UFAAFU WA ANWANI TUMBO LISILOSHIBA
Tumbo Lisiloshiba
ni anwani ya moja kati ya hadithi zilizotungwa na Said A. Mohamed. Hadithi hii inapatikana katika kitabu
cha hadithi fupi chenye jina Tumbo
Lisiloshiba na Hadithi Nyingine. Kitabu hiki kimehaririwa na Alifa Chokocho
na Dumu Kayanda.
Kichapishi changu hiki kinaegemea hadithi ya kwanza kwenye kitabu hiki ambayo ni Tumbo Lisiloshiba. Utafiti wangu
unachunguza ufaafu wa anwani hii katika hadithi hii. Je, anwani hii inaifaa
hadithi hii au la? Bila shaka hoja zifuatazo zinadhibitisha kuwa anwani hii
inaiafiki hadithi hii.
Viongozi
wamejenga majengo mengi mjini na kumaliza nafasi yote hadi hakuna nafasi ya
kuvuta pumzi.
Viongozi wana
majengo mengi mjini lakini bado wanahitaji ardhi zaidi ya kujengea majengo
mengine.
Kutotosheka kwa
matajiri kunawafanya kutaka kuwapokonya Wanamadongoporomoka ardhi zao bila
kujali kule ambako maskini hao wangeenda.
Viongozi wameweka
vikwazo vya kisheria ili raia wasiweze kuzitetea mali zao baada ya wao
kuwanyanganya.
Jitu lina
tumbo lisiloshiba kwa vile linaingia mkahawani na kula chakula chote
kilichokuwa kimepikwa.
Jitu hilo
pia linaagiza kuandaliwa chakula maradufu ambalo lingekuja kula mkahawani siku
ambayo ingefuata.
Kwasababu ya
kutotosheka kwa viongozi, wanawabomolea raia makazi yao wakiwa wamelala ili
waweze kuinyakua ardhi zao.
Tamaa ya
viongozi inawafanya kuwatumia askari wa baraza la jiji pamoja na jeshi la
polisi ili kuwasaidia kupata ardhi zaidi wakati tayari wana majengo mangi
mjini.
Wanasheria wamekosa
uaminifu kwa sababu ya tamaa ya pesa. Wanakosa kuwatatulia masikini sharia ngumu
zinazowakabili.
Viongozi wanataka
kuwalipa Wanamadongoporomoka fidia duni/ visenti vichache ili waondoke
Madongoporomoka na kuwaachia ardhi hiyo.
Kutokana na hoja hizi, niko radhi kutoa uamuzi kwamba anwani Tumbo Lisiloshiba inaiafiki hadithi hii. Wawezadondoa hoja zingine ambazo zinadhihirisha kwamba ni kweli anwani hii inaifaa hadithi hii.
GUSA HAPA KUPATA WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
GUSA HAPA KUPATA WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
Wow,,, help me a lot
ReplyDeleteufaafu
DeleteWa nini
DeleteKwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo na shogake dada and ndevu fafanua changamoto zinazowakumba vijana
ReplyDeleteTaja umuhimu au majukumu ya kila mhusika uliyemtaja
ReplyDeleteKwa uchambuzi zaidi, majibu ya maswali na makala mengine, subscribe channel yetu ye YoutTube hapa.
ReplyDeletehttps://www.youtube.com/channel/UC3EEBQNhW-y6VNg3JgpN76Q
Huku ukirejelea hadithi ya mame bakari eleza matatizo ya wanawake na nafasi zao
ReplyDeleteAnwani
ReplyDeleteAnwani
ReplyDeleteI need sifa ama umuhimu za wahusika
ReplyDeleteNafurahia this site really helpful to me
ReplyDeleteThank you for good guide
ReplyDelete