UTAFITI NYANJANI:
UKUSANYAJI WA DATA YA FASIHI SIMULIZI
Hiki ni kitendo cha kwenda katika jamii fulani na kukusanya data inayohitajika na kuichambua.
UMUHIMU WA UTAFITI NYANJANI KATIKA FASIHI SIMULIZI
ü Huwezesha kuendelezwa kwa utamaduni wa jamii mbalimbali
ü Hukuza na kuendeleza somo la fasihi simulizi.
ü Huzia kupotea kwa fasihi simulizi.
ü Hushughulikia mambo mapya ambayo hayakushughulikiwa hapo
mwanzoni.
ü Hukuza na kusambaza maarifa na ujumbe wa fasihi simulizi kwa
jamii pana.
ü Humpa mwanafunzi mbinu za utafiti anazoweza kutumia katika
masomo mengine.
ü Huibua na kukuza vipawa vya watafiti kama vile utambaji,
uigizaji, usogora na kadhalika.
HATUA ZA KUFANYA UTAFITI
1)
Maandalizi: Huhusisha mambo yafuatayo:
i. Uteuzi wa mada ya utafiti
ii. Kubainisha na kueleza
malengo ya utafiti huo.
iii. Kutambia eneo la kufanyia
utafiti
iv. Kutambua utafiti ambao
tayari ulifanywa kuhusu mada yako.
v. Kukadiria gharama katika
shughuli nzima.
2) Ukusanyaji
wa Data yenyewe
Ukusanyaji unawezakufanywa
kupitia jia hizi:
ü Kushuhudia
ü Kujaza fomu
ü Kushiriki
ü Kuhoji nk
3) Kurekodi
Data yako
Unahitaji kurekodi data
zako kupitia njia zifuatazo:
ü Kuandika
ü Kupiga picha
ü Kuchukua video
ü Kunasa habari nk
4) Kuchunguza
Data
Data ambayo umekusanya
inahitaji kuchunguzwa, kufsiriwa na kuandikwa upya, neno baada ya neno ili
maana halisi inayokusudiwa isipotezwe.
5) Kuchambua
na kufasili Data
Data uliyokusanya inahitaji
kuchambuliwa, kulinganishwa, kufasiliwa, kutathminiwa na kisha kujumuishwa ili
kupata matokeo kamili ya utafiti wako.
TO SUPPORT US, DONATE TO US ON MPESA 07-02-37-18-29
MBINU ZA KUKUSANYA DATA