BLOG VISITORS

Saturday, October 23, 2021

UFAAFU WA ANWANI CHECHE ZA MOTO na KAKA BOLLO

 UFAAFU WA ANWANI CHECHE ZA MOTO-MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO

Maana ya cheche-Cheche ni vijisehemu vya kitu chenye mwangaza, vinavyotoa mwanga au mwangaza. Maana ya cheche za moto- Vijisehemu vya moto vinvyoweza kusababisha moto vikiruka na kutua katika mazingira yanayowezakusababisha/ kukuza moto. Katika riwaya ya Cheche za Moto, anwani hii inarejelea vitendo vinavyohatarisha maisha ya wananchi wa kawaida, kuwaletea maumivu au hata vifo. Cheche za moto katika riwaya hii zinatolewa na kiongozi Osman Jumbe, Askari Jeshi, Polisi, kachero wa Osman Jumbe na vyombo vingine vya Dola.

Anwani hii inaifaa riwaya hii kwa sababu inadokeza kwa undani mifano kadhaa ya cheche za moto kama ifuatavyo:

1.   Askari wanampiga Benta risasi kwake nyumbani na kutoweka na mumewe uk 14.

2.   Askari wanambaka mkewe Mule na wengine jumajiana na Mule kishoga uk. 5, 6

3.   Mafuvu ya vichwa vinajazwa kule The Red Valley wakati wa utawala wa Osman Jumbe uk. 5

4.   Askari anamfyatua Mwanakombo risari na kumuua uk. 6/uk. 9

5.   Askari wanawa piga Mule, mkewe na Rita wanapowavamia uk. 3, 5

6.   Wasichana na wavulana wadogo kupigwa risasi uk. 23

7.   Vita kati ya askari Ali na askari jeshi watatu uk. 20

8.   Polisi anamuua kijana kwa kugombania mwanamke vilabuni uk. 25

9.   Osman Jumbe anawaambia Wahindi wa Malanga waondoke warudi kwao uk. 27

10. Masaba anatolewa kwake na askari baaba ya kuambiwa aiage familia yake uk. 35/37    

          KUNA MIFANO MINGINE ZAIDI YA HAMSINI KATIKA MWONGOZO WETU

MWONGOZO HUU PIA UMESHEHENI YAFUATAYO:

1. Wahusika na sifa zao

2. Dhamira ya mwandishi

3. Maudhui na maelezo yao

4. Mbinu za uandishi na mifano yao

5. Maswali ya kudurusu

JIPATIE NAKALA YA MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO 

            NUNUA MWONGOZO WA RIWAYA YA CHECHE ZA MOTO KUTOKA KWETU KWA SHILINGI 500 PEKEE

            BONYEZA HAPA ILI KUNUNUA MWONGOZO-TUMA SHILINGI MIA TANO

PIA TUNAWAPA MAELEKEZO WANAFUNZI KATIKA RIWAYA YA CHECHE ZA MOTO

WASILIANA NASI KWA NAMBARI 0702371829 KWA MAELEZO ZAIDI

ULIZA SWALI AU TOA MAONI KATIKA SEHEMU YA MAONI HAPA CHINIπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡


SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...