MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
(a) Linanisha na utofautishe
sauti zifuatazo (al.2)
(i) /th/,/dh/
(c) Tunga sentensi inayodhihirisha (al.4)
(i) Nomino ya wingi
(ii) Kitenzi kishirikishi kuipungufu
(d) Tumia jozi ya maneno
yafuatayo kutunga sentenzi moja (al.2)
Fumba na vumba
(e) Tofautisha matumizi ya
ngali katika sentenzi zifuatazo; (al.2)
(i) Wanafunzi wangali wanasherehekea
(ii) Wanafunzi wetu
wangalisoma wangalipita mtihani
(f) Tumia ‘O’ rejeshi ili
kudhihirisha hali ya mazoea (al.2)
Mgonjwa ambaye
anakula lishe bora ndiye ambaye atapona haraka
(g) Bainisha aina za virai
katika sentensi ifuatayo (al.3)
Walimshangilia
mgeni wao kwa shangwe
(h) Ainsha viambishi katika
neno lifuatalo (al.3)
Tutakayempiga
(i) Bianisha aina za yambwa
katika sentensi ifuatayo (al.3)
Mkulima aliyekata
nyasi kwa mundu amewalisha punda
(k) Andika katika usemi
halisi (al.2)
Robi alisema kuwa
ilikuwa lazima wao waonyeshe heshima kwa watu wote ikiwa walitaka kuendelea vyema maishani.
(i) Sahihisha sentensi
zifuatazo (al.2)
(i) Mbona haujaenda
sokoni
(ii) Penye niliandika ni hapo
(m) Andika katika ukubwa (al.2)
Wazee hawa wana wake
na watoto wengi
(n) Changanua sentensi
ifuatayo kwa njia ya visanduku (al.3)
Motto aliyekamatwa
jana ni mwizi
(o) Unda nomino mbili
kutokana na kitenzi ‘chuma’ (al.2)
(p) Andika kinyume cha: (al.2)
Furaha anajenga nyumba mjini
(q) Nyambua vitenzi
vifuatavyo katika kauli ya kutendeshea na kutendeshwa (al.2)
(i) Fa
(ii) Nywa
(r) Kanusha sentensi
ifuatayo (al.1)
Ningelikuwa na pesa
ningelinunua kitanu kile
ISIMU JAMII (Alama 10)
Eleza kwa kutolea
mifano dhana zofuatazo
(a) Sajili
(b) Lafudhi
(c) Lahaja
(d) Lingua franka
(e) Krioli