ANWANI TUMBO LISILOSHIBA
  3. MASWALI YA TUMBO LISILOSHIBA
  4. MTIHANI WA MAISHA
BONYEZA HAPA KUSOMA NGELI

Uliza swali moja kwa moja kupitia <WHATSAPP>

Post your comment/question in the comment section below πŸ‘‡


SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...