BLOG VISITORS

Tuesday, April 14, 2020

TUMBO LISILOSHIBA


MASWALI YA HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA


1.     Kwa kutolea mifano mwafaka, eleza ufaafu wa anwani Tumbo lisiloshiba  katika hadithi ya Tumbo Lisiloshiba. (al.20)

2.     Uozo wa maadili katika jamii ya Afrika umekithiri. Huku ukirejelea hadithi ya Shibe inatumaliza,  thibitisha ukitolea mifano maridhawa. (al.20)


3.     Kwa kurejelea  hadithi ya  Mapenzi ya Kifaurongo, Mame Bakari, Shogake dada ana ndevu na Masharti ya kisasa,  eleza jinsi maudhui ya mapenzi yanavyosawiriwa na waandishi wa hadithi hizi. (al.20)

4.     Tama na ubinafsi wa viongozi huwaathiri watawalwa. Thibisisha kauli hii kwa kurejelea hadithizi fuatazo. (al.20)
a.     Tumbo lisiloshiba
b.     Shibe inatumaliza
c.      Mkubwa
5.     Elimu ni kivukio cha ufanisi maishani. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi hizi.
a.      Mapenzi ya Kifaurongo
b.     Masharti ya Kisasa
c.      Mwalimu mstaafu
6.     Sekta ya elimu inakumbwa na changamoto maridhawa. Ukirejelea hadithi zifuatazo, thibitisha. (al.20)
a.     Mapenzi ya kifaurongo
b.     Shogake dada ana ndevu
c.      Mame Bakari
d.     Mwalimu mstaafu
e.     Mtihani wa maisha.

7.     Huku ukirejelea hadithi zozote tatu katika diwani ya Tumbo Lisiloshioba na Hadithi nyingine, taja na ufafanue matatizo yanayokumba mataifa mengi barani Afrika. (al.20)

8.     Jadili maudhui katika hadithi ya Mwalimu mstaafu. (al.20)


9.     Onyesha jinsi mwandishi wa hadithi ya  ndoto ya Mashaka amefaulu katika matumizi ya mbinu hihi. (al.20)
a.      Chuku
b.     Tashihisi
c.      Tashbihi
d.     Majazi
10.  Thibitisha namna ufisadi, na dawa za kulevya zinavyojitokeza katika hadithi ya MKUBWA. (al.20)

11. Jadili maudhui ya uonngozi mbaya katika hadithi hizi. (al.20)
a.     Tumbo lisiloshiba
b.     Shibe inatumaliza
c.      Mkubwa.
12. Hebu skiza jo,! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?”
a.     Eleza muktadha wa dondoo hili (al.4)
b.     Ukitolea mifano mwafaka, eleza mbinu nne za lugha katika dondoo hili. (al.4)
c.      Thuibitisha ukweli wa kauli, “ nzi kufa kidondani” (al.4)
d.     Jadili maudhui ya mapuuza katika hadithi hii (al.6)

13. Kwa sababu mimi najuana na Bogoa mmoja ambaye anatoka kweni mate”
a.     Weka dondoo hili katika muktadha wake (al.4)
b.     Taja na ufafanue mbinu ya kifasihi katika dondoo hili. (al.2)
c.      Jadili sifa za wahusika wafuatao
Sebu
Bogoa
Bi. Sinai.
14. …Hawawezi, hawawezi kabisaa hawawezi!.
a.     Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b.     Huku ukitolea mifano, tambua mbinu za lugha katika dondoo hili. (al.2)
c.      Ni masaibu gani yanayowakumba warejelewa katika dondoo? (al.14)

15. Una nini? Umeshtuka mwanangu! Unaogopa? Unaogopa nini?
a.     Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b.     Eleza sifa za msemaji (al.4)

JIBU MASWALI YAFUATAYO.

1. Taja wahusika wote katika hadithi hii na jinsi wavavyohusiana. (Al. 3)

2. " Ameshakufa...Ameshakufa..."

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Al.4)

b. Taja na ueleze sifa tano za mrejelewa. (Al.5)

c. Eleza uozo unaodhihirishwa katika dondoo hili. (Al.2)



3. FAFANUA maudhui yoyote manne yanayodhihirika katika hadithi hii. (Al. 12)

BOFYA HAPA KWA KIGOGO
BONYEZA HAPA KWA FASIHI SIMULIZI
BONYEZA HAPA KWA CHOZI LA HERI

POST A COMMENT DOWN THERE πŸ‘‡

4 comments:

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...