MAUDHUI YA MABADILIKO KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO
Madadiliko
mbalimbali yanafanyika katika jumuiya ya Sagamoyo na mengine yanafanywa na
wahusika mbalimbali. Baadhi ya mabadiliko ni kama yafuatayo:
Ashua ambaye amekuwa na Sudi katika ndoa ya mapenzi na Amani anabadilika na kusema kuwa
Sudi amemchosha na kumwomba talaka. (Uk.47)
Uwanja wa ikulu ya Majoka hujaa pomoni kufikia saa moja asubuhi kila wafanyapo
sherehe lakini leo hii siku ya kusherehekea uhuru inayosadifiana na siku ya
kuzaliwa kwa Majoka, watu hawajafika uwanjani humu. Ni saa nne lakini kuna watu
kumi tu. (Uk.86)
Kingi, mkuu wa polisi ambaye amekuwa akitimiza amri za
Majoka leo amebadilika na kukataa kutii Majoka anapomwamuru awapige risasi
waliohudhuria mkutano wa Tunu katika lango la soko. Baadaye anajiunga na
kikundi wanaouunga mkono Tunu (Uk.90)
Kenga, mshauri mkuu wa Majoka ambaye amekuwa akimsaidia
Majoka anamgeuka Majoka na kumwambia kuwa iwapo (Majoka) amekataa kushindwa, basi
yeye (Kingi) amekubali. (Uk91)
Mamapima/Asiya aliyepewa kibali cha kuuza pombe haramu kwa kumuunga
mkono serikali ya Majoka anabadilika na kumuunga mkono Tunu na kuwaomba Wanasagamoyo msamaha. (Uk.92)
Chopi na Mwango waliokuwa walinzi katika serikali ya Majoka wanamgeuka
na kumtoa jukwaani na kumpisha Tunu ili azungumze na Wanasagamoyo. (Uk.92)
Mzee Kenga anabadilika na kumwacha Majoka na kujiunga na umati wa Wanasagamoyo unaomuunga
mkono Tunu. (Uk.91)