MBINU REJESHI KATIKA CHOZI LA HERI
Riwaya
hii imejengwa kwa kiasi kikubwa kupitia mbinu rejeshi au kisengerenyuma ambayo
inajitokeza katika mifano ifuatayo:
1.
Ridhaa
anakumbuka kupepesa kwa jicho lake la kulia, anguko aliloanguka sebuleni,
mavune yaliyouandama mwili wake na kuunyongonyeza kwa muda, jeshi la kunguru
lililotua juu yap aa la maktaba yake, milio ya bundi, kerengende, iliyomtia
kiwewe. (Uk.1)
2.
Ridhaa
anakumbuka mazungumzo kati yake na Terry
mkewe, Terry akimuuliza, “since when has man ever changed his
destiny?” (Uk.2)
3.
Ridhaa anakumbuka
maneno ya marehemu mamake akimwambia kuwa machozi ya mwanaume hayapaswi
kuonekana hata mbele ya majabali ya maisha. (UK.3)
4.
Ridhaa anakumbuka
kilio cha mkewe Terry akimwambia Mzee kedi kuwa asiwauwe kwa vile wao ni
majirani. (Uk.3)
5.
Ridhaa anakumbuka
jinsi mwanawe Mwangeka alivyozaliwa
katika chumba chake ambach kwa sasa kimeteketea.(Uk.4)
6.
Ridhaa anakumbuka
mjadala kati yake na mwanawe Tila kuhusu
mafanikio ya baada ya uhuru. (Uk.5)
7.
Mwandishi
kupitia mbinu rejeshi anatueleza jinsi Ridhaa alivyojipata natika Msitu wa
Heri, jinsi babake Mzee Mwimo Msubili alivyowahamisha
wake zake wawili wa mwisho kutoka Ukungu
hadi Ughaishu/Msitu wa Heri. Mamake
Ridhaa akiwa ni mmoja wao. (Uk.9)
8.
Ridhaa anakumbuka
maneno ya baba yake akimwambia jinsi umiliki wa kibinafsi wa ardhi
haukusisitizwa kabla ya miaka hamsini kama ilivyo sasa. (Uk.9)
9.
Ridhaa anakumbuka
jinsi wanafunzi wenzake walivyomtenga shuleni na kumuita “mfuata mvua” (Uk. 10)
10. Ridhaa anakumbuka kuwa Mzee
Kedi ndiye aliyemsaidia kupata shamba, kwamba mwanawe Kedi, Mhandisi Kombo ndiye aliyesimamia
ujenzi wa nyumba yake, kuwa dadake Kedi ndiye aliyemuuzia shamba na jinsi Terry na mkewe Kedi walivyokuwa kama
ndugu wa toka nitoke. (Uk11)