BLOG VISITORS

Friday, July 17, 2020

USHAIRI KIKORONA

            

         Soma shairi lifuatalo kwa kina kisha ujibu maswali yanayofuata

1.         Natunga nikiwaasa, msije kujijutia,
Mitego sije wanasa, mkaja kuangamia
Tamaa nyingi za pesa, gereza, zitawatia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


2.         Jela inamkonyeza, kama hutajizuwia
Haina ndugu gereza, jela si ya kuchezea,
Inajuvya na kupoza, wenye nguvu kutulia
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


3.         Rushwa si kitu chema, walaji jihadharini,
Mkila zitawakwama, zitawatoka puwani,
Wazilao hulalama, si mimi ila Fulani
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


4.         Ridhika na upatacho, kama moja au mbili,
Usitaraji mkocho, upatao, bwana Ali,
Tama zako za macho, zitakulea mbuli
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza


5.         Ni mema kemukemu, wenye vyeo kutumia
Maleba wakiwahimu, rushwa kuwaletea,
Muogopeni karimu, leba haombwi rushwa,
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza

6.         Kuna wengi mahakimu, haki wanazopinduwa,
Yatima huwa dhulumu, kwa kupapia rushwa
Kwa kutaka darahimu, aso haki anapewa
Kila mpenda rushwa, jela inamkonyeza

Maswali
(a)   Andika kichwa mwafaka cha shairi hili .                                                                  (al.1)
(b)   Taja madhara manne ya rushwa.                                                                               (al.4)
(c)   Eleza  umbo la shairi hili.                                                                                          (al.4)
(d)  Andika ubeti wanne katika lugha nathari.                                                                 (al4)
(e)   Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika shairi hili.                      (al.3)

(f)   Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili .                        (al.4)
(i)              Gereza
(ii)            Mkocho
(iii)          Karimu
(iv)          Darahimu



SPECIAL FEATURE-PHOTOSYNTHESIS

  PHOTOSYNTHESIS AND WHY IT IS IMPORTANT Photosynthesis and Why it is Necessary Photosynthesis is a critical process that sustains plants ...