Soma
shairi lifuatalo kwa kina kisha ujibu maswali yanayofuata
1. Natunga nikiwaasa, msije kujijutia,
Mitego
sije wanasa, mkaja kuangamia
Tamaa
nyingi za pesa, gereza, zitawatia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza
2. Jela inamkonyeza, kama hutajizuwia
Haina ndugu gereza, jela si ya kuchezea,
Inajuvya
na kupoza, wenye nguvu kutulia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza
3. Rushwa si kitu chema, walaji
jihadharini,
Mkila
zitawakwama, zitawatoka puwani,
Wazilao
hulalama, si mimi ila Fulani
Kila
mpenda rushwa, jela inamkonyeza
4. Ridhika na upatacho, kama moja au mbili,
Usitaraji
mkocho, upatao, bwana Ali,
Tama
zako za macho, zitakulea mbuli
Kila
mpenda rushwa, jela inamkonyeza
5. Ni mema kemukemu, wenye vyeo kutumia
Maleba
wakiwahimu, rushwa kuwaletea,
Muogopeni
karimu, leba haombwi rushwa,
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza
6. Kuna wengi mahakimu, haki wanazopinduwa,
Yatima
huwa dhulumu, kwa kupapia rushwa
Kwa
kutaka darahimu, aso haki anapewa
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza
Maswali
(a)
Andika kichwa mwafaka cha shairi hili . (al.1)
(b) Taja madhara manne ya rushwa. (al.4)
(c) Eleza
umbo la shairi hili. (al.4)
(d) Andika
ubeti wanne katika lugha nathari. (al4)
(e)
Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika
shairi hili. (al.3)
(f)
Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa
katika shairi hili . (al.4)
(i)
Gereza
(ii)
Mkocho
(iii)
Karimu
(iv)
Darahimu