BLOG VISITORS

Sunday, May 24, 2020

WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA

WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA


Katika fasihi, mhusika ni kiumbe aliyefasiriwa au kubuniwa na mtunzi, anayemwiga na kufanana na kiumbe halisi duniani kwa kiasi Fulani. Kuna aina mbalimbali za wahusika kama vile:

a)    Mhusika mkuu

Huyu ni mhusika ambaye anajitokeza katika hadithi kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko wahusika wengine. Huweza kujitokeza kuanzia mwanzo hadi mwisho wa hadithi.

b)    Wahusika wadogo/ wasaidizi

Hawa ni wahusika ambao hutangamana na mhusika mkuu na kumsaidia kuibua dhamira na maudhui katika hadithi. Wahusika hawa hujitokeza kwa kiasi kidogo tu kwenya hadithi na kisha kupotea.

Diwani ya Tumbo Lisiloshiba ina hadithi kumi na tatu (13) na wahusika ni wafuatao.

TUMBO LISILOSHIBA-Said A. Mohamed

1.     Mzee Mago-Mhusika mkuu
2.     Mwene
3.     Kabwe
4.     Bi. Suruta
5.     Bi. Fambo
6.     Jitu

MAPENZI YA KIFAURONGO-Kenna Wasike
1.     Dennis- Mhusika mkuu
2.     Daktari Mabonga
3.     Penina (mpenzi wa Dennis)
4.     Shakila
5.     Wanafunzi chuoni
6.     Bwana Kitime- babake Penina

SHOGAKE DADA ANA NDEVU-Alifa Chokocho
1.     Safia -mhusika mkuu
2.     Bwana Masudi- babake Safia
3.     Bi. Hamida-mamake Safia
4.     Mkadi (Mtoto wa Habiba Chechei)
5.     Lulua (mnuna wake Safia)
6.     Kimwana (Shogake Safia)

SHIBE INATUMALIZA- Salma Omar Hamad
1.     Sasa
2.     Mbura –wahusika wakuu ni Sasa na Mbura
3.     Mzee Mambo
4.     DJ

MAME BAKARI-Mohammed Khelef Ghassany
1.     Sara –mhusika mkuu
2.     Sarina- rafikiye Sara
3.     Beluwa- dadake Sarina
4.     Bi. Aluwiya- mamake Sara
5.     Babake Sara
6.     Mame Bakari- mtoto aliyezaliwa na Sara
7.     Janadume
8.     Mwalimu Mkuu

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...