MAUDHUI YA NDOA KATIKA CHOZI LA HERI
Ndoa ni
makubaliano rasmi ya mwanaume na mwanamke kuishi pamoja kama mume na mke. Pia huitwa
chuo. Katika riwaya ya Chozi la Heri, maudhi
ya ndoa yanajitokeza baina wahusika mbalimbali. Ndoa hizi zinakumbwa na
changamoto tofauti tofuti huku zingine zikisambaratika na zingine zikiimarika. Mifano
ya ndoa riwayani ni kama yafuatayo:
Ndoa kati ya
Mwimo Msubili na wake zake kumi na
wawili akiwemo mamake Ridhaa. Ridhaa ni mmoja wa zao la ndoa hili.
Ndoa kati ya Ridhaa na Terry. Wanaozaliwa
kutokana na ndoa hii ni Mwangeka,
Annatila(Tila) Dede na Mukeli.
Ndoa kati ya
Mwangeka na Lily Nyamvula. Becky anazaliwa kutokana na ndoa hii lakini anaangamia
katika mkasa wa kuchomwa kwa jumba la Ridhaa. Lily pia anateketea katika mkasa
huo.
Ndoa kati ya
Racheal Apondi na Mandu. Wanamzaa Sophie. Mandu anaaga vitani anapoenda
kulinda Amani ughaibuni.
Ndoa kati ya
Mwangeka na Racheal Apondi baada ya
wawili hawa kufiwa na wenzao katika ndoa zao za kwanza. Wanamzaa Ridhaa.
Ndoa kati ya
Kaizari na Subira. Lime na Mwanaheri ni mazao ya ndoa hii.
Ndoa kati ya
kangata (mfanyikazi wa Kiriri) na Ndarine. Wanawazaa Lunga
Kiriri Kangata, Akelo Kiriri-Kaango na Lucia Kiriri Kangata.
Ndoa kati ya
Akelo Kiriri na Kaango. Wawili hawa
wanawazaa Ngaire na Mumbi.