BLOG VISITORS

Tuesday, May 12, 2020

MABADILIKO SAGAMOYO: KIGOGO

MAUDHUI YA MABADILIKO KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO


Madadiliko mbalimbali yanafanyika katika jumuiya ya Sagamoyo na mengine yanafanywa na wahusika mbalimbali. Baadhi ya mabadiliko ni kama yafuatayo:

Ashua ambaye amekuwa na Sudi katika ndoa ya mapenzi na Amani anabadilika na kusema kuwa Sudi amemchosha na kumwomba talaka. (Uk.47)

Uwanja wa ikulu ya Majoka hujaa pomoni kufikia saa moja asubuhi kila wafanyapo sherehe lakini leo hii siku ya kusherehekea uhuru inayosadifiana na siku ya kuzaliwa kwa Majoka, watu hawajafika uwanjani humu. Ni saa nne lakini kuna watu kumi tu. (Uk.86)

Kingi, mkuu wa polisi ambaye amekuwa akitimiza amri za Majoka leo amebadilika na kukataa kutii Majoka anapomwamuru awapige risasi waliohudhuria mkutano wa Tunu katika lango la soko. Baadaye anajiunga na kikundi wanaouunga mkono Tunu (Uk.90)

Kenga, mshauri mkuu wa Majoka ambaye amekuwa akimsaidia Majoka anamgeuka Majoka na kumwambia kuwa iwapo (Majoka) amekataa kushindwa, basi yeye (Kingi) amekubali. (Uk91)

Mamapima/Asiya aliyepewa kibali cha kuuza pombe haramu kwa kumuunga mkono serikali ya Majoka anabadilika na kumuunga mkono Tunu na kuwaomba Wanasagamoyo msamaha. (Uk.92)

Chopi na Mwango waliokuwa walinzi katika serikali ya Majoka wanamgeuka na kumtoa jukwaani na kumpisha Tunu ili azungumze na Wanasagamoyo. (Uk.92)

Mzee Kenga anabadilika na kumwacha Majoka na kujiunga na umati wa Wanasagamoyo unaomuunga mkono Tunu. (Uk.91)



MAUDHUI TAWALA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
POST A COMMENT DOWN THERE πŸ‘‡

No comments:

Post a Comment

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...