BLOG VISITORS

Thursday, April 30, 2020

UFAAFU WA ANWANI-CHOZI LA HERI

UFAAFU WA ANWANI-CHOZI LA HERI


Chozi ni matone ya maji yanayotoka kwenye jicho/macho ya mtu kutokana na maumivu au furaha. Heri ni hali ya kuwa salama au hali ya kupata jambo jema. Pia linamaanisha nafuu au afadhali. Maneno haya yakiunganishwa pamoja yanaleta maana ya chozi linalomtoka mtu wakati hali imakuwa salama au kupata jambo zuri. Au chozi analotoa mtu hali inapokuwa nafuu au afadhali kwake.

Hoja zifuatazo zinathibitisha ufaafu wa anwani hii ya Chozi la Heri.

1.     Familia ya mzee Mwimo Msubili inateseka kutokana na udogo wa ardhi lakini hali inakuwa nzuri babake Ridhaa anapowahamisha wake zake wawili wa mwisho, katika Msitu wa Heri. Mmoja wa hawa ni mamake Ridhaa.

2.     Ridhaa anadhulumiwa na wanafunzi wenzake shulenina kutukanwa kuwa yeye ni mfuata mvua lakini hali inakuwa nzuri baada yamamake kwenda na kuzungumza na mwalimu mkuu na hali nii kusitishwa.

3.     Eneo la Msitu wa Heri lilikuwa kame (Kalahari) lakini inageuka kuwa nzuri baada ya Ridhaa kuwaletea maji ya mabomba na eneo hilo kutwaa rangi ya kichani kiwiti.

4.     Hali inakiwa nsuri kwa Mzee Kedi Ridhaa anapoyathamini masomo ya wapwa zake wawili.

5.     Mwekevu anapoingia kwenye siasa anatusiwa na watu lakini hali hii inabadilika na kuwa bora baada ya kushinda uchaguzi.

6.     Familia ya Kaizari inapata taabu anapovamiwa na wahuni lakini anapata heri wakati jirani yake Tulia anapomsaidia kutorokea palipo salama.

7.     Kaizari anapovamiwa na mkewe Subira kujeruhiwa na wananwe Lime na Mwanaheri kubakwa, anapata heri Tulia anapojitolea kumlindia nyumba isije ikaharibiwa na wahuni.

8.     Wakimbizi wanapoteseka kambini kutokana na ukosefu wa chakula, misikiti na makanisa yana waletea chakula na kuwafanya kuona heri.

9.     Wakimbizi wanapoteseka kwa kulala vibandani, shirika la Makazi Bora linajitolea kuwajengea makao bora.

10.  Selume anapotaabika baada ya kukataliwa na mumewe Mwanzi, anakutana na Ridhaa anayemsaidia kupata kazi ya uuguzi katika hospitali ya umma.

11.  Kuchomwa kwa familia ya Ridhaa kunamletea ugojwa wa shinikizo la damu lakini anasaidiwa kudhibiti hali hiikutokana na huduma za ushauri na uelekezaji kutoka kwa wataalamu.

12.  Lime na Mwanaheri wanabakwa lakini wanapata heri abaada ya kutibiwa na wauguzi waliotumwa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

13.  Ridhaa anafuraha kupatana na mwanawe Mwangeka vita vya baada ya uchaguzi vilivyozuka na kusababisha wanawe wengine pamoja na mkewe Terry kuangamia.

14.  Usalama unazorota katika nchi ya Wahafidhina lakini wanapata heri jamii ya kimataifa inapowasaidia kurejesha Amani.

15.  Kiriri anamsaidia mfanyikazi wake Kangata kuyadhamini masomo ya binti zake wawili.

16.  Riziki Immaculata, kitoto kinachotupwa na mamake kwenye biwi la taka linapata heri kinapookolewa na Neema anayekipeleka katika kituo cha watoto cha Benefactor.

17.  Umulkeri amekuwa akilia kwa kukosa wazazi lakini hali inakuwa bora kwake Apondi na Mwangeka wanapomchukua na kuishi naye kama mwana wao wa kupanga.

18.  Chanda Chema anataabika kwa kukosa malezi lakini Bwana Tenge na Bi. Kimai wanamchukua na kumlea kama mwanao.

19.  Mwaliko anatekwa nyara na nyumbani kwa Bi.Kangara lakini anaokolewa na polisi na kupelekwa katika kituo cha Benefactor.

20.  Mwangeka anafiwa na mkewe Lily Nyamvula lakini anapata heri anapowoa Apondi.

21.  Apondi anafiwa na mumewe aliyeenda kudumisha amani  lakini anapata nafuu anapoolewa na Mwangeka.

22.  Hazina anataabika barabarani kama ombaomba lakini anapata heri Umu anapompa pesa.

23.  Umulkheri anapoteseka mjini anabahatika kumpata Hazina aliyempa pesa miaka mingi iliyopita. Hazina anamsaidia Umukheri.

24.  Dick anapata heri anapojinasua kutoka kwenye biashara ya kuuza dawa za kulevya na kuanza biashara yake ya kuuza vifaa vya elekroniki.

25.  Tuama anapoteza damu nyingi baada ya kupashwa tohara lakini anapata heri anapotibiwa na kupona.

26.  Neema anataabika kwa kukosa mtoto lakini hali yake inaimarika anapofaulu kupewa Mwaliko na Mtawa Anastacia kutoka kituo cha watoto cha Benefactor na kumlea kama mtoto wa kupanga.

SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...