1. LAZIMA
“Asante ya punda kweli
ni mateke. Sikujua ungekuja kunihangaisha ...”
a) Weka
dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Onyesha
jinsi msemewa anamwangaisha msemaji. (alama 2)
c) Kwa
kurejelea tamthilia nzima onyesha ukweli wa methali “Asante ya punda ni
mateke.” (alama 14)
HADITHI FUPI
Tumbo lisiloshiba na
hadithi nyingine
2. “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu,
maskini na tajiri”
a) Eleza
muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Taja
na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo
hili. (alama
4)
c) Mambo
yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana
? (alama 6)
d) Taja
na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo
hili. (alama 6)
3. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani
ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi
katika malezi. (alama 20)
Kigogo
Tibu
swali la 2 au 3
2. Tusiwaruhusu watu
wachache waliojazwa kasumba….kuturejesha ….hatuwezi kukubali kutawaliwa
kidhalimu
tena.
a. Eleza
muktadha wa dondoo hili.
b. Kwa
kumrejelea mzungumzaji wa maneno haya, bainisha unafiki katika kauli hii. (alama
16)
3. Eleza jinsi
mbinu ya taharuki ilivyotumika kufanikisha maudhui katika tamthilia ya
kigogo. (ala
20)
HADITHI FUPI
Eunice Kimaliro : Mtihani wa
Maisha.
4. “…..ilmuradi mawazo
yanamwadhibu sasa”
a. Eleza
muktadha wa dondoo
hili.
b. Fafanua
sifa za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)
c. Onyesha
mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.
Alfa
Chokocho : Tulipokutana tena
5. a. “
Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza
muktadha wa dondoo hili.
ii) Tathmini
umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi
hii.
b.
Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto
ya Mashaka”
2. “
Do ! Do ! Simameni ! Simameni leo kutanyesha mawe! “
i) Eleza
muktadha wa dondoo hili.
ii) Fafanua mbinu
za lugha zilizotumika katika dondoo
iv) Dhihirisha kwa
kuzingatia hoja sita jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika tamthilia
ya “ Kigogo.” (alama 12)
3) Eleza kwa kutolea
mifano mitano mitano jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu za :
i)
majazi
ii)mbinu
rejeshi
SEHEMU C: HADITHI FUPI
Tumbo
Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
4. i) Sekta ya elimu ina changamoto
nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo : (alama 20)
a) Mapenzi ya Kifaurongo
b)
Shogake dada ana Ndevu
c)
Mwalimu Mstaafu
d)
Mtihani wa maisha
5) ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya
mwenye njaa… ‘’
i) Thibitisha ukweli wa kauli hii
kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo
Lisiloshiba (al
10)
ii) Jadili uhalisia wa hadithi ya
Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja
kumi. (al
10)
6. Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe
macho”.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo
hili.
(c) Ushauri uliotolewa na msemaji baadaye kama njia mojawapo
ya kuwa macho ni wa
kidhalimu. Fafanua. (alama
4)
(d) Eleza namna unafiki wa msemaji na upumbavu wa mnenewa
unavyodhihirika katika muktadha wa dondoo hili.(alama
(e) Onesha jinsi ukweli wa kauli hii ulivyojitokeza baadaye
katika tamthilia.
3. Jadili migogoro
inayojitokeza katika tamthilia ya kigogo, kisha utathmini namna
ilivyosuluhishwa. (alama 20)
SEHEMU
YA C:HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
Jibu swali la 4 au 5
4. “Kesho kama sote
tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo
hili (alama 4)
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika
dondoo hili. (alama 4)
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya (alama
6)
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka
katika bara la Afrika.
Taja mambo sita (alama 6)
5.Ukengeushi huzorotesha
maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya
‘Mkubwa’. (alama 20)
“ Mguu huu ni wako”
· Eleza
muktadha wa dondoo hili (al. 4)
· Ni
tamathali gani ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. Eleza maana yake (al.2)
· Msemewa
alipewa ahadi zipi (al. 5)
· Eleza
sifa na umuhimu wa mzungumzaji (al. 9)
5 Eleza mbinu ya
· Majazi
(al.10)
· Kinaya (al.10)
6. TUMBO
LISILOSHIBA
Kwa kuzingatia hadithi
zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo
lisiloshiba (Diwani)
7 “Kesho panapo
majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu
zinazosimamia juu ya ardhi
hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
b Eleza sifa nne za msemaji (al. 4)
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo
hili (al. 2)
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina
tumbo lisiloshiba (al. 10)
“Oooh bebi, miaka yaenda mbio sana,
nayo sura yako inachujuka……”
a) Weka
dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Mhusika
anayehusishwa na wimbo huu ana msimano gani wa kimapinduzi?( 8)
c) Taja
sifa zozote nane za muhusika huyu (alama 8)
5. Tamthilia
ya ‘Kigogo’ ni kioo cha uhalisia wa maisha ya jamii
nyingi za kiafrika. Thibitisha. (alama
20)
SEHEMU YA
D: HADITHI FUPI TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINEZO
Jibu swali la 6 au la 7
6. “Rasta
twambie bwana!”
a) Weka
dondo katika muktadha (ala 4)
b) Taja
mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (ala 2)
c) Ni
kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe? ( 4)
d) Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya
hadithi hii. (alama10 )
7. Jadili
mashaka ya Mashaka katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka” (alama
20
2. “Kitabu si jalada, fungua ndani usome
mambo. Kitanda
usichokilalia kunguni wake huwajui.”
(i) Eleza
muktadha wa dondoo hili. (al.4)
(ii) Kwa
kurejelea tamthilia ya kigogo, thibitisha ukweli wa
dondoo hili. (al.14)
(ii) Taja tamathali
za usemi zilizotumika katika dondoo hili. (al.2)
3. Eleza
mbinu alizotumia majoka kuendeleza uongozi wake. (al.20)
HADITHI FUPI: TUMBO
LISILOSHIBA.
6.Huku ukirejelea
hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji
wa
haki. (al.20)
Tumbo
lililoshiba na Hadithi nyingine
4. "Penzi lenu na nani? . . . .
Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo
hii. (alama 4)
b) Taja naufafanue mbinu mbili
za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
c)Onyesha vile maudhui ya
utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
d)Eleza sifa sita za
mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)
5. Ilikuwa kama vile katia
saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa
kitanzi.
a)Fafanua tamathali mbili
zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
b)Jadili vipengele vitano vya
sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. (alama 10)
c)Onyesha dhiki
iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo. (alama 6)
KIGOGO Pauline Kea
“Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza
majeraha yao ya kufungiwa soko.”
a) Weka
maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
b) Tambua
mbinu mbili za lugha katika dondoo hili (alama 2)
c) Kando
na kufungiwa soko, Wanasagmoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa
na utawala wa Majoka (alama 5)
d) Fafanua
sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 9)
SEHEMU C: HADITHI FUPI :TUMBO
LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE