CHANGAMOTO ZINAZOKUMBA VIJANA
ü Magonjwa sugu (ukimwi)
ü Dawa za kulevya
ü Ukosefu wa ajira
ü Umaskini uliokithiri
ü Uigaji wa tamaduni za kigeni
ü Athari za utandawazi
ü uchumi kudoroa (Kustaafishwa mapema)
ü Kuibuka kwa lugha ya vijana
isiyoeleweka na wavyele wao, basi kukosa maongozi bora.
ü Shinikizo la hirimu (marika)
ü Ujana (Ushababi)
Taja zozote 5 (changamoto na
pendekezo la kusuluhisha)
DHULUMA DHIDI YA WANAUME
ü Kupigwa
ü Kufanyizwa kazi nzito za kinyumbani.
ü Kutusiwa/kukashifiwa.
ü Kunyimwa haki za ndoa.
ü Kukejeliwa (wakosapo ajira)
ü Kushurutishwa kutoa pesa zote.
ü Kunyimwa uhuru wa kutoa maoni.
ü Kunyimwa chakula (wafikapo nyumbani
kuchelewa/walevi)
HATUA ZINAZOPASWA KUCHUKULIWA ILI KUIMARISHA MATOKEO
YA MTIHANI SHULENI MWETU
Mwili uzingatie hoja zifuatazo.
ü Kuimarisha nidhamu
ü Kununua vifaa vya kimsingi k.v vitabu
ü Kuhimiza matumizi ya Kiswahili na
kiingerza shuleni
ü Kuhimiza matumizi yafaayo ya wakati
ü Kuhimiza vipindi vyote vya masomo
kuhudhuriwa.
ü Kununua makala ya kudurusu
ü Kuhimiza wazazi kuwajibikia majukumu
yao
ü Kuhimiza uwajibikaji wa walimu na wanafunzi
ü Kutoa nasaha na ushauri katika masomo
mbalimbali na umuhimu wa elimu kwa jumla.
ü Kuimarisha mahabara na maktaba
Mtahiniwa azingatie pande zote mbili hasara na faida kasha achukue msimamo
UTANDAWAZI UNA HASARA KULIKO FAIDA JADILI:
Hasara za utandawazi
ü Maovu
kuzagaa haraka kote
ü Miigo ya mambo yasiyofaa
ü Maadili kuzorota
ü Uhalifu kuongezeka
ü Matumizi mabaya ya mtandao
ü Wanafunzi kuchanganyikiwa
Faida za utandawazi
ü Kukuza maendeleo
ü Kubadilishana mawazo
ü Kuimarisha biashara za kimataifa
ü Kuimarisha elimu
ü Kuhimiza mataifa na uchunguzi
ü Kuimarisha teknolgia ya habari na
mawasiliano
ü Mtahiniwa azingatie hoja zilizo hapo
juu.
Hoja nyiongine zikadiriwe
ipasavyo
HOJA MUHIMU ZA TAWASIFU
ü Jina la mwandishi
ü Tarehe ya kuzaliwa
ü Mahali alipozaliwa
ü Wazazi wake
ü Motot wa ngapi katika uzawa wake
ü Jinsia yake
ü Alikosoma na wakait aliposima
ü Alichosemea na livyofaulu
ü Taaluma, kazi na tajriba
ü Uraibu wake
ü Uananchama wowote
ü Mafanikio yake maishani/tuzo na vyeit
alivyowahi kushinda
ü Pingamizi zozote alizowahi kukumbana
nazo maishani
ü Hali yake ya ndoa/familia
ü Warejelewa wake
ü Semina/makongamano ambayo amewahi
kuhudhuria
ü Majukumu au mchango wake katika jamii
ü Matarajio yake/azma yake/manifesto
yake katika wadhifa wake mpay wa Useneta
ü Anatetea nini zaidi katikak jamii
ü Falsafa/mtazamo wake katika jamii
kuhusu maswali mbalimbali
PENDEKEZA NJIA KADHAA ZINAZOWEZA KUTUMIWA KATIKA KUBUNI
NAFASI ZA KAZI HAPA NCHINI
ü Upanuzi wa viwanda
ü Kuimarisha uchmi wanachi ili pesa
zipatikane za kuwaajiri watu
ü Kuhimiza watu kujiajiri na serikali
ü Kupunguza mishahara mikubwa mikubwa
ili pes hizo zitumike kuajiri watu wengine
ü Uimarishaji wa sekta ya elimu ili
watu wapewe ujuzi mbalimbali
ü Masomo shulnie yalenge kufnza ubunifu
wa kiakzi
ü Serikali itoe ya kigeni yanayotaka
kufanya biashara nchini yawekewe sheira kuwa ni lazima yaajiri idaid Fulani ya
wenyeji ndipo yaruhusiwe kufanya biashara nchini
ü Kushiriki katika shughuli za jua kali
ü Wafanyikazi wa kgieni watozwe usuhur
ziaidi kwa mishahara yao ili kuwazuia kuja kuchukua nafasi za kikazi mabazo
zingekuwa za wenyeji
ü Sekta ya michezo iimarishwe
UHALIFU
Aina za uhalifu
ü Wizi wa kimabavu
ü Mapigano ya kikabila
ü Ugaidi
ü Ubakaji
ü Mauaji ya kikatili
ü Udanganyifu katika biashara (bidhaa gushi)
ü Ulanguzi wa dawa za kulevya
ü Ulanguzi wa binadamu
Njia za kukabiliana na uhalifu
ü Kuwasaka na kuwakamata wahalifu
ü Kuimarisha usalama nchini.
ü KuhimizaWananchi kuripoti visa vya uhalifu
au watu wanaowashuku kuwa wahalifu.
ü Tume ya ukaguzi na ukadiriaji wa ubora
kutekeleza wajibu wake.
ü Walinda usalama kupewa motisha.
ü Kufutwa kazi kwa maafisa wausalama wanaoshirikiana
na uhalifu.
MANUFAA YA UHIFADHI WA MAZINGIRA
ü Kuwepo kwa miti – ivutayo mvua
ü Itupayo chakula, dawa n.k.
ü Hutupa mbao za ujenzi.
ü Tabaka la ozoni likihifadhiwa
tutakingwa dhidi ya miale ya jua isababishayo kansa ya ngozi n.k.
ü Binadamu atakuwa na afya nzuri
kutokana na hewa safi yenye oksijeni.
ü Uhifadhi wa msitu utazuia maporomoko
ya ardhi yasababishayo vifo na uharibifu mkubwa.
ü Misitu pia itasaidia kuzuia gharika
iletayo maafa.
ü -Wanyama na mimea itakuwa bila
matatizo na yatokanayo na kemikali hatari na takataka nyingine.
ü Mito na maziwa yatakuwa na maji safi.
SABABU ZA KUTOFANYA VIZURI KATIKA MITIHANI YA KITAIFA
ü uhaba wa walimu
ü uchache wa madarasa
ü uhaba wa vitabu/vifaa
ü kutokamilisha silabasi kwa wakati ufaao
ü Msongamano wa wanafunzi
madarasani
ü Uzembe miongoni mwa
walimu
ü migomo shuleni
MADHARA YANAYOTOKANA NA UFISADI
ü Kuharibika kwa
miundo msingi kwa vile barabara
ü Ufisadi huwafanya watu kukosa kufanya kazi vizuri
ü Wananchi kukata
tama wakati jasho lao hafalidiwi
ü Viwanda kuporomoka
ü Ufisadi umewatajarisha matajiri huku maskini
wakidhulumiwa
ü Ufisad umesababisha ukosefu wa amani
ü Ufisadi umeendeleza ajali nyingi barabarani
ü Ufisadi umeendelea ajli nyingi bvarabarani
ü Ufisadi umesababisha ukosefu wa maadili katika jamii .
k,m uavyaji wa mimba
ü Elimu umeadhirika kutokana na maafisa wafsadi
TAJA MAMBO
YANAYOCHANGIA VITA VYA UKABILA
Sababu
ü Siasa
– vyama vya siasa
ü uchochezi
kutoka kwa viongozi
ü Chuki
na uhasama baina ya makabila
ü Umaskini
ü Ukosefu
wa ajira
ü Vikundi
haramu vya vijana k.m mungiki, sungusungu MRC nk
ü Ugaidi
ü Dhuluma
za kihistoria
Mapendekezo
ü Wachochezi
kuchukuliwa hatua za kisheria
ü Wananchi
kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani
ü Serikali
na washikadau kushirikiana ili kukabili tatizo la umaskini
ü Kubuni
nafasi za ajira kwa vijana
ü Serikali
kukabili vikundi haramu na ugaidi vilivyo
NAMNA KATIBA ILIVYOSHINDWA KUTIMIZA MALENGO YAKE KWA
WANANCHI
ü Imeongeza
gharama ya mishahara ya wabunge na wawakilishi hivyo kuacha mzigo kwa wananchi
ü Wananchi
wengi wamesalia katika maisha ya ukata licha ya mabadiliko ya kikatiba
ü Licha
ya katiba kubadilika viongozi walisalia wale wale wenye ufisadi, ukosefu wa utu,
katili kutojali n.k
ü Haikupendekeza
namna ya kutatua matatizo sugu yanayowakumba wanchi k.v ukosefu wa kazi
ü Serikali
imetumia fedha nyingi kufanikisha utekelezaji wake badala ya kuunda miundo
misingi ya kuboresha maisha
ü Kuwepo
kwa viwango tofauti vya uongozi yaani serikali ya kitaifa na kimajimbo kumezorotesha kasi ya maendeleo
ü Katiba
haikupendekeza malipo / ajira ya wafanyakazi wa umma badala yake ikapendekeza
tume kupiga msasa mishahara hiyo
ü sheria mpya za usafiri - Michuki
ü Mf.mikanda ya usafiri
ü Vithibiti mwendo kutumika.
ü kusitishwa kwa safari za usiku
ü Idadi ya abiria kuzingatiwa
ü maafisa wa usalama barabarani kuwa
chonjo
ü magari mabovu kuondolewa barabarani
ü vyeti vya madereva kuchunguzwa upya
ü maafisa wa usalama barabarani
wanaochukua hongo kuchukuliwa hatua za kisheria.
JADILI FAIDA NA
HASARA ZA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
Faida
ü Uchukuzi
na mawasiliano ya haraka kama vile katika
ndege, magari moshi yatumiayo stima,mawasiliano ya meme, barua pepe,
kipepesi.n.k
ü Elimu
kupitia vyombo kama vile runinga, redio,magazeti n.k
ü Katika
kilimo kuna mbinu mpya kupitia kwa utafiti wa kisasa.
ü Katika
sekta ya afya, kuna uvumbuzi wa madawa ya kisasa n.k
Madhara
ü Uzembe
kwa kutumia vyombo vya kisasa, watu wengine hawawezi kujifanyia jambo lolote
mitambo inapokwama.
ü Uozo
wa kijamii hasa miongoni mwa vijana sababu ya tarakilishi zinazoonyesha mambo
yaliyo miiko katika baadhi ya jamii za kiafrika
ü Madhara
yanayoambatana na vyombo hivyo kama vile kuharibika macho kutokana na matumizi
ya tarakilishi.
ü Madhara
ya vyakula vilivyokuzwa kwa kemikali nyingi n.k.
ü Hata hivyo,yamkini faida ni nyingi kuliko madhara
kwa hivyo ni muhimu kutambuliwe njia za
kujikinga na madhara hayo.
JADILI FAIDA NA KASORO ZA LUGHA YA MATANGAZO YA
BIASHARA
Faida za matangazo ya biashara (kuunga)
ü Hutufahamisha ni bidhaa gani
zinazopatikana.
ü Hutueleza faida za bidhaa fulani.
ü Huzitaja sifa nzuri za bidhaa.
ü Hutumia lugha ya kushawishi.
ü Hurahusisha kazi ya mnunuzi kuchagua
bidhaa.
ü Hutuwezesha kulinganisha bidhaa za
aina mbalimbali.
ü Huwasaidia wasomaji /watazamaji
kuongeza ufahamu.
Kasoro za matangazo
ü Huwakanganya wasikilizaji /wanunuzi.
ü Hayasemi lolote kuhusu ubaya wa
bidhaa.
ü Lugha yenyewe hupotosha.Huathiri maisha
ya wanajamii kiafya au kitamanduni.
ü Hutumia chuku sana ambayo huweza
kuathiri watumiaji wa bidhaa fulani.
CHANGAMOTO ZA SERIKALI ZA UGATUZI
ü Ukosefu wa usawa katika ugawaji wa
fedha gatuzi mbalimbali
ü Kutoelewana kwa serikali kuu na
serikali ya jimbo/gatuzi
ü Kutoelewa kwa maana ya ugatuzi kwa
magavana
ü Kuingiliwa hasa siasa kwa mchakato wa
ugatuzi
ü Ukosefu wa mipango katika kutokeleza
ugatuzi
ü Ufisadi wa baadhi ya uongozi (
magavana)
ü Ukosefu wa uwezo wa kuttekeleza
majukumu ya serikali ya ugatuzi
ü Miundo msingi hafifu nchini
ü Wafanyikazi wa serikali kuu kukosa
imani kwa serikali za majimbo
ü Kudhoofika kwa uchumi wa serikali
ü Ukosefu wa wataalamu ( wana taaluma)
ü Kutowajibika kwa viongozi wa gatuzi
SABABU ZA UDANGANYIFU KATIKA MTIHANI NCHINI
Matokeo/yaliyopatikana
ü Maenedeleo ya teknolojia mfano rukono kurahisisha mawasiliano
ü Mtihani wa kitaifa kuwa ndio kigezo
cha maisha ya baaday
ü Ushawishi kutoka kwa wanafunzi na
walimu
ü Kuorodheshwa kwa shule bora/ sifa
nzuri kwa shule zinazofanya vizuri
ü Kigezo cha kupandishwa madaraka kwa
walimu
ü Kutotayarisha wanafunzi vizuri
ü Kutokamilishwa kwa mtaala wa masomo
kwa kuwa ni pana
ü Ushindani miongoni mwa wakuu (walimu)
wa shule mbali mbali
ü Uoga wa kutimuliwa kutoka shule
Fulani
ü Baraza la kufanya mitihani kutokuwa
na usalama wa kutosha
ü Tamaa kwa wafanyikazi wa baraza la
kufunza mtihani
Mapendekezo
ü Rukono kutoruhusiwa shuleni hasa
wakati wa mtihani kwa wanafunzi au watahiniwa na wasimamizi wa mtihani
ü Kutorodheshwa kwa shule pamoja na
wanafunzi bora
ü Kukamilisha silabasi kwa wakati ufaao
ü Kuweka usalama wa kutosha kwa mtihani
ü Hatua kali za kisheria kuchukuliwa
kwa watakaopatikana na kosa la wizi wa mtitihani
ü Mjia mbadala kutumika katika
kutathmini uwezo na sifa za uongozi kwa walimu
ü Kuwaandaa wanafunzi vizuri kabla hawajafanya
mtihani
ü Vigezo vingine kutumika katika uteuzi
wa viongozi au wafanyi kazi mbalimbali
MANUFAA YA ELIMU BILA MALIPO KATIKA SHULE ZA MSINGI NA
ZA UPILI.
Manufaa
ü Idadi ya wanafunzi shuleni
imeongezeka
ü Uliopaji na masali ya karo si mzigo
kwa wazazi na shuleni
ü Maktaba na mahabara nk zimeweza kuwa
na kai zimeongezeka kuwa na vifaa vya kutosha.
ü Nafasi za kazi zimeongezeka kwa shule
na taasisi za Elimu nchini.
ü Wafanyikazi wameweza kupata mishahara
yao kwa wakati ufaao
ü Dhuluma na ajira kwa watoto imepungua
kwa sababu hakuna kisingizio au kuna sheria kali inayowalinda watoto.
Madhara
ü Uhaba wa Elimu
ü Uhaba wa vifaa kwa shule kwa vile
serikali imekuwa na mzigo mzito
ü Kiwango cha Elimu kimeshuka
ü Wazazi huzembea na kuachia serikali
mzigo mzito wa gharama
ü Kucheleweshwa kwa malipo na serikali
na hivyo kusambaratisha shughuli za masomo shuleni
ü Malipo/pesa zinazotolewa ni kidogo
ukilinganisha na mahitaji au hali ya uchumi /maisha
VIJANA WANA UWEZO MKUBWA WA KUENDELEZA
NCHI ZAO KULIKO WAZEE-JADILI
Swali hili liwe na pande
mbili-kuunga na kupinga
Mtahiniwa mwishowe atoe
msimamo kutokana na sehemu aliyoipa hoja nyingi (nzito)
Upande unaounga matahiniwa usipungue haja sita
Kuunga
ü Vijana wana uwezo/nguvu za
kutosha,wakilinganishwa na wazee
ü Vijana wengi wana uwezo wa kuvumbua
mambo yatakoendeleza nchi
ü Wanaweza kukopa na kuiga mambo mapya
ambayo yatafanikisha maendeleo
ü Vijana wana uelewa wa teknolojia ya
saha
ü Vijana ni wengi kuwaliko wazee
ü Vijana ni wengi ni vijana hivyo basi
wana uwezo na nafsi ya kuendeleza nchi
ü Wanajechi wananchihuhitaji vijana
walio na nguvu
ü Katika michezo za aina mbalimbali
kuna vijana
ü Wengi wa vijana huwa na uvumbuzi na
mioyo ya kushiriki kwa biashara.
Kupinga
ü Vijana waaweza kupapia mambo Fulani
kutokana na nguvu/haraka waliyonayo katika maisha
ü Vijana wengi wana mapuuza hasa kwa
mashauri ya wazee hii ni changamoto kwa kuendeleza maendeleo
ü Katika kuiga/kukopa ,wanaweza kukopa
mambo ambayo huyawezi kutumika katika nchi yao
ü Vijana wengi hukimbilia sehemu ambazo
zimeendelea kwa sababu ya kutaka kazi rahisi
ü Wengi wa vijana huhofia kuwa
waanzilishi wa maendeleo
ü Vijana wengi uhamia nchi
zilizoendelea kwa madhumuni ya elimu na kukosa kurudi kwani wanavutiwa na
maendeleo na halo nzuri ya masiha kule nje
ü Aghalabu wazee ni wazalendo-hupenda
ncho zao kuwaliko vijana
UKIMBIZI NI SUALA KITAIFA NA KIMATAIFA AMBALO LINA ATHARI NCHINI KENYA.FAFANUA
ü Mfumo wa elimu kusambaratika
/wanafunzi kukatizwa masomo
ü Usalama wa wanajamii kusambaratika
ü Huduma za afya kudorora
ü Watoto kuachwa mayatima
ü Utengano wa kifamilia/ndoa nyingi
kuvunjika
ü Watu kuishi wakiwa wa woga
ü Njaa kuangezeka/uhaba wa chakula
ü Uharibifu mkubwa wa mali
ü Utegemezi wa misaada/mzigo kwa
serikali watu kuishi katika makazi mabaya/makambi /mahema
ü Upweke /ukiwa baada ya kuachwa na
jamaa na marafiki
ü Malazi mabaya/msongamano kambini
ü Ukosefu wa siri/faragha
ü Ubakaji /ulawiti
ü Uchumi wananchi kusambaratika
ü Athari z kisaikolojia
CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI VIRANJA NA MAPENDEKEZO
changamoto
ü Ukosefu wa motisha wa viranja
ü Ukosefu wa demokrasia wakati wa
uteuzi wa viranja
ü Viranja kuadhibiwa mbele ya wanafunzi
wengine
ü Mkabala usio mzuri baina ya viranja na walimu
ü Vitisho kutoka kwa wanafunzi shuleni
ü Viranja kuegemea wajibu wao na
kudidimia kimasomo
ü Viranja kuafikia uamuzi bila ya ushauri
kutoka kwa walimu kuhusu masuala fulani shuleni
ü Ukosefu wa umoja miongoni mwa viranja
Mapendekezo
ü Kubuni kamati inayoshughulikia
malalamishi ya wanafunzi
ü Kuwepo semina ya kila mara ya viranja
ü Walimu na washika dau wengine shuleni
kuwapa viranja motisha kwa kuwatuza waliowajibika
ü Kuzingatia sheria za wizara ya elimu
kuhusu uteuzi na uchaguzi wa viranja\
ü Adhadu kwa viranja kutekelezwa kwa
njia isiyo waaibisha
ü Wanafunzi kuruhusiwa kushiriki baraza
mara kwa kujadili matatizo yao na kutoa mapendekezo
ü Idara ya ushauri na uelekezaji
kuimarishwa shuleni ili kudumisha nidhanmu ya wanafunzi
MATUMIZI MABAYA YA
MALI YA UMMA KATIKA MAGATUZI MBALIMBALI NCHINI NA UPENDEKEZE NJIA ZA
KUKABILIANA NA TATIZO HILO
Majibu
ü Wawakilishi wa wodi kujilimbikizia marupurupu
ya kila aina.
ü Safari za nje ya gatuzi ambazo hazina
manufaa yoyote kwa gatuzi.
ü Ununuzi wa vifaa kwa bei ya juu kuliko
ilivyo kwenye masoko.
ü Ujenzi wa barabara na nyumba kwa gharama
ya juu kutokana na kuwepo kwa ulaghai wakati wa utoaji wa zabuni.
ü Matumizi mabaya ya magari ya umma Kwamfano
magavana kuwa na misafara mirefu ya magarinakuandaa karamu zamarakwamara.
ü Wanakandarasi kulipwa kiasi kikubwa
cha pesa kuliko inavyopaswa na kuendeleza miradi duni.
ü Huduma za afya kukumbwa na migogoro ya
mara kwa mara kwa sababu yahelazasektahiyokutumiwavibayakwingine.
ü Kuajiriwa kwa maafisa pasi na kuzingatia
taaluma yao ila ukabila na unasaba.
VIPINDI VYA SINEMA ZA KIMAGHARIBI KWENYE RUNINGA VINA
MADHARA MAKUBWA
ü Matumizi ya lugha ya matusi
ü Kuubomoa utamaduni wa Kiafrika na kuupendelea
ule wa kigeni.
ü Huhimiza mahusiano ya kimapenzi
yasiyofaa
ü Hutoa mafunzo hasi kwa vijana mfano ugomvi,
kulipakisasi, ujambazi n.k.
ü Hukuza uvivu – uraibu wa kuzitazama kila
wakati.
ü Hutisha/kutia hofu miongoni mwa watazamaji
wa umri wa chini.
ü Baadhi huwa na picha chafu kwa mfano watu
wakiwa uchi, picha za ngono n.k.
ü Sinema nyingine huhusu vita, ulevi,
dawa za kulevya na hivyo kueneza maadili yasiyofaa.
ü Huwa ghali kununua au hata kulipia ili
mtu azitazame.
ü Huwatia watu matumaini wasiyo yaafikia.
Kwa mfano, mtu kutamani kuhama nchi yake ili kwenda ng’ambo kuishi maisha ya starehe.
KUPATIKANA KWA MAFUTA NCHINI KENYA KUTACHANGIA KIWANGO
KIKUBWA KWAMAENDELEO YA NCHI. JADILI.
Kuunga
ü Ujenzi wa miundo msingi kama vile barabara,
mitandao ya simu, mabomba ya kusafisha mafuta,n.k. utafanyika ili kuziunganisha
sehemu za uzalishaji mafuta na sehemu nyingine za nchi.
ü Huduma za kijamii kama vile elimu,
afya, kazi n.k. zitaimarishwa katika sehemu za visiwa vya mafuta.
ü Wenyeji watapata kazi katika viwanda
vya mafuta na hivyo kuinua hali ya maisha.
ü Uchumi wa nchi utaweza kuimarika
kutokana na mapato ya mauzo ya mafuta
nje ya nchi.
ü Gharama ya maisha itakuwa chini
kutokana na bei ya chini ya mafuta. Hali ya maisha itaimarika.
ü Wananchi wataimarika katika nyanja ya
ujuzi katika masuala ya uzalishaji wa mafuta.
ü Biashara za aina mbalimbali
zitanawiri kutokana na kipato kitakachowawezesha watu kuwa na fedha za
kununulia bidhaa na huduma mbalimbali.
Kupinga
ü Uzalishaji mafuta utachangia uchafuzi
wa mazingira.
ü Migogoro itazuka kautokana na ugavi
wa mapato kutokana mapato ya mafuta kwa mfano kati ya serikali ya kitaifa na
ile ya gatuzi/kaunti.
ü Uwezekano wa aina mbalimbali za ajali
zinazotokana na mafuta na hivyo kusababisha maafa na hasara kubwa.
ü Migogoro baina ya jamii mbalimbali
kugombania mashamba kwa sababu ya kupatikana kwa mafuta ndani yake.
ü Uzalishaji wa vyakula utapungua kwa
sababu ya utegemezi wa mapato ya mafuta.
ü Mtahini ahakiki hoja za mtahiniwa na
akubali hoja zozote mwafaka.
UDANGANYIFU KATIKA MTIHANI WA KITAIFA NI TATIZO SUGU.
ANDIKA TAARIFA ITAKAYOSOMWA KWA REDIO KUHUSU SULUHISHO LA TATIZO HILI
Suluhisho
· Wanafunzi
walenge kupata alama kulingana na uwezo wao
· Wazazi
wawe na matarajia kulingana na uwezo wao.
· Mtazamo
wa jamii ubadilishwe
· Wanafunzi
na shule washindane (zishindane) kulingana na kiwango
· Mfumo
wa elimu ubadilishwe usiegemee sana kupita mtihani pia uangazie vipawa vya
wanafunzi
· Wasimamizi
wawe macho wakati wa kusimamia mtihani
· Hatua
kali kuchukuliwa kwa wale watakao juhusisha na udanganyifu (hoja zozote sita)
KATIBA MPYA ITABORESHA MAISHA YA WAKENYA. JADILI
Baadhi ya hoja za kuunga mkono
ü Kuzingatiwa na haki za binadamu
ü Ugavi wa rasilimali utafanywa kwa
uwazi
ü Uongozi mzuri na uajibikaji
ü Kuwepo kwa usawa
ü Ugatuzi utaleta maendeleo
ü Kushirikisha wakenya wote katika
maendeleo
ü Maswala ya vta baada ya ucahguzi
yatotuliwa
ü Idara ya mahakama kuwa kuwa
ü Umoja wa kitaifa
ü Utangamano
ü Utatilia maanani haki za jamii
haswa zile zinazohisi kutengwa
ü Utaimarisha democrasia
ü Utaimarisha kuhusisha wananchi katika
utawala
Baadhi ya hoja za kupinga
ü Ufisadi-ubadhirifu wa pesa
ü Kuvuruga baadhi ya tamaduni k.m nafasi ya mwanamke
ü Kuendeleza ukabila
ü Baadhi ya maeneo kubaki nyuma
kimaendeleo
ü Migogoro kati ya viongozi k.m
magavana na maseneta
ü Utata katika kuelewa, kutafsiri au kufasiri vifungu vya katiba mpya
ü Serikali kuu kutoachilia baadhi ya
vitengo vya utekelezaji wa katiba mpya
ü Matumizi mabaya ya mamlaka na
viongozi
ü Kuna baadhi ya vipengele vya katiba
mpya ambavyo havijatiwa baadhi ya masharti
ü Ushuru utakuwa mwingi kwa wananchi
wow
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteGood work
ReplyDelete