BLOG VISITORS

Tuesday, June 30, 2020

PANUA BONGO NA FASIHI




 1.   LAZIMA
       “Asante ya punda kweli ni mateke. Sikujua ungekuja kunihangaisha ...”
       a)    Weka dondoo hili katika muktadha wake.     (alama 4)
       b)    Onyesha jinsi msemewa anamwangaisha msemaji.    (alama 2)
       c)    Kwa kurejelea tamthilia nzima onyesha ukweli wa methali “Asante ya punda ni mateke.”       (alama 14)

 HADITHI FUPI
       Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
2.    “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
       a)    Eleza muktadha wa dondoo hili.     (alama 4)
       b)    Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.            (alama 4)
       c)    Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ?       (alama 6)
       d)    Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.       (alama 6)
3.    Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.    (alama 20)

  Kigogo
       Tibu swali la 2 au 3 
2. Tusiwaruhusu watu wachache waliojazwa kasumba….kuturejesha ….hatuwezi kukubali kutawaliwa
    kidhalimu tena.
              a.    Eleza muktadha wa dondoo hili.     
              b.    Kwa kumrejelea mzungumzaji wa maneno haya, bainisha unafiki katika kauli hii. (alama 16)
  3. Eleza jinsi mbinu ya taharuki ilivyotumika kufanikisha maudhui katika tamthilia ya kigogo.                               (ala 20)

HADITHI FUPI
              Eunice Kimaliro :  Mtihani wa Maisha.
4. “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
              a.   Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                       
              b.   Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.  (alama 6)
              c.   Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili. 

              Alfa Chokocho  :  Tulipokutana tena

5. a.   “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
       i)   Eleza muktadha wa dondoo hili.          
       ii)  Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii. 
    b. Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”   

2.  “ Do ! Do ! Simameni ! Simameni leo kutanyesha mawe! “
i)   Eleza muktadha wa dondoo hili.  
ii) Fafanua mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo    
iv) Dhihirisha kwa kuzingatia hoja sita jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika tamthilia ya  “ Kigogo.”      (alama 12)

3) Eleza kwa kutolea mifano mitano mitano jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu za :
     i) majazi                          
     ii)mbinu rejeshi                

SEHEMU C: HADITHI FUPI
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
4. i)  Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo : (alama 20) 
           a) Mapenzi ya Kifaurongo
           b) Shogake dada ana Ndevu
           c) Mwalimu   Mstaafu
           d) Mtihani wa maisha
          
5) ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’
i)  Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba                    (al 10)
ii)  Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.                       (al 10)   

    
6. Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe macho”.                                                
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.  
(b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.  
(c) Ushauri uliotolewa na msemaji baadaye kama njia mojawapo ya kuwa macho ni wa kidhalimu.  Fafanua.          (alama 4)
(d) Eleza namna unafiki wa msemaji na upumbavu wa mnenewa unavyodhihirika katika muktadha wa dondoo hili.(alama   
(e) Onesha jinsi ukweli wa kauli hii ulivyojitokeza baadaye katika tamthilia.    

3. Jadili migogoro inayojitokeza katika tamthilia ya kigogo, kisha utathmini namna ilivyosuluhishwa.    (alama 20)

       SEHEMU YA C:HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
Jibu swali la 4 au 5
4. “Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a)   Eleza muktadha wa dondoo hili      (alama 4)
(b)  Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.   (alama 4)
(c)   Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya  (alama 6)
(d)  Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita      (alama 6)
5.Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii.  Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.  (alama 20)
“ Mguu huu ni wako”
·       Eleza muktadha wa dondoo hili   (al. 4)
·       Ni tamathali gani ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. Eleza maana yake  (al.2)
·       Msemewa alipewa ahadi zipi   (al. 5)
·       Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji  (al. 9) 
5 Eleza mbinu ya
·       Majazi    (al.10)
·       Kinaya   (al.10)


6. TUMBO LISILOSHIBA
Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo lisiloshiba   (Diwani)

7 “Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimamia juu ya              ardhi hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili  (al. 4)
b Eleza sifa nne za msemaji   (al. 4)
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili (al. 2)
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina tumbo lisiloshiba (al. 10)
“Oooh bebi,  miaka yaenda mbio sana, nayo  sura yako inachujuka……”
a)   Weka dondoo hili  katika muktadha wake.  (alama 4)
b)   Mhusika anayehusishwa na wimbo  huu ana msimano gani wa kimapinduzi?( 8)
c)   Taja sifa zozote nane za muhusika huyu   (alama 8)
5.   Tamthilia ya ‘Kigogo’ ni kioo cha  uhalisia wa maisha ya jamii nyingi  za kiafrika.  Thibitisha.               (alama 20)

SEHEMU YA D:  HADITHI FUPI TUMBO LISILOSHIBA  NA HADITHI NYINGINEZO
Jibu swali la 6 au la 7
6.    “Rasta twambie bwana!”
a)   Weka dondo katika muktadha  (ala 4)
b)   Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi  katika dondoo hili  (ala 2)
c)   Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe?  ( 4)
d)   Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya hadithi hii. (alama10 )

7.  Jadili mashaka ya Mashaka  katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”  (alama 20
2.  “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni wake huwajui.”
(i)  Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
     (ii)    Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo, thibitisha ukweli wa dondoo           hili. (al.14)
(ii) Taja tamathali za usemi zilizotumika katika dondoo hili.  (al.2)
3.  Eleza mbinu alizotumia majoka kuendeleza uongozi wake.  (al.20)

HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA.
6.Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki.               (al.20)

Tumbo lililoshiba na Hadithi nyingine
      4.   "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
      a) Eleza muktadha wa dondoo hii.   (alama 4)
      b) Taja naufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.  (alama 4)
      c)Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima.  (alama 6)
      d)Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo.  (alama 6)
    
5. Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
      a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
      b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. (alama 10)
 c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo. (alama 6)

KIGOGO   Pauline Kea
“Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko.”
a)          Weka maneno haya katika muktadha wake.  (alama 4)
b)          Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili  (alama 2)
c)          Kando na kufungiwa soko, Wanasagmoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka  (alama 5)
d)          Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 9)

SEHEMU C:  HADITHI FUPI :TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

2.      “hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?
a)     Weka dondoo hili katika muktadha wake.  (alama 4)
b)     Tambua mbinu tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili na umuhimu wake (alama 6)
c)     Onyesha jinsi dhana ya nzi kufia kidondani inabainika hadithini  (alama  4)
d)     Hali ya kutowajibika inajitokeza vipi katika hadithi? (alama 6)
3.      Huku ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana katika jamii  (alama 20)

SHIBE INATUMALIZA - Salma Omar Hamad.
1. Lazima. (alama 20)
          “Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”
    (a) Eleza mukadha wa dondoo hili.  (alama 4)
     (b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.  (alama 2)
     (c) Eleza umuhimu wa mnenaji. (alama 4)
     (d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza”  Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii.  (alama 10)

TAMTHILIA
       Pauline Kea: Kigogo
4. “Shika hamsini zako wewe ... Hatutaki kufanya nira na mtu ...”
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.  (alama 4)
    (b) Eleza tamathali ya usemi iliyotumika. (alama 2)
    (c) Uongozi wa Majoka umesheheni sumu ya nyoka.
         Thibitisha kwa kudokeza hoja kumi na nne. (alama 14)
5.Utawala mbaya ni tatizo sugu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika.
  Jadili, kwa kurejelea matukio ishirini katika tamthilia ya Kigogo. (alama 20)

PAULINE KEA: KIGOGO
Jibu swali la 4 au la 5.
4. “Ukitaka kukula asali kaa na nyuki!”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. [alama 4]
b) Bainisha mbinu iliyotumika katika dondoo hili.  [alama 2]
c) Eleza jinsi wahusika hawa walivyofaidika kutokana na kukaa na nyuki. [alama 14]
i) Chopi
ii) Kenga
iii) Ngurumo
iv) Mamapima
                       
5. Eleza jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya majazi.  [alama 20]

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI:Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
6. Eleza sifa za wahusika wafuatao.  [alama 20]
i) Mwalimu Musi
ii) Jairo
iii)  Sera
iv) Mke wa Jairo

7. “ Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili  [alama 4]
b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili.    [alama 8]
c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii.   [alama 8]

KIGOGO na Timothy A . Rege
1.    “………..Acha porojo  zako . Kigogoo hachezewii watafuta maangamimi!”
a)Eleza muktadha wa dondoo hili ( alama 4)
b)Fafanua sifa za muzungumzaji ( alama 4)
c)El;eza jinsi msemewa alivyokuwa akimchezea kigogo katika muktadha huu.(2)
Kwa kurejelea hoja kumi kutoka kwenye  tamthilia  Onyesha ukweli kuwa ‘Kogogo  hachezewi
2.   Kwa kirejelea tamthilia ya kigogo , jadili  mbinu  - ishi  tunazojifunza kutokana na kijana Tunu . ( alama 20)

3. HADITHI FUPI
Tumbo lisilishiba na hadithi nyingine.

Shogake Dada ana Ndevu.
“Hapana cha ala, bwana. Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo  mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu .  Mtungi  wenyewe ni  mimi ……”
a)   Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)
b)   Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili ( alama 2
c)   Fafanua sifa moja u a msemaji inayodokezwa na dondoo hili  ( alama 2)
d)   Msemaji  wa mabo  haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtundini. Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi.       ( alama 4)
e)   Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojotokeza katika hadithi ya shogaka Dada ab Ndevu .                                             ( alma 8
4.   Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi  ya kifaurongo 
b) Shagake dada ana ndevu .
c) Mamake Bakari .
d) Mwalimu  mstaafu .
e) Mtihani  wa maisha .

TAMTHLIA -  KIGOGO – PAULINE KEA
Jibu swali la 2 au la 3
2. “ Mimi ni mtu wa vitendo, si wa vishindo.”
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.                                                                                                            (al. 4)
(b) Kwa kurejelea dondoo eleza sifa mbili za mnenaji                                                                                             (al. 4)
(c) Thibitisha ukweli wa kauli ya mnenaji.                                                                                                               (al. 12)
3.  Ukiukaji haki na uvunjaji sheria ni mambo yaliyokithiri katika jimbo la Sagamoyo. Thibitisha.  (al. 20)

SEHEMU IV:  HADITHI FUPI;
Tumbo  Lisiloshiba na hadithi Nyingine.
6. Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba  na ya  Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka.      (al. 20)
Pauline Kea: Kigogo
4. Uongozi mbaya ni tatizo sugu linalokumba mataifa mengi ya Afrika. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo.  (Alama 20)
5. ``Haja zako ni haja zangu, shida zako ni shida zangu, kiu yangu ni kiu yako.``
      a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (Alama 4)
b) Kwa kurejelea dondoo taja na ueleze sifa nne za msemaji na msemewa.(AL8)
     c) Taja tamathali ya usemi inayojitokeza katika dondoo  (Alama 2)
    d) Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo eleza jinsi mbinu zifuatazo zimejitokeza ( 6)
         i) Nyimbo
        ii) Jazanda
        iii) Majazi

SEHEMU D: HADITHI FUPI
  
6. a) Anwani  ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua  (ALama 10)
  b) Fafanua sifa kumi za mzee Mago (Alama 10)
7. Huku ukirejelea  hadithi za:
    i) Mapenzi ya kifaurongo
   ii) Shogake dada ana ndevu
   iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa.  (Alama 20)

TAMTHILIA (Kigogo)
2. Eleza jinsi mbinu zifuatazo zilivyotumika katika Tamthlia hii. (alama 20)
a)   Kinaya 
b)   Majazi
3.  Ami ? Tangu lini ukawa ami yangu?
a) Eleza muktadha wa dondoo  (Alama 4)
b) Taja  mbinu iliyotumika katika dondoo hili   (AIama 2)
c) Eleza sifa za msemaji    (AI 8)
d) Bainisha maudhui ya nafasi ya mwanamke ukizingatia mhusika huyu  (AIama 8)

SEHEMU YA TANO: HADITHI FUPI
8..Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka. (Alama 20)

8.    Huacha shughuli zote za pale zifanywe na ndugu yake.... Yeye mno hupiga mbio huku na kule, kujaribu hili na lile
a. Fafanua muktadha wa dondoo hili (al.4)
b. Eleza shughuli zilizomfanya mrejelewa kumwachia nduguye shughuli za pale.  (al.2)
c. Huku ukitoa mifano mwafaka kutoka hadithini eleza sifa bainifu za mrejelewa. (al. 14)

SEHEMU C: TAMTHILIA KIGOGO
4.    Kwa kurejelea mifano mbalimbali thibitisha dai kuwamwandishi huyu amemlika uhalisia wa   jamiiya Kenya  (al. 20)
5.    Ona sasa! Mnaniharibia biashara. Nimewapa dakika moja muione nyumba hii paa. Nikiwapatahapa, mtajua kwa nini wananiita
a.  Fafanua muktadha wa dondoo hili.  (al. 4)
b. Tambua kwa kutolea mfano mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika muktadha huu (al.2)
c. Kwa kurejelea mifano mbalimbali eleza madhara/matokeo ya shughuli za msemaji katika dondoo hili kwa jamii husika.

HADITHI FUPI- TUMBO LISILOSHIBA

1.      “Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a)     Eleza muktadha wa dondoo hili   (alama 4)
b)     Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili  (alama2)
c)     Fafanua sifa za msemaji   (alama 4)
d)     Jadili maudhui ya utabaka ukjirejelea hadithi husika. (alama 10)
2.      a)    Mhini na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya mkubwa  (alama10)
       b)    thibitisha kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa  (alama10)

SEHEMU YA D. KIGOGO
3.      a)    Utawala wa sagamoyo unatumia mbinu nyingi kubakia mamlakani. Fafanua zozote kumi (ala 10)
       b)    Mwanamke ni nguzo imara katika ujenzi wa jamii. Eleza kauli hii ukirejelea tamthilia ya kigogo (ala 10)
          
4.      “ Tuacheni kufumbatia maji kama jiwe. Sagamoyo inahitaji mabadiliko ,damu nyepesi ili kuufungua ukurasa mpya”
a)     Eleza muktadha wa dondoo hili (ala 4)
b)     Kwa kutoa mifano taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili   (ala4)
c)     Kwa nini sagamoyo inahitaji mabadiliko?  (ala 10)
d)      Taja sifa moja ya msemaji inayojitokeza katika dondoo hili  (ala2)
 “Unayazika matumizi yetu .Unaifukia kesho yetu.”
       a.    Eleza muktadha wa dondoo hili.
       b.    Onyesha jinsi anayeambiwa maneno haya anavyoifukia kesho ya wenzake
3.    ”Msiba wa kujidunga hauna kilio.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea ya Kigogo  (alama 20)

4.    HADITHI FUPI
       “Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”
       a.    Eleza muktadha wa dondoo hili
       b.    Tathmini umuhimu wa mzungumzaji
       c.    “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
5.  Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.’                                                                                                                             
Kigogo; Pauline Keya
Ndege ruka, ndege ruka, na barua mkononi,
Kifika kamwambie kimbuga usiku mchana,
Kila uchao twasema heri yaliyopita jana
Hata nami sasa naja mbuga nami nachama
Hapa hapataniweka najua tutaonana

4.    (a)   Weka dondoo hili katika muktadha wake ( alama 4)
       (b)  Eleza aina ya urudiaji inayojitokeza katika dondooo ( alama 2)
       (c)   Eleza sifa na umuhimu wa mhusika anayesema maneno haya ( alama 4)
       (d) Fafanua maudhui yanayojitokeza katika dondoo ( alama 2)
       (e)   Taja na ueleze matumizi mengine manne ya mbinu hii katika tamthilia ukifafanua ujumbe unaowasilishwa ( alama 8)

5.    Amenifukuza, anataka mkufu wangu wa dhahabu, nimeuficha.
       (a)   Fafanua muktadha wa dondoo hili ( alama 4)
       (b) Eleza mbinu ya sanaa inayojitokeza katika dondoo ( alama 1)
       (c)   Eleza maudhui yanayojitokeza katika muktadha                                     (alama 2)
       (d) Jadili sifa zozote sita za mnenaji wa maneno haya                                  (alama 6)
       (e)   Toa matumizi mengine ya mbinu hii na ueleze ujumbe uliomo  (alama 4)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
Tumbo lisiloshiba na hadithi zingine
       6.    ……… “ Mimi naweza kumtoa mtu chango sasa hivi! Usituangalie bwana. Kwani tunakula kwa babako?”
       (a)   Kwa nini msemaji anaongea hivi?  (alama 2)
       (b) Anayeambiwa ni nani? Alikuwa anaenda wapi?                                      (alama 2)
       (c)   Anayezungumza ni kielelezo cha watu  walioathirika katika jamii kwa kurejelea hadithi nzima. Onyesha vile mwandishi
              amesawiri athari hiyo   (alama 10)
       (d) Eleza sifa za anayeambiwa  (alama 4)
       (e)   Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo.      (alama 2)

7.    Said.A.Mohammed (Tumbo lisiloshiba) na Salma Omar Hamad ( Shibe inatumaliza) walidhamiria kuonyesha uozo katika jamii za kiafrika. Thibitisha (alama 20)

KIGOGO                                                                                                                        
4. "Mataifa mengi ya Afrika yamekumbwa na tatizo la uongozi mbaya."  Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (al 20)

HADITHI FUPI (ALAMA 20)
Jadili ufaafu wa anwani TUMBO LISILOSHIBA kwenye hadithi hii.  (Alama 20)
1.               Utawala wa majoka katika jimbo la sagamoyo umejaa sumu ya nyoka’’. Jadili usemi huu  kwa hoja kuntu. (Alama 20)
2 ‟Wamenimaliza… Wamenigeuka…″.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.   (Alama 4)
b)  Eleza namna msemaji amemalizwa na kugeukwa?  (Alama 4)
c)  Eleza umuhimu wa msemaji.  (Alama 4)
d) Eleza jinsi wahusika wengine walivyomaliziwa katika tamthilia. ( Alama 8)
SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
Tumbo lisiloshiba
3.    (a) Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa  Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba  (alama 10)
      (b)Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo  (alama 10)
7.  Aliyeumwa na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka  (alama 4)
a) Weka dondoo hili katika muktadha
b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka   (alama 6)
c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu? (alama 10)

KIGOGO
1.  Hivi vishahada vyao wanavyovipata siku hizi vinawavimbisha kichwa! Mtu anaitwa daktari na hata kazi ya maana hana....
a.      Weka dondoo hili hili katika muktadha wake   (Alama 4)
b.      Fafanua mbinu mbili za sanaa alizozitumia mwandishi   (Alama 4)
c.      Ukirejelea tamthilia ya Kigogo, dhihirisha kuwa mtu anaitwa daktari na hata kazi ya maana hana. 
                           
HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
Jibu swali la 4 au 5
2.      “Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...”
a.      Eleza muktadha wa dondoo hili      (Alama 4)
b.      Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili (Alama 2)
c.      Fafanua kile kilichokuwa kikitokea  (Alama 2)
d.      Eleza juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke  (Alama 12)

3.       
a.      Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii   (Alama 10)
b.      Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya kisasa  (Alama 10)

BONYEZA HAPA KUWASILIANA NAMI KATIKA WHATSAPP. 

BONYEZA KISWAHILI ILI KUPATA MAKALA MENGINE YA KISWAHILI

CLICK HISTORY TO READ MORE MATERIALS ON HISTORY

POST YOUR COMMENT DOWN THERE πŸ‘‡

No comments:

Post a Comment

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...