KONSONANTI GHUNA NA SIGHUNA
KONSONANTI GHUNA
NA SIGHUNA
Ughuna
wa sauti, hasa konsonanti huchunguzwa kwa kuzingatia kigezo cha mtetemeko wa nyuzi sauti.
Mtetemeko wa nyuzi sauti
Kwa
kuangalia kigezo cha mtetemeko wa nyuzi sauti, tunapata aina mbili za
konsonanti.
I.
Sauti/
Konsonanti ghuna/nzito
II.
Sauti/
Konsonanti sighuna/ konsonanti hafifu.
Konsonanti ghuna ni sauti ambazo
zinapotamkwa huwa kuna mtatameko/
mtikisiko wa nyuzi sauti.
Mfano
wa sauti ghuna ni : /z/, /b/, /g/, /d/, /gh/, /ny/, /ng/, /j/, /v/, /w/, /dh/,
/y/, /n/, /m/.
Konsonanti
sighuna
ni sauti ambazo zinapotamkwa huwa hakuna
mtetemeko au mtikisiko wa nyuzi sauti.
Mfano wa sauti sighuna ni: /s/, /k/, /t/, /p/, /ch/, /f/, /l/, /h/, /th/.
TANBIHI:
Ni
muhimu kutambua kwamba sighuna na ghuna hujitokeza katika majozi ya sauti za
vitate.
Kwa
mfano;
Sighuna ghuna
/p/ /b/
/t/ /d/
/th/ /dh/
/ch/ /j/
/f/ /v/
/k/ /g/
/kh/ /gh/
/s/ /z/
-
/n/,
/ny/, /ng/, /m/
/h/ -
/r/, /l/
##MIFANO ZAIDI##
TANBIHI
ü Nazali ghuna
ya midomoni-/m/.
ü Nazali ghuna
ya ufizi-/n/
ü Nazali ghuna
ya kaakaa laini-/ng’/
ü Nazali ghuna
ya kaakaa gumu-/ny/
ü Kizuio
kwamiza ghuna-/j/
ü Kizuio
kwamiza sighuna-/ch/
ü Kipasuo
ghuna ya kaakaa laini-/g/
ü Kipasuo
sighuna ya kaakaa laini-/k/
ü Kikwamizo
ghuna ya midomo na meno-/v/
ü Kikwamizo
ghuna cha ufizi- /z/
ü Kikwamizo
sighuna cha midomo na meno-/f/.
ü Kikwamizo
sighuna cha ufizi- /s/
ü Kitambaza ghuna cha ufizi-/l/
ü Kikwamizo
sighuna cha koromeo-/h/
JIKUMBUSHE
VIGEZO VYA KUAINISHA IRABU NI:
- Mwinuko wa ulimi (chini, kati, juu)
- Mahali pa kutamkia (Mbele, kati au nyuma ya ulimi)
- Mkao wa midomo (Mtandazo au mviringo)
VIGEZO VYA KUAINISHA KONSONANTI NI:
- Mahali pa kutamkia
- Jinsi/ namna ya kutamka
- Mtetemeko wa nyuzi sauti
- Mkao wa glota/ mkondo hewa