BLOG VISITORS

Tuesday, June 30, 2020

PANUA BONGO NA FASIHI




 1.   LAZIMA
       “Asante ya punda kweli ni mateke. Sikujua ungekuja kunihangaisha ...”
       a)    Weka dondoo hili katika muktadha wake.     (alama 4)
       b)    Onyesha jinsi msemewa anamwangaisha msemaji.    (alama 2)
       c)    Kwa kurejelea tamthilia nzima onyesha ukweli wa methali “Asante ya punda ni mateke.”       (alama 14)

 HADITHI FUPI
       Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
2.    “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
       a)    Eleza muktadha wa dondoo hili.     (alama 4)
       b)    Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.            (alama 4)
       c)    Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ?       (alama 6)
       d)    Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.       (alama 6)
3.    Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.    (alama 20)

  Kigogo
       Tibu swali la 2 au 3 
2. Tusiwaruhusu watu wachache waliojazwa kasumba….kuturejesha ….hatuwezi kukubali kutawaliwa
    kidhalimu tena.
              a.    Eleza muktadha wa dondoo hili.     
              b.    Kwa kumrejelea mzungumzaji wa maneno haya, bainisha unafiki katika kauli hii. (alama 16)
  3. Eleza jinsi mbinu ya taharuki ilivyotumika kufanikisha maudhui katika tamthilia ya kigogo.                               (ala 20)

HADITHI FUPI
              Eunice Kimaliro :  Mtihani wa Maisha.
4. “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
              a.   Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                       
              b.   Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.  (alama 6)
              c.   Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili. 

              Alfa Chokocho  :  Tulipokutana tena

5. a.   “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
       i)   Eleza muktadha wa dondoo hili.          
       ii)  Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii. 
    b. Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”   

2.  “ Do ! Do ! Simameni ! Simameni leo kutanyesha mawe! “
i)   Eleza muktadha wa dondoo hili.  
ii) Fafanua mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo    
iv) Dhihirisha kwa kuzingatia hoja sita jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika tamthilia ya  “ Kigogo.”      (alama 12)

3) Eleza kwa kutolea mifano mitano mitano jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu za :
     i) majazi                          
     ii)mbinu rejeshi                

SEHEMU C: HADITHI FUPI
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
4. i)  Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo : (alama 20) 
           a) Mapenzi ya Kifaurongo
           b) Shogake dada ana Ndevu
           c) Mwalimu   Mstaafu
           d) Mtihani wa maisha
          
5) ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’
i)  Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba                    (al 10)
ii)  Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.                       (al 10)   

    
6. Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe macho”.                                                
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.  
(b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.  
(c) Ushauri uliotolewa na msemaji baadaye kama njia mojawapo ya kuwa macho ni wa kidhalimu.  Fafanua.          (alama 4)
(d) Eleza namna unafiki wa msemaji na upumbavu wa mnenewa unavyodhihirika katika muktadha wa dondoo hili.(alama   
(e) Onesha jinsi ukweli wa kauli hii ulivyojitokeza baadaye katika tamthilia.    

3. Jadili migogoro inayojitokeza katika tamthilia ya kigogo, kisha utathmini namna ilivyosuluhishwa.    (alama 20)

       SEHEMU YA C:HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
Jibu swali la 4 au 5
4. “Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a)   Eleza muktadha wa dondoo hili      (alama 4)
(b)  Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.   (alama 4)
(c)   Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya  (alama 6)
(d)  Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita      (alama 6)
5.Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii.  Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.  (alama 20)
“ Mguu huu ni wako”
·       Eleza muktadha wa dondoo hili   (al. 4)
·       Ni tamathali gani ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. Eleza maana yake  (al.2)
·       Msemewa alipewa ahadi zipi   (al. 5)
·       Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji  (al. 9) 
5 Eleza mbinu ya
·       Majazi    (al.10)
·       Kinaya   (al.10)


6. TUMBO LISILOSHIBA
Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo lisiloshiba   (Diwani)

7 “Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimamia juu ya              ardhi hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili  (al. 4)
b Eleza sifa nne za msemaji   (al. 4)
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili (al. 2)
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina tumbo lisiloshiba (al. 10)
“Oooh bebi,  miaka yaenda mbio sana, nayo  sura yako inachujuka……”
a)   Weka dondoo hili  katika muktadha wake.  (alama 4)
b)   Mhusika anayehusishwa na wimbo  huu ana msimano gani wa kimapinduzi?( 8)
c)   Taja sifa zozote nane za muhusika huyu   (alama 8)
5.   Tamthilia ya ‘Kigogo’ ni kioo cha  uhalisia wa maisha ya jamii nyingi  za kiafrika.  Thibitisha.               (alama 20)

SEHEMU YA D:  HADITHI FUPI TUMBO LISILOSHIBA  NA HADITHI NYINGINEZO
Jibu swali la 6 au la 7
6.    “Rasta twambie bwana!”
a)   Weka dondo katika muktadha  (ala 4)
b)   Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi  katika dondoo hili  (ala 2)
c)   Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe?  ( 4)
d)   Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya hadithi hii. (alama10 )

7.  Jadili mashaka ya Mashaka  katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”  (alama 20
2.  “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni wake huwajui.”
(i)  Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
     (ii)    Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo, thibitisha ukweli wa dondoo           hili. (al.14)
(ii) Taja tamathali za usemi zilizotumika katika dondoo hili.  (al.2)
3.  Eleza mbinu alizotumia majoka kuendeleza uongozi wake.  (al.20)

HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA.
6.Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki.               (al.20)

Tumbo lililoshiba na Hadithi nyingine
      4.   "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
      a) Eleza muktadha wa dondoo hii.   (alama 4)
      b) Taja naufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.  (alama 4)
      c)Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima.  (alama 6)
      d)Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo.  (alama 6)
    
5. Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
      a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
      b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. (alama 10)
 c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo. (alama 6)

KIGOGO   Pauline Kea
“Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko.”
a)          Weka maneno haya katika muktadha wake.  (alama 4)
b)          Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili  (alama 2)
c)          Kando na kufungiwa soko, Wanasagmoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka  (alama 5)
d)          Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 9)

SEHEMU C:  HADITHI FUPI :TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...