WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
Katika
fasihi, mhusika ni kiumbe aliyefasiriwa au kubuniwa na mtunzi, anayemwiga na
kufanana na kiumbe halisi duniani kwa kiasi Fulani. Kuna aina mbalimbali za
wahusika kama vile:
a) Mhusika
mkuu
Huyu ni
mhusika ambaye anajitokeza katika hadithi kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko
wahusika wengine. Huweza kujitokeza kuanzia mwanzo hadi mwisho wa hadithi.
b) Wahusika
wadogo/ wasaidizi
Hawa ni
wahusika ambao hutangamana na mhusika mkuu na kumsaidia kuibua dhamira na
maudhui katika hadithi. Wahusika hawa hujitokeza kwa kiasi kidogo tu kwenya
hadithi na kisha kupotea.
Diwani ya Tumbo Lisiloshiba ina hadithi kumi na
tatu (13) na wahusika ni wafuatao.
TUMBO LISILOSHIBA-Said A. Mohamed
1.
Mzee Mago-Mhusika mkuu
2.
Mwene
3.
Kabwe
4.
Bi. Suruta
5.
Bi. Fambo
6.
Jitu
MAPENZI YA KIFAURONGO-Kenna Wasike
1.
Dennis- Mhusika mkuu
2.
Daktari Mabonga
3.
Penina (mpenzi wa Dennis)
4.
Shakila
5.
Wanafunzi chuoni
6.
Bwana Kitime- babake Penina
SHOGAKE DADA ANA NDEVU-Alifa Chokocho
1.
Safia -mhusika mkuu
2.
Bwana Masudi- babake Safia
3.
Bi. Hamida-mamake Safia
4.
Mkadi (Mtoto wa Habiba Chechei)
5.
Lulua (mnuna wake Safia)
6.
Kimwana (Shogake Safia)
SHIBE INATUMALIZA- Salma Omar Hamad
1.
Sasa
2.
Mbura –wahusika wakuu ni Sasa na
Mbura
3.
Mzee Mambo
4.
DJ
MAME BAKARI-Mohammed Khelef Ghassany
1.
Sara –mhusika mkuu
2.
Sarina- rafikiye Sara
3.
Beluwa- dadake Sarina
4.
Bi. Aluwiya- mamake Sara
5.
Babake Sara
6.
Mame Bakari- mtoto aliyezaliwa na
Sara
7.
Janadume
8.
Mwalimu Mkuu