MAUDHUI YA NDOA KATIKA CHOZI LA HERI
Ndoa ni
makubaliano rasmi ya mwanaume na mwanamke kuishi pamoja kama mume na mke. Pia huitwa
chuo. Katika riwaya ya Chozi la Heri, maudhi
ya ndoa yanajitokeza baina wahusika mbalimbali. Ndoa hizi zinakumbwa na
changamoto tofauti tofuti huku zingine zikisambaratika na zingine zikiimarika. Mifano
ya ndoa riwayani ni kama yafuatayo:
Ndoa kati ya
Mwimo Msubili na wake zake kumi na
wawili akiwemo mamake Ridhaa. Ridhaa ni mmoja wa zao la ndoa hili.
Ndoa kati ya Ridhaa na Terry. Wanaozaliwa
kutokana na ndoa hii ni Mwangeka,
Annatila(Tila) Dede na Mukeli.
Ndoa kati ya
Mwangeka na Lily Nyamvula. Becky anazaliwa kutokana na ndoa hii lakini anaangamia
katika mkasa wa kuchomwa kwa jumba la Ridhaa. Lily pia anateketea katika mkasa
huo.
Ndoa kati ya
Racheal Apondi na Mandu. Wanamzaa Sophie. Mandu anaaga vitani anapoenda
kulinda Amani ughaibuni.
Ndoa kati ya
Mwangeka na Racheal Apondi baada ya
wawili hawa kufiwa na wenzao katika ndoa zao za kwanza. Wanamzaa Ridhaa.
Ndoa kati ya
Kaizari na Subira. Lime na Mwanaheri ni mazao ya ndoa hii.
Ndoa kati ya
kangata (mfanyikazi wa Kiriri) na Ndarine. Wanawazaa Lunga
Kiriri Kangata, Akelo Kiriri-Kaango na Lucia Kiriri Kangata.
Ndoa kati ya
Kiriri (tajiri aliyemwajiri Kangata) na Annet. Wanawazaa Songoa na
wengine walioenda kusomea na baadaye kufanya kazi ughaibuni.
Ndoa kati ya
Lunga na Naomi. Wanawazaa Umulkheri, Dick na Mwaliko.
Ndoa kati ya
Billy na Sally. Ndia hii inasambaratika kwa sababu Sally anasema kwamba
hawezi kuishi katika “nest” ambayo
ilijengwa na Billy. Anakataa na kurudi kwa ughaibuni.
Ndoa kati ya Neema na Mwangemi. Wawili hawa wanakosa kupata mtoto na hivyo wanaamua na
kumpanga Mwaliko.
Ndoa kati ya
Bwana Tenge na Bi. Kimai. Bwana Tenge si mwaminifu katika ndoa hii na hukigeuza
chumba chake danguro wakati Bi. Kimai ameenda nyumbani.
Ndoa kati ya
mamake Sauna na Bwana Kero. Wanamzaa Sauna.
Ndoa kati ya
Bwana Maya na mamake Sauna
Ndoa kati ya
Shamsi (Bwana Dengelua) na Bi. Halua ambaye ni mkewe.
Ndoa kati ya
Pete na Fungo.
Ndoa kati ya
Pete na Nyangumi.
POST A COMMENT DOWN THERE π
Soo helpful
ReplyDeleteVery helpful.
ReplyDeleteSo helpful
ReplyDeletenice
ReplyDeleteIt is very important and helpful
ReplyDeletePlz provide challenges this marriages faced
ReplyDeletethanks its helpful
ReplyDeleteVery helpful
ReplyDelete