MENU

SEARCH HERE/ TAFUTA HAPA

Tuesday, April 14, 2020

TAMTHILIA YA KIGOGO



MASWALI YA TAMTHILIA YA KIGOGO


1.     Kigogo hachezewi; watafuta maangamizi!”
(a)  Eleza muktadha wa dondoo hii. (al. 4)
(b) Jadili ufaafu wa jina Kigogo kwa mrejelewa (al. 16)

2.     Msichana mrembo kama wewe, ni kitu gani kinakufanya usiolewe?
Elimu unayo ya kutosha, hata nga’ambo umeenda ukarudi.
Ukionyesha majivuno kwa vijana, utazeeka ukiwa nyumbani kwenu.
Oooh bebi,  miaka yaenda mbio sana,, nayo sura yako ninachujuka.
a.      Eleza muktadha wa dondoo hii. (al.4)
b.     Eleza maswala muhimu yanayodokezwa na dondoo hii. (al.6)
c.      Tathmini umuhimu wa mbinu ya ishara klatika kujenga tamthilia ya Kigogo (al.10)

3.     Eleza jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya kinaya katika tamthilia ya Kigogo (al.20)

4.     Eleza ujumbe unaopatikana kwenye nyimbo zifuatazo; (al.20)
a.      Wimbo wa uzaledo unaoimbwaredioni mjumbe anapotangaza kuhusu maandalizi ya sherehe.
b.     Wimbo wa Mamapima
c.      Wimbo wa Daudi Kabaka anaoimbiwa Tunu.
5.     a. Nini umuhimu wa matumizi ya lugha ya kishairi katika tamthilia ya Kigogo? (al.6)
b. Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia lugha ya kishairi katika tam,thilia ya Kigogo. (al.14)

6.     bainisha tamathali za usemi zilizotumiwa katika kauli zifuatazo. (al.12)
i.       “mwimbaji ninga kwelikweli”
ii. “…asidiriki katu kuionja kuonja shubiri na tamu ya mapambano.”
iii. “…lakini huu wako wa kuishi milele suiwezi.”
iv. “…sitaki hawa makunguru wanidhuru.”
v. “…kitu cha aali cha tunu kama wewe.”
vi. “Sitaacha kula mkate kwa kuchelea kiungulia.”
7.     Bainisha mbinu za kimtindo zilizotumiwa katika kauli zifuatazo. (al.8)
a.      Viongozi wa usoni wa Sagamoyo. Hamjambo?
b.     “ kila kitu ni Tunu. Tunu, Tunu, Tunu.
c.      “…nayo haina maisha Sagamoyo.”
d.     “Jamani mimi, wa kulinganishwa Samsoni Myahudi…”
8.     ‘Nusura roho ianguke mwanangu. Wametutia woga mwingi sana. Tywaishi kwa hofu.’
a.      Eleza muktadha wa dondoo hii (al.4)
b.     Eleza uhusiano kati ya msemaji na msemewa wa kauli hii. (al.2)
c.      Bainisha imani zozote mbili  za kidini zinazojitokeza katika kauli za baadaye za mnenaji wa maneno haya. (al.4)
d.     Fafanua jinsi maidhui ya kuzorota kwa usalama yanavyodokezwa na dondoo hili na yanavyojitokeza katika tamthilia nzima. (al.10)

9.     ‘koma! Wajua ni hatia kuuza pombe haramu?
a.      Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b.     Aliyeambiwa maneno haya alitoa jibu gani? (al.2)
c.      Fafanua sifa zozote mbili za aliyeambiwa maneno haya (al.4)
d.     Msemaji ni kielelezo cha maadili katika jamii ya Sagamoyo. Fafanua. (al.10)

BOFYA HAPA KWA 'O' NA 'AMBA' REJESHI

MAUDHUI TAWALA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA

No comments:

Post a Comment