UFAAFU WA ANWANI-CHOZI LA HERI
Chozi ni matone ya maji yanayotoka kwenye jicho/macho ya
mtu kutokana na maumivu au furaha. Heri ni hali ya kuwa salama au hali ya
kupata jambo jema. Pia linamaanisha nafuu au afadhali. Maneno haya
yakiunganishwa pamoja yanaleta maana ya chozi linalomtoka mtu wakati hali
imakuwa salama au kupata jambo zuri. Au chozi analotoa mtu hali inapokuwa nafuu
au afadhali kwake.
Hoja zifuatazo zinathibitisha ufaafu wa
anwani hii ya Chozi la Heri.
1.
Familia ya mzee Mwimo Msubili inateseka kutokana na
udogo wa ardhi lakini hali inakuwa nzuri babake Ridhaa anapowahamisha wake zake
wawili wa mwisho, katika Msitu wa Heri.
Mmoja wa hawa ni mamake Ridhaa.
2.
Ridhaa anadhulumiwa
na wanafunzi wenzake shulenina kutukanwa kuwa yeye ni mfuata mvua lakini hali
inakuwa nzuri baada yamamake kwenda na kuzungumza na mwalimu mkuu na hali nii
kusitishwa.
3.
Eneo la Msitu wa Heri lilikuwa
kame (Kalahari) lakini inageuka kuwa nzuri baada ya Ridhaa kuwaletea maji ya
mabomba na eneo hilo kutwaa rangi ya kichani kiwiti.
4.
Hali inakiwa nsuri kwa Mzee Kedi Ridhaa anapoyathamini
masomo ya wapwa zake wawili.
5.
Mwekevu
anapoingia kwenye siasa anatusiwa na watu lakini hali hii inabadilika na kuwa
bora baada ya kushinda uchaguzi.
6.
Familia ya Kaizari inapata taabu anapovamiwa na wahuni lakini anapata heri
wakati jirani yake Tulia anapomsaidia
kutorokea palipo salama.
7.
Kaizari
anapovamiwa na mkewe Subira
kujeruhiwa na wananwe Lime na Mwanaheri kubakwa,
anapata heri Tulia anapojitolea
kumlindia nyumba isije ikaharibiwa na wahuni.
8.
Wakimbizi
wanapoteseka kambini kutokana na ukosefu wa chakula, misikiti na
makanisa yana waletea chakula na kuwafanya kuona heri.
9.
Wakimbizi
wanapoteseka kwa kulala vibandani, shirika la Makazi Bora linajitolea kuwajengea makao bora.
10. Selume anapotaabika
baada ya kukataliwa na mumewe Mwanzi, anakutana
na Ridhaa anayemsaidia kupata kazi ya uuguzi katika hospitali ya umma.
11. Kuchomwa kwa familia
ya Ridhaa kunamletea ugojwa wa shinikizo la damu lakini anasaidiwa kudhibiti
hali hiikutokana na huduma za ushauri na uelekezaji kutoka kwa wataalamu.
12. Lime na Mwanaheri wanabakwa
lakini wanapata heri abaada ya kutibiwa na wauguzi waliotumwa na mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali.
13. Ridhaa
anafuraha kupatana na mwanawe Mwangeka vita
vya baada ya uchaguzi vilivyozuka na kusababisha wanawe wengine pamoja na mkewe
Terry kuangamia.
14. Usalama
unazorota katika nchi ya Wahafidhina lakini
wanapata heri jamii ya kimataifa inapowasaidia kurejesha Amani.
15. Kiriri anamsaidia
mfanyikazi wake Kangata kuyadhamini
masomo ya binti zake wawili.
16. Riziki Immaculata, kitoto kinachotupwa
na mamake kwenye biwi la taka linapata heri kinapookolewa na Neema anayekipeleka katika kituo cha
watoto cha Benefactor.
17. Umulkeri amekuwa
akilia kwa kukosa wazazi lakini hali inakuwa bora kwake Apondi na Mwangeka wanapomchukua na kuishi naye kama mwana wao wa
kupanga.
18. Chanda Chema anataabika
kwa kukosa malezi lakini Bwana Tenge na
Bi. Kimai wanamchukua na kumlea kama mwanao.
19. Mwaliko anatekwa
nyara na nyumbani kwa Bi.Kangara lakini
anaokolewa na polisi na kupelekwa katika kituo cha Benefactor.
20. Mwangeka anafiwa
na mkewe Lily Nyamvula lakini
anapata heri anapowoa Apondi.
21. Apondi anafiwa
na mumewe aliyeenda kudumisha amani
lakini anapata nafuu anapoolewa na Mwangeka.
22. Hazina anataabika
barabarani kama ombaomba lakini anapata heri Umu anapompa pesa.
23. Umulkheri anapoteseka
mjini anabahatika kumpata Hazina
aliyempa pesa miaka mingi iliyopita. Hazina anamsaidia Umukheri.
24. Dick anapata
heri anapojinasua kutoka kwenye biashara ya kuuza dawa za kulevya na kuanza
biashara yake ya kuuza vifaa vya elekroniki.
25. Tuama anapoteza
damu nyingi baada ya kupashwa tohara lakini anapata heri anapotibiwa na kupona.
26. Neema anataabika
kwa kukosa mtoto lakini hali yake inaimarika anapofaulu kupewa Mwaliko na Mtawa Anastacia kutoka kituo
cha watoto cha Benefactor na kumlea
kama mtoto wa kupanga.
BONYEZA HAPA ILI KUSOMA MBINU REJESHI KATIKA CHOZI LA HERI
HUSA HAPA KWA 'O' NA 'AMBA' REJESHI
POST A COMMENT DOWN THERE π
HUSA HAPA KWA 'O' NA 'AMBA' REJESHI
POST A COMMENT DOWN THERE π