Samweli Matandiko baada ya kuanguka mtihani anaamua kujitoa uhai
kwa kujitupa kidimbwini ili afe.
Mamake Samweli anamwambia kuwa japo ameshindwa
na mtihani wa shule, hawezi kushindwa na mtihani wa maisha.
Samweli
anaporudi shuleni kuchukua matokeo yake, mawazoni anamwona mwalimu mkuu kama
hambe au zuzu.
Jamii inaamini
kuwa mtu akianguka mtihani wa shuleni basi hawezi kufaulu katika mtihani wa
maisha.
Elimu ya
shuleni inakadiriwa kama msingi wa maisha bora baada ya shuleni ndiposa
Samweli, dada zake na wanafunzi wengine shuleni wanahudhuria masomo.
Ni wajibu wa
wazazi kugharamia elimu ya watoto wao hadi wamalize elimu yao. Babake Samweli
anafadhili masomo ya binti zake na mwanawe Samweli.
Samweli anamaliza
mtihani wa shule na anapopokea matokeo mabaya, anatamauka na kujitumbukiza
majini ili afe.
Mtihani wa
shule ulimshinda kwa vile anafeli. Anasema kuwa mto Limpopo unapatikana Misri
na Mto Zambezi upo Tanzania.
Samweli anatembea
kilomita sita asubuhi na jioni kwa miaka mine akihudhuria shule ya Busukalala kisha mwishowe anafeli
mtihani.
Babake Samweli anatarajia mwanawe kupita
mtihani na kupata alama bora. Anauza ng’ombe ili kufadhili elimu yake.
Dada zake
Samweli ambao ni Bilha na Mwajuma
wanasoma katika shule ya Busukalala kabla ya Samweli na wanapita mitihani yao
na kujiunga na elimu ya juu.
Babake Samweli
anakasirishwa na kufeli kwa Samweli. Anapompata Samweli kando ya bwawa baada ya
kuokolewa na mpita njia, anampa Samweli
Kamba ili ajitie kitanzi.
Samweli anajipendekeza
kwa mpenzi wake Nina kuwa bingwa
masomoni. Baadaye anamwona Nina miongoni mwa umati wa wanakijiji wanaomzuia
asijitose majini tena.
MADA ZINGINE ZILIZOSHUGHULIKIWA HUMU
HADITHI FUPI- TUMBO LISILOSHIBA
- WAHUSIKA KATIKA TUMBO LISILOSHIBA
- UFAAFU WA ANWANI TUMBO LISILOSHIBA
- MASWALI YA TUMBO LISILOSHIBA
RIWAYA CHOZI LA HERI
TAMTHILIA YA KIGOGO
Post your comment in the comment section below π