BLOG VISITORS

Monday, May 11, 2020

MBINU REJESHI: CHOZI LA HERI



MBINU REJESHI KATIKA CHOZI LA HERI

Riwaya hii imejengwa kwa kiasi kikubwa kupitia mbinu rejeshi au kisengerenyuma ambayo inajitokeza katika mifano ifuatayo:

1.     Ridhaa anakumbuka kupepesa kwa jicho lake la kulia, anguko aliloanguka sebuleni, mavune yaliyouandama mwili wake na kuunyongonyeza kwa muda, jeshi la kunguru lililotua juu yap aa la maktaba yake, milio ya bundi, kerengende, iliyomtia kiwewe. (Uk.1)

2.     Ridhaa anakumbuka mazungumzo kati yake na Terry mkewe, Terry akimuuliza, “since when has man ever changed his destiny?” (Uk.2)

3.     Ridhaa anakumbuka maneno ya marehemu mamake akimwambia kuwa machozi ya mwanaume hayapaswi kuonekana hata mbele ya majabali ya maisha. (UK.3)

4.     Ridhaa anakumbuka kilio cha mkewe Terry akimwambia Mzee kedi kuwa asiwauwe kwa vile wao ni majirani. (Uk.3)

5.     Ridhaa anakumbuka jinsi mwanawe Mwangeka alivyozaliwa katika chumba chake ambach kwa sasa kimeteketea.(Uk.4)

6.     Ridhaa anakumbuka mjadala kati yake na mwanawe Tila kuhusu mafanikio ya baada ya uhuru. (Uk.5)

7.     Mwandishi kupitia mbinu rejeshi anatueleza jinsi Ridhaa alivyojipata natika Msitu wa Heri, jinsi babake Mzee Mwimo Msubili alivyowahamisha wake zake wawili wa mwisho kutoka Ukungu hadi Ughaishu/Msitu wa Heri. Mamake Ridhaa akiwa ni mmoja wao. (Uk.9)

8.     Ridhaa anakumbuka maneno ya baba yake akimwambia jinsi umiliki wa kibinafsi wa ardhi haukusisitizwa kabla ya miaka hamsini kama ilivyo sasa. (Uk.9)

9.     Ridhaa anakumbuka jinsi wanafunzi wenzake walivyomtenga shuleni na kumuita “mfuata mvua” (Uk. 10)

10.  Ridhaa anakumbuka kuwa Mzee Kedi ndiye aliyemsaidia kupata shamba, kwamba mwanawe Kedi, Mhandisi Kombo ndiye aliyesimamia ujenzi wa nyumba yake, kuwa dadake Kedi ndiye aliyemuuzia shamba na jinsi Terry na mkewe Kedi walivyokuwa kama ndugu wa toka nitoke. (Uk11)


11.  Ridhaa anakumbuka taarifa kupitia runinga iliyotangazwa miaka minne iliyopita kuhusu majumba yake matatu yaliyobomolewa katika mtaa wa Tononokeni. (Uk.13) (53)

12.  Kaizari anakumbuka jinsi watu/Wahafidhina walivyoshikilia silaha kupigania uhuru wao baada ya kutawazwa kwa kiongozi(musumbi) mpya aliyekuwa mwanamke. (Uk.17)

13.  Tetei, mwanaharakati anakumbuka jinsi wanaume walivyotumikishwa katika enzi za kiistimari (Uk.17)

14.  Bi.Shali anakumbuka jinsi Mwekevu alivyojitosa ugani, akaomba kura, akastahimili matusi na mwishowe kuchaguliwa kuwa kiongozi. (Uk.18)

15.  Kaizari anakumbuka jinsi roho zisizo na hatia zilisalimu amri chini ya pambaja za risasi na mapigo ya rungu na vitoza machozi kutoka kwa askari. (Uk.20)

16.  Kaizari anakumbuka malalamishi kutoka kwa mja aliyevaa shati lilioandikwa Hitman mgongoni kabla ya kuteketeza magari. (Uk.21)

17.  Mja aliyevaa shati lilioandikwa Hitman mgongoni anakumbuka jinsi kila baada ya miaka mitano viongozi huwatumia katika kampeni zao na kishiriki katika njama za viongozi za kuiba kura.(Uk22)

18.  Kaizari anakumbuka jinsi askari wa Penda Usugu Ujute walivyowafyatulia risasi vifuani vijana waliokuwa wakiandamana na kuwaua. (Uk.24)

19.  Kaizari anakumbuka jinsi genge la wahuni lilivyomvamia kwake na kumkata mkewe Subira kwa sime na kuwabaka mabinti zake wawili, Lime na Mwanaheri.

20.  Kaizari anakumbuka safari yao kutoka nchi ya Wahafidhina kuelekea Msitu wa Mamba baada ya vita kuzuka baada ya Mwekevu kutawazwa kama Musumbi. (Uk.26/27)
21.  Ridhaa anakumbuka Selumealipokuja kwake akilia baada ya mume wake kumuoa msichana wa kikwao. (Uk.34)
22.  Akiwa katika uwanja wa ndege ya Rubia, Ridhaa anakumbuka jinsi kadhia(mkasa) ilivyompoka familia yake. (Uk. 35)
23.  Ridhaa akimngoja Mwangeka katika uwanja wa ndege ya Rubia anakumbuka mazungumzo kati yake na bintiye Annatila (Tila), Tila akimwambia kuhusu somo la fasihi alilofunzwa na Mwalimu Meli (Uk.38)
24.  Ridhaa anakumbuka wimbo ambao mama yake alizoea kumwimbia baba yake alipokuwa katika safari zake za kazi (Uk. 49)
25.  Kupitia mbinu rejeshi, Ridhaa anamwambia Mwangeka kuhusu kifo cha ami yake-Makaa aliyechomeka alipoenda kuwaokoa watu walioteketea walipoenda kuchota mafuta kutoka kwenye lori lililobingirika.
26.  Ridhaa anakumbuka kuwa siku ambayo familia yake ilichomeka, alikuwa ameitwa hospitalini kumfanyia upasuajimajeruhi mmoja. (Uk.56)
27.  Mwangeka anakumbuka jinsi babake alivyomchapa baada ya kumpata yeye na wenzake wakiigiza mazishi ya nduguye Dedan Kimathi (Dede) aliyefariki akiwa miaka sita.(Uk.60)
28.  Kupitia kisengerenyuma, mwandishi anatueleza jinsi Mwangeka alivyokutana na Lily Nyamvula mkewe wa kwanza-katika chuo kikuu. (Uk. 61)
29.  Mwandishi anatueleza kuwa Kiriri-mwajiri wa Kangata alikufa kutokana na kufilisika na kihoro alichoachiwa na mkewe Annet aliyehamia ughaibuni baada  ya kupata Green Card. (Uk.64)

30.  Kupitia kisengerenyuma, mwandishi anatueleza jinsu Lunga Kiriri Kangata alivyokuwa akitoa hotuba kuhusu uhifadhi wa mazingira akiwa shuleni.
  Kuna mifano zaidi mingi kutoka riwayani. 

POST A COMMENT DOWN THERE πŸ‘‡

25 comments:

  1. Heko kazi nzuri

    ReplyDelete
  2. kazi nzuri ya kuelimisha Asante

    ReplyDelete
  3. ⓚⓐⓩⓘ ⓜⓩⓤⓡⓘ

    ReplyDelete
  4. What of remaining chapter

    ReplyDelete
  5. Kazi nzuri.Mungu aibariki kazi ya mikono yako

    ReplyDelete

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...